Hivi watanzania wenzangu kweli hili haliwezekani???!!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Siku ya jumamosi wiki iliyopita rafiki yangu wa karibu sana alinipa mualiko wa ghafla ambao sikuutaraji. Pamoja na hali hiyo niliitikia wito. Pale nyumbani kwake tulikuwa wageni takribani 50 wake kwa waume. Sikujua undani wa mwaliko ule. Lakini baada ya sintofahamu ya muda mfupi baadae mwenyeji wetu alitupa undani wa mkusanyiko ule.

Kwa wengi waliokuwepo pale ilionekana kama ni kitu kipya ingawa mimi niliona ni aina ya mapinduzi tunayotakiwa kuyatarajia katika jamii yetu ya kitanzania. Yule mwenyeji alitueleza kuwa nia ya kutualika pale licha ya kula na kunywa lakini alitaka kupata msaada kutoka kwetu sisi ambao alituona ni watu wake wa karibu, tulioshibana nae hivyo tungemsaidia. Mtoto wake wa kiume ambae ni wa kwanza kuzaliwa amepata nafasi ya chuo nchini Scotland. Hii ina maana kuwa mzazi kwa nafasi yake hakuwa na uwezo sana kugharamia masomo ya kijana yule. na kwa maelezo yake alijaribu kupita hata katika taasisi za serikali e.g wizara na idara za serikali lakini bila mafanikio ili kupata msaada wa ufadhili hata ikibidi kwa mkopo. So tulitakiwa kumchangia ili kuongezea pale penye upungufu kwani alishakuwa na kiasi cha fedha lizoweza kupata.

Minong'ono niliyosikia ikienda chini kwa chini ilinishangaza sana, kwani mtu alihoji kuwa kama ni kuchangia ada ya mtoto kusoma nje ni jukumu la mzazi sio kuita watu eti na kuwapotezea muda wao???!! Watu tumekuwa wepesi sana wa kuchangia harusi kwa michango ya pesa nyingi tu, vipi elimu. Kwa kuwa tu kwenye harusi utahudhuria na kujilipa kwa njia ya vinywaji na maubwabwa basi?? Kifupi kikao hakikwenda vizuri mwisho wa kikao pledge zilizotoka pale Mmmmh!! Nashauri tuwe na harambee za kuchangia elimu sio miharusi tu..
 
Hiyo kitu ni nzuri na jamii inatakiwa ibadilike ni bora mtu uchangie elimu kuliko harusi mana huyo mtoto akipata hiyo elimu atakuja kulisaidia taifa.
 
Hiyo kitu ni nzuri na jamii inatakiwa ibadilike ni bora mtu uchangie elimu kuliko harusi mana huyo mtoto akipata hiyo elimu atakuja kulisaidia taifa.
...Nafurahi umeliona hilo ingawa yaelekea itatuchukua miaka mingi sana kuja kulielewa hili na hatimaye kutoa ushirikiano.
 
Wivu ni kitu kibaya sana. Wabongo hawachangii elimu kwa kuwa wanajua jamaa akiwa msomi ataweza kupoiga gape familia za wengine kirahisi. Tatizo ni wivu ulovuka mipaka
 
Tulijaribu sana kuchangia huko nyuma kwenye topic za vitchen party etc.. kwamba watanzania wamekuwa wanaendekeza mambo ya starehe kuliko elimu watu wanachanga fedha nyingi eti sijui kitchen party, kumtoa mwali, baby shower na upuuzi mwingine mwingi tu wakati muhimu ilikuwa ni kuchangia elimu. Serikali yetu imeshindwa kutusomesha basi tujisomeshe wenyewe sasa mtu anaomba msaada wa elimu ninyi mnamwona hazimo kweli tutafika???
 
Wivu ni kitu kibaya sana. Wabongo hawachangii elimu kwa kuwa wanajua jamaa akiwa msomi ataweza kupoiga gape familia za wengine kirahisi. Tatizo ni wivu ulovuka mipaka

Huenda wivu ikawa ni sababu, ila nahisi kuna suala lingine pia, vipaumbele vya kila familia. Kuna baadhi ya familia elimu si kipaumbele, mtoto anaweza kufaulu vyema na wazazi ama ndugu wasiwajibike kuchangia elimu yake, ingawa wanakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kimsingi tunahitaji mabadiliko makubwa sana.
 
Mimi nafikiri tuache kuchangia mambo ya harusi tuanze kuchangia elimu kama huyu aliyewaita ndugu na jamaa.
 
binafsi hii habari imenisikitisha sana! watu wamekuwa wepesi kuchangia mambo yasiyo na tija na kuyaacha yale ya msingi:-

Mfano;

  1. watu wanakuwa mstari wa mbele kuchangia harusi pesa nyingi sana, ikija kwenye suala la elimu kila mtu anatoa excuses zake
  2. Watu wanakuwa mstari wa mbele kuchangia msiba kuliko kumchangia mgonjwa ambaye huenda angepona kama angewezeshwa kulipia gharama za matibabu
watz inabidi tubadilike!
 
Hii harambe ya elimu inafanyika sana Kenya tuige vitu vizuri,kuhusu misiba nilishuhudia mgonjwa alieshindwa kulipiwa matibabu na kutolewa hospitali kwa kukosa mil 2 lakini alipofariki zikachangwa mil 3.2 kufanikisha msiba/mazishi.
 
Hii harambe ya elimu inafanyika sana Kenya tuige vitu vizuri,kuhusu misiba nilishuhudia mgonjwa alieshindwa kulipiwa matibabu na kutolewa hospitali kwa kukosa mil 2 lakini alipofariki zikachangwa mil 3.2 kufanikisha msiba/mazishi.
..Usemacho ni kweli tupu nadhani tunashindwa kupambanua mambo lipi lifanyike wakati gani tukiangalia gharama. Utashangaa mtu mwingine anakosa pesa ya kumlipia mtoto shule lakini inafika wakati eti anatafuta michango kwa ajili ya sherehe harusi, ubatizo, kipaimara, komunio etc etc. na ndio maana hao wakenya unaozungumzia uporoto wanatupiga bao kwenye mambo mengi tu na haya mambo ya jumuia ya afrika ya mashariki tunaishia kutetemeka tu!
 
Back
Top Bottom