Hivi watengeneza sera wanajua vijana wanaofeli kidato cha 4 siku hizi wanakwenda wapi?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Sera bora hutegemea yafuatayo;

1. Nini uhitaji wa hiyo SERA kwa jamii?

2. Ushirikishwaji wa wadau (wanajamii, wanasiasa, dini, & watekelezaji/implementors wa hiyo sera ili kupata maoni sahihi

3. Mchango wa tafiti kadhaa kuhusu hiyo SERA

4. Utekelezaji bora wa SERA husika

SIASA

Najua kuna kundi la kutetea chama tawala,lakini kundi sahihi kwa nchi ni lile linalotoa ninikifanyike.

Hii dhana ya shule ni upotezaji wa muda imewaingia hawa vijana kwa kasi. Yani betting na kampani hawaoni kama inapoteza muda (kiume), na wa (kike )hawaoni engage yao kwenye drama za dating na fashion trends kama upotezaji wa muda.

Policy makers +Teknolojia = hapa kazi tunayo

Mr Mkiki.
 
Halafu form 4 failure kwa nchi hii ni popo, si ndege si mnyama.

Na maanisha si Darasa la Saba wala si form4 kwa sababu hana cheti!

Na hakuna wa kuwasemea!
 
Unajua hili ni suala nyeti na la muhimu sana ambalo serikali ilipaswa iliangalie kwa umakini sana.

Huwa najiuliza sana wanafunzi wanaopata zero kwenye matokeo ya IV serikali ina mpango gani nao, VETA inawatosha? Bodaboda mtaani zitawatosha? Viwanda vipo vya kuwatosha?

Dah,
 
Serikali inatengeneza jeshi la watu wasio na kazi.

Siku za hivi karibuni matukio ya wizi yameongezeka sana.

Maisha magumu, biashara hakuna, ajira hakuna, hela hakuna, zamani watu waliambiwa wakalime, siku hizi watu wamejazana mijini hakuna mashamba.

Maisha ghali, watu wanataka kuishi maisha ya Facebook na instagram wakati hawana hela.

Utaona uhalifu unazidi tu.

Wiki chache nilikuwa naongea na rafiki yangu, wezi wamevunja kwake wameiba wakati yeye hayupo.

Leo pia rafiki yangu mwingine waneruka ukuta wameiba vitu kibao kwake.

Something's gotta give.

People have to eat.

Tunatengeneza jeshi la majambazi.
 
"Serikali inatengeneza Jeshi la watu wasio na kazi"

Note
 
Toa ushauri nini kifanyike nakusikiliza.
 
Zianzishe detention camps vijana wote wanaofeli shule wapelekwe huko waanzishiwe viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama wakati wa Hitler pia nashauri kodi ya kichwa irudishwe ili vijana wajitume kuchekecha akili zao.

Unakuta likijana lingine limemaliza shule ila lipo tu nyumbani linachagua kazi za kufanya halitaki kujiongeza kodi ya kichwa ikirudi naamini itaongeza hamasa kwa vijana kujituma aaaaghhh!!!
 
Note!!
 
I agree with you.
 
Naanza kwa kuunga mkono hoja.

Nashauri serikali ipanue vyuo vya ufundi stadi (VETA) na kujiunga huko isiwe tena hiari iwe LAZIMA kwa vijana wanaomaliza form 4 na kupata division sifuri au four.

Nikiwa na maana baada ya vijana kumaliza form 4 serikali ichuje, wakwenda form 5, wakwenda vyuo vya taaluma na wale wanaobaki wapangiwe vituo vya VETA kwenda huko.

Hii haitaacha kijana mzururaji na itatoa hamasa kwa wazazi kupeleka watoto wao huko.

Mfumo huu unaweza kuwekwa na kuunganishwa kuanzia pale kijana anapoingia form 4 achague yeye mwenyewe ikitokea anakwenda VETA angependa kusomea nini.

Ifikie hatua tutambue kufeli shule haimaanishi mtu hafai au hawezi kufanya makubwa.

Kuna vijana wengi wenye vipaji wanapotea kutokana na mifumo yetu kumuona hana thamani tena baada ya kufeli shule.

Naomba kuwasilisha.
 
Zianzishe detention camps vijana wote wanaofeli shule wapelekwe huko waanzishiwe viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama wakati wa Hitler pia nashauri kodi ya kichwa irudishwe ili vijana wajitume kuchekecha akili zao.

Unakuta likijana lingine limemaliza shule ila lipo tu nyumbani linachagua kazi za kufanya halitaki kujiongeza kodi ya kichwa ikirudi naamini itaongeza hamasa kwa vijana kujituma aaaaghhh!!!
Kama analishwa ugali kupata nguvu za kushinda vijiweni, kodi ya kichwa ikirejeshwa, pia atalipiwa.
 
Unajua hili ni suala nyeti na la muhimu sana ambalo serikali ilipaswa iliangalie kwa umakini sana.

Huwa najiuliza sana wanafunzi wanaopata zero kwenye matokeo ya IV serikali ina mpango gani nao, VETA inawatosha? Bodaboda mtaani zitawatosha? Viwanda vipo vya kuwatosha?

Dah,
Kwani wanaopata digrii wanaenda wapi ? Maana nao hawana ajira
 
Naunga mkono hoja ya mtoa mada,

Form four awe ana cheti au hana lkn akishakosa form 5 na vyuo vya taaluma tayari anakuwa hana kazi, hana utaalam wowote sawa na aliyeishia la4C...

Nini kifanyike?

1. Tuwe serious kidogo kwenye content inayofundishwa darasani, yaan mtu aliyesoma soil profile, poultry farming nk nk awe na ujuzi au stadi za kazi, tuone kama kweli ni muhimu vijana hawa kuendelea kukariri Kinjekitile kafa lini...,

2. Kuongezwe vyuo vya veta ( serikali na private) kama walivyosema wengine, Ingawa hili halitokei tuu, hata sahv vyuo vinaongezeka with needs..., ukienda Arusha na dar utakuta vyuo vingi vya utalii, hotelia na lugha kutokana na mahitaji ya sehem ile.
So hapa cha kufanya ni kuongeza mahitaji, kama ambavyo tumesema TZ ya viwanda, mana yake kwenye entire chain watahitajika veta wengi kuliko hata professionals..

-Panua bandari, improve miundombinu kwenda nchi jirani, punguza kodi kwa makampuni ya usafirishaji, Ila lazima waajiri madereva waTZ...., Yaani tuwe busy Kwa wingi wetu kuhudumu nchi zingine
-empower makampuni ya ndani ya utalii yafanye Hadi nchi zingine, yaan mtalii aanzie hapa kwenda kwingine, siyo anakuja kupitia Kenya, mfano
-tafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazolimwa nchini, hata soko likiyumba kuwe na bima za kusaidia, ili kilimo kiwe kitu kinacholipa, watu watajikuta wapo humo. Kwa sasa betting inalipa kuliko kulima mahindi.
KWA UJUMLA, TENGENEZA MAHITAJI, WATANZANIA WATACHANGAMKIA FURSA NAAMINI

3. JKT ni muhimu na lazima, nafikiri zingeongezwa, afu ziwezeshwe, baada ya yale mafunzo ya awali, kunakuwa na section ya ufundi stadi, wazalishe bidhaa zote zinazohitajika serikalini..., Afu serikali inawalipa ujira mdogo wakati wa kujifunza, akipata cheti anabaki Kwa ajira au anatembea mbele..
-Kwann tununue chaki
-Kwann serikali inunue mahindi ya kuweka kwenye ghala la taifa wakati mashamba ya jkt yamelala Tu pale
- shule hazina madawati
-ofisi hazina samani
- chaki za kuagiza China
- toothpick za Indiana
-viberiti sijui vya wapi

Nitaendelea
 
Back
Top Bottom