Hivi watoto wa kishua wanajisahau wapi, mpaka wazazi wanafariki ndo wanakumbuka shuka

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Yaani unakuta mtoto kipindi baba yake au wazazi wake wakiwa hai watoto wanakuwa hawaambiliki kabisa

1. Yaani ukimuelezea habari za shule hataki kusikiaa

2. Unakuta mtoto akipewa mtaji wa biashara anakulaa

3.Unakuta wazazi wanapamba kila akitafutiwa kazi afanye hataki unakuta anafanya kazi siku moja baada ya hapo anaachaa

4. Unakuta mzazi anambeleza soma basi hata chuo hataki anaona elimu kwake haina maana.

5. Akipewa biashara za baba yake asimamie au yeye ndo awe msimamizi anavuruga saa nyingine anaiba alafu siku tatu hataki tena ile kazii

Yaani inasikitika unaona mzazi anapamba kwa ajiri ya mtoto wake lakini mtoto mwenyewe sasa hasikii haambiliki. Lakini siku ambayo wazazi labda wanafariki au hawapo duniani ndo unaona sasa watoto wanangaika unashangaa wanauza Mali za familia, wanagombana mambo ya urisii mwishowe wengine wanaishia kutanga tanga na dunia wanabaki kuomba ombaaaa

Hivi tatizo linakuwa ni nini mpka vijana wanajisahau
 
Back
Top Bottom