Hivi watawala wanayafanyia kazi maoni ya watanzania au ndio wanategemea dora kuwasaidia?

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,316
216
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia maoni ya namna serikali hii inavyoendesha mambo yake. Pasipo na shaka nimegundua kuwa watanzania wamechoka na namna mambo yanavyoendeshwa hii ni kutokana na maoni wanayotoa. Ambacho kinanitia shaka ni namna watendaji wa serikali na chama tawala wanavyodharau maoni hayo na hivyo kutegemea dora pekee km njia ya mkato kwa matatizo yaliyopo
Maoni yanayotolewa jf ,kwenye mitandao mingine km mwananchi,kipima joto itv,makongamano km lile la jukwaa la katiba kwa uchache ni ishara tosha kwamba watanzania walio wengi wamechoka na namna mambo yanavyoendeshwa.
Ufike wakati sasa wanaoongoza dora waache watanzania waamue future yao na sio kuwalazimisha kufuata matakwa ya watawala ambao wengine hata saikologia na sociologia ya kuongoza hawana,mfano waziri wa mambo ya ndani anaposema bila yeye hakuna mwingine anaye weza kuongoza.
Je nawewe unaushauri gani kwa watawala ili waache mabavu kwani ndio njia pekee waliyobakia nayo na si diplomasia tena maana hawana jipya
 
Maoni yako naona yanamashiko sana. Ngoja tuunde tume ilikufuatilia kwa undani zaidi inaonekana unapoint.
 
Back
Top Bottom