Hivi watoto hawa wazazi wao hawalipi kodi!!!!

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
[h=1]WANAFUNZI WAFANYISHWA MTIHANI UWANJA WA MPIRA![/h]

Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro,akisimamia mtihani leo asubuhi.
...Wanafunzi wakiendelea na mtihani huo.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL, MOROGORO
KATIKA hali isiyo ya kawaida, wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro, leo asubuhi walinaswa na mtandao huu wakiwa wametapakaa kwenye uwanja wa mpira wakifanya mtihani huku wakiwa chini ya uangalizi mkali wa mwalimu wao.

Alipohojiwa na mwanidshi wa mtando huu juu ya wanafunzi hao kufanya mtihani kwenye uwanja huo, mwalimu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mazinda, alisema uongozi wa shule hiyo uliwapeleka wanafunzi hao kufanya mtihani huo uwanjani hapo kwa lengo la kuwapa nafasi ili wasiangaliane majibu.

"Tumeamua wafanye mtihani huu wa majaribio hapa kiwanjani kwa lengo la kuwapa uhuru zaidi kwani pale darasani huwa wanabanana, lakini sambamba na hilo, hali hii itasadia kwa wale wanafunzi wenye tabia ya kunakiri majibu kutoka kwa wenzao washindwe kufanya hivyo," alisema mwalimu huyo kwa kujiamini.

Hata hivyo, mwandishi wetu alishuhudia wanafunzi hao wakifanya mtihani huo kwa shida kubwa kwani walilazimika kuinama kwa muda wote wakiwa hapo.

Picha zaidi za tukio hilo:
 
Kufanya mtihani katika uwanja wa mpira jua kali, vumbi jingi, hakuna kivuli ubora wa elimu utokee wapi? Afisa wa elimu anakuja kuwatembelea na V8 ya milioni 250 kweli this is not fair at all!!!!
 
eeeeh mungu tunusuru na hii serikali mbofu mbofu ya CCM! napenda sana watoto nikiona wanateseka kwa nama yeyote ile napandwa na hasira mbaya. nna hasira sn na CCM kufanya sherehe ya miaka hamsini, hizo pesa si wangenunua madawati shule kibao tuu!!
 
Duh! Hii inasikitisha sana. Posho za Wabunge zikiondolewa na kuelekezwa katika kujenga madarasa basi tutaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa au kumaliza kabisa tatizo la kubanana madarasani.
 
Kufanya mtihani katika uwanja wa mpira jua kali, vumbi jingi, hakuna kivuli ubora wa elimu utokee wapi? Afisa wa elimu anakuja kuwatembelea na V8 ya milioni 250 kweli this is not fair at all!!!!

Tunaomba ushahidi wa hili.
 
Nape kama yuko humu aje atolee majibu. CCM hapo watajibalabuza hatatokea hata mmoja hapa kujibu hoja ila wanasubiri kutukana CDM tu! CCM ni wanafiki wakubwa kwa watatnzania wanawadanganya huku wakijua wanawadanganya. Sasa maisha bora ndo hayo? Jamani kuongoza nchi si mchezo jamani.
 
Tunaomba ushahidi wa hili.

Muulize waziri wako mkuu wa Nchi hii Toyota Landcruiser V8 inathamani ya shillingi ngapi ikisha kaangalie pale wizara ya elimu V8 zimejipanga ngapi na maafisa wa elimu wanaoenda kutembelea huko Mikoani huwa wanaendeshwa na magari gani.
 
Bwana tumeambiwa kompyuta ziankuja mpaka shule za msingi.

Ngeleja anabana umeme,

Walimu ndo hivyo,

Halmashauri hazina madawati

Tutegemee nini???????
 
Hao walimu nao hawaja tulia huwezi kmweka kwenye vumbi mtoto wa mwenzio eti kisa wasiangaliziane it sounds non sense
 
wanafunzi01.JPG wanafunzi 02.JPG

Wanafunzi wa shule ya msingi Bungo mkoani Morogoro wakifanya mtihani wa katikati ya muhula , Jamani kweli tutafika . Mungu aturehemu
 
labda ni mtihani wa majaribio, na wametengwa ili wajitegemee. na huo ni ubunifu wa mwalimu wa taaluma ili kukuza taaluma, ifanyiwe utafiti, kama inafaa irasmishwe tukiwa kwenye mchakato wa kuiadabisha serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom