Amosi msigwa
Senior Member
- Jul 9, 2018
- 109
- 141
Wazo uli
Wazo ulilotoa naliunga mkono asilia 100, hakuna haja ya wanafunzi wote kwenda form six na vyuo vikuu ,wanafunzi wote wanaofeli na kupata wastni wa chini waende vyuo vya ufundi kwa maana hilo Tanaka ndilo linalo jenga uchumi was nchi.Naanza kwa kuunga mkono hoja.
Nashauri serikali ipanue vyuo vya ufundi stadi (VETA) na kujiunga huko isiwe tena hiari iwe LAZIMA kwa vijana wanaomaliza form 4 na kupata division sifuri au four.
Nikiwa na maana baada ya vijana kumaliza form 4 serikali ichuje, wakwenda form 5, wakwenda vyuo vya taaluma na wale wanaobaki wapangiwe vituo vya VETA kwenda huko.
Hii haitaacha kijana mzururaji na itatoa hamasa kwa wazazi kupeleka watoto wao huko.
Mfumo huu unaweza kuwekwa na kuunganishwa kuanzia pale kijana anapoingia form 4 achague yeye mwenyewe ikitokea anakwenda VETA angependa kusomea nini.
Ifikie hatua tutambue kufeli shule haimaanishi mtu hafai au hawezi kufanya makubwa.
Kuna vijana wengi wenye vipaji wanapotea kutokana na mifumo yetu kumuona hana thamani tena baada ya kufeli shule.
Naomba kuwasilisha.