Hivi watanzania wanahitaji ripoti kuhusu MCHANGA(makombo)au DHAHABU iliyozalishwa na migodi?

Sasa huo mchanga unadhani unakurupuka tu na kubadili makubaliano ya nyuma!?
Jamaa lazima watakuwa na contract ya kupeleka mchanga nje,na walikuwa wanapeleka baada ya Taasisi ya serikali iitwayo Tanzania Mineral Agency kuukagua mchanga huo na kutoka kibali,sasa tuone serikali inavikataaje vibali ilivyotoa yenyewe

Pia hawa jamaa huwezi kuwalazimisha wajenge mtambo wa kuchenjua mchanga wakati wanajua mgodi wenyewe hauna muda mrefu wa kuzalisha na hiyo sio sehemu ya mkataba
 
Ni kukurupuka tu Mkuu. Alikuwemo huyu ndani ya Serikali wakati wanasaini hii mikataba ya kifisadi na hakutia neno kupinga mikataba ile sasa anahangaika na mchanga!

Jamaa lazima watakuwa na contract ya kupeleka mchanga nje,na walikuwa wanapeleka baada ya Taasisi ya serikali iitwayo Tanzania Mineral Agency kuukagua mchanga huo na kutoka kibali,sasa tuone serikali inavikataaje vibali ilivyotoa yenyewe

Pia hawa jamaa huwezi kuwalazimisha wajenge mtambo wa kuchenjua mchanga wakati wanajua mgodi wenyewe hauna muda mrefu wa kuzalisha na hiyo sio sehemu ya mkataba
 
Mzungu asingewekeza mabilioni yake kupata hicho unachokisema,huo uwanja wa ndege mgodini ni kwq ajili ya kubeba Dhahabu,ingekuwa hivyo unavyosema,basi wasingewekeza
Lakini pia hawawezi export MCHANGA usio na kitu au wenye kitu kidogo, jamaa kaeleza vizuri tu na kitaalamu sijui kwanini hamuelewi.
Grade ya mchanga unaopatikana toka kwenye pit huwa ni ndogo sana, sasa ili kupunguza kupunguza hasara ya kusafirisha tonnage nyingi zenye grade ndogo(diluted ore) wanafanya initial processing ya ore na kupata "concentrate" yenye grade kubwa kuliko mchanga uliotoka shimoni.
Hivyo yale si MAKOMBO, Ule si UCHAFU kama ufikiriavyo.
Vitu vingine ni vya kitaalamu chunguza kwanza kabla ya kuandika maada na usiruhusu siasa ikutawale namna hii, ni mbaya hata kiafya. Kuhusu kiwanja mgodini kinasafirisha dhahabu itokayo kwenye gold ore ambayo recovery yake ni rahisi kwa kutumia mercury. Kuanzia sasa fahamu kuwa gold inapatikana katika namna(ores) tofauti ambazo complexity of processing nayo inakuwa tofauti.
BTW, ingawa si mimi mineral processing engineer taaluma yangu ni geology lakini nafahamu vyema formation na sifa za mineral ores mbalimbali.
Uchafu hausafirishi kwenda overseas, bali unaachwa sababu hauna faida kwao. Dhahabu yote wanakuwa wamesafisha na kupeleka kwao. Nenda mgodi wowote mafungu na mafungu ya uchafu huo uuzungumziawo.
 
Utakuwa ni zuzu wewe kuacha dhahabu ichukuliwe na hao wachukuaji na sisi kuambulia royalties ya 4% tu. Kama kweli tunataka kufaidika na rasilimali za nchi kwanini tusishupalie mikataba ya dhahabu yenyewe ili iboreshwe badala ya kung'ang'ana na mchanga!

Ni utaahira wa hali ya juu dhahabu inachukuliwa bure kabisa halafu tunapoteza muda na mchanga. Aliyeiita hii nchi kichwa cha mwendawazimu hakukosea kabisa.
We ndugu yakupasa ufahamu kuwa ule si MCHANGA bali gold concentrate(high grade ore)
Gold inapatikana kwa kiasi kikubwa in form of ores(mchanganyiko au compound ya gold na madini mengine kama copper) na ni nadra kuipata gold in pure state. Hivyo dhahabu inapatikana zaidi katika hali hio ya MCHANGA au unafikiri wakisha blast mwamba ndio basi wanatoka na dhahabu? Mchanga huo unahitaji processing ndugu ili kutenganisha mchanga "halisi" na dhahabu.
Mzungu hawezi kuwa chizi asafirishe tonnes za uchafu usio na FAIDA hata siku moja.
Na tunaibiwa sana wanapoenda kusafisha dhahabu hio kwao sababu wanacho-recover si gold pekee bali na madini mengine Yaliochanganyika na dhahabu.
Hivyo report hii ni ya muhimu sana kwa taifa.
Hata hivyo mikataba nayo ni tatizo.
 
Ninachojua au kudhani ninajua ni kwamba ripoti inayotolewa kesho ni kuhusu mchanga uliobaki baada ya Dhahabu nyingi kufyonzwa na kupelekwa ulaya!

Yaliyobaki ni makombo,yaani chakula kimeliwa,kinachofanywa ni kukokoa ukoko kuhakikisha sufuria halina kitu!

Je kwa nini tunatumia nguvu kugombania makombo na si Dhahabu ile nyingi inayokwenda? Yaani mwana mfalme anagombania makombo(mchanga)?

Tunahitaji juhudi kufaidi chakula halisi,mbona hatuambiwi Dhahabu halisi tumepunjwa wapi tunaishia kugombania makombo yanayodondoka meza kuu baada ya chakula kuliwa?

Nadhani ndugu zangu wabunge wa ccm wanajifunza matunda ya kusema "NDIYOOOOOOO........" Katika miswaada mbalimbali inayipelekwa bungeni na KUWAZOMEA wapinzani wanapotaka kuirekebisha ili iwe na maslahi kwa taifa.Mmoja wa miswada ni muswada wa Madini!!!!

NDIYOOOOO!!! Na kupongeza kwa asilimia 100 kumefanya migodi isilipe kodi kwa asilimia 100 na muda si mrefu migodi inaanza maandalizi ya kufunga biashara na kuondoka!! Wanaondoka wakituacha tumekula hasara asilimia 100!! Tena bila kufanya diversification......south Africa waliiwekeza faida katika Kilimo maeneo ya migodi ili kubalansi uchumi pale migodi inapofungwa,wanashinyanga watayumba migodi ikifungwa,zile baa,mahoteli,majumba yatakosa wakaaji kama ilivyo kwa miji ya russia

KWA WASIOJUA

Makombo ni mabaki ya chakula kilicholiwa,inaweza kuwa mifupa ya kuku yenye mabaki ya mate na vinyama kidogo,wali uliodondoka chini au kubaki kwenye sinia baada ya kushikwashikwa na wanaomega tonge
NATANGAZA HADHARANI KWAMBA SITATHUBUTU KUFUATILIA RIPOTI YA MAPANKI YA DHAHABU , EEE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE .
 
We ndugu yakupasa ufahamu kuwa ule si MCHANGA bali gold concentrate(high grade ore)
Gold inapatikana kwa kiasi kikubwa in form of ores(mchanganyiko au compund ya gold na madini mengine kama copper) na ni nadra kuipata gold in pure state. Hivyo dhahabu inapatikana zaidi katika hali hio ya MCHANGA au unafikiri wakisha blast mwamba ndio basi wanatoka na dhahabu? Mchanga huo unahitaji processing ndugu ili kutenganisha mchanga "halisi" na dhahabu.
Mzungu hawezi kuwa chizi asafirishe tonnes za uchafu usio na FAIDA hata siku moja.
Na tunaibiwa sana wanapoenda kusafisha dhahabu hio kwao sababu wanacho-recover si gold pekee bali na madini mengine Yaliochanganyika na dhahabu.
Hivyo report hii ni ya muhimu sana kwa taifa.
Hata hivyo mikataba nayo ni tatizo.
Ili kukwepa yote haya , kwanini msichimbe wenyewe hiyo dhahabu ili muambulie vyote ?
 
Kama watanzania na waafrika kwa ujumla hamtatambua matatizo yenu kwa undani wake kabisa mtabaki kuwa watu wa kulaumu na kulumbana tu hadi kiama.

Iko hivi;

Unakaribisha biashara mpya ndani ya nchi yako, unaita wafanyabiashara walio katika hiyo gemu na uzoefu wa hiyo biashara kwa miaka nenda rudi.

Inafika hatua ya kunegotiate deal, mfanyabiashara analeta jopo la wazee ambao wapo kwenye gemu ya hiyo biashara kwa miaka 40 hadi 50 wakiwa wameshika position za kila aina katika makampuni tofauti tofauti, wanaielewa hiyo biashara nje ndani, wana experience ya kila kitu.

Wewe katika negotiation panel unapeleka mawaziri na makatibu wa wizara, walimu wa vyuo vikuu na wachambuzi magazetini, hao ndio wanaenda kujadili deal na vile vizee vilivyokulia na kuzekea kwenye hiyo biashara. Wewe huna watu wenye operational experience ya hiyo biashara, basi angalau hata ukodi makampuni yenye uzoefu na hizo biashara wasimame badala yako katika kujadili hiyo mikataba kuliko kutegemea viongozi wa serikali walioenda kufanya ziara ya wiki moja migodini nje ya nchi.

Hapa vizee vile vinakaa tu vinawasikiliza mnavyojiunguza wenyewe, hamjui mnachokisema wala kukifanya.

Hapo ndipo tulipoangukia.

Kwa ninyi mlio katika mtazamo wa kisiasa zaidi endeleeni kulaumu na kutukana viongozi wa kisiasa, ukweli ni kwamba siasa zinatawala utaalamu katika Afrika yote kusini mwa jangwa la sahara
100%
 
Narudia tena NI UTAAHIRA MKUBWA kwa nchi kuacha dhahabu yake ichukuliwe bila kufaidika na kwenda kupoteza muda kwenye mchanga wa mabaki ya hiyo dhahabu husika. Huo mchanga KAMWE hauwezi kuwa na thamani kubwa kuliko dhahabu.

We ndugu yakupasa ufahamu kuwa ule si MCHANGA bali gold concentrate(high grade ore)
Gold inapatikana kwa kiasi kikubwa in form of ores(mchanganyiko au compund ya gold na madini mengine kama copper) na ni nadra kuipata gold in pure state. Hivyo dhahabu inapatikana zaidi katika hali hio ya MCHANGA au unafikiri wakisha blast mwamba ndio basi wanatoka na dhahabu? Mchanga huo unahitaji processing ndugu ili kutenganisha mchanga "halisi" na dhahabu.
Mzungu hawezi kuwa chizi asafirishe tonnes za uchafu usio na FAIDA hata siku moja.
Na tunaibiwa sana wanapoenda kusafisha dhahabu hio kwao sababu wanacho-recover si gold pekee bali na madini mengine Yaliochanganyika na dhahabu.
Hivyo report hii ni ya muhimu sana kwa taifa.
Hata hivyo mikataba nayo ni tatizo.
 
We ndugu yakupasa ufahamu kuwa ule si MCHANGA bali gold concentrate(high grade ore)
Gold inapatikana kwa kiasi kikubwa in form of ores(mchanganyiko au compund ya gold na madini mengine kama copper) na ni nadra kuipata gold in pure state. Hivyo dhahabu inapatikana zaidi katika hali hio ya MCHANGA au unafikiri wakisha blast mwamba ndio basi wanatoka na dhahabu? Mchanga huo unahitaji processing ndugu ili kutenganisha mchanga "halisi" na dhahabu.
Mzungu hawezi kuwa chizi asafirishe tonnes za uchafu usio na FAIDA hata siku moja.
Na tunaibiwa sana wanapoenda kusafisha dhahabu hio kwao sababu wanacho-recover si gold pekee bali na madini mengine Yaliochanganyika na dhahabu.
Hivyo report hii ni ya muhimu sana kwa taifa.
Hata hivyo mikataba nayo ni tatizo.
Wakala wa madini huchukua sample kabla ya kusafirishwa kwenda nje,na kupima kiwango cha makombo kilichomo,na TRA hulipwa chake kabisaaaa kabla mchanga haujasafirishwa
 
Ili kukwepa yote haya , kwanini msichimbe wenyewe hiyo dhahabu ili muambulie vyote ?
Sawa sawa ndugu nakubaliana na wewe. Hili ndilo suala ambalo tungelipaswa kufanya, ni vigumu sana tena sana kutegemea mwekezaji wa nje aje atumie 100% ya capital kwenye uwekezaji wa billions of money kuanzia exploration phase, development phase hadi production phase halafu utegemee eti akufaidishe wewe mwenye nchi. Hata kwangu ingekuwa ni ngumu.
They are always after profit na ndio maana wanatumia gharama kubwa pia kuajili highly experienced tax advisors ili kutafuta loopholes katika sheria za nchi husika ilikukwepa kodi.
Na tusitegemee kufaidika hata siku moja kwenye rasilimali hizi kama tusipobadirika na sisi kuwa na shares angalau 30% katika initial investments, hii kidogo itawabana kwa sababu na serikali nayo inakuwa la kusema katika uendeshaji wa company. Tunawapa mamlaka makubwa mno katika raslimali zetu.
Bila kufanya hivyo hata gas ya mtwara haiwezi kutufaidisha bali itafadisha nchi zao ambako pesa zote ndiko ziendako.
Kingine wataalamu wapo wanamaliza kila mwaka geologists, mineral processing engineers na mining engineers toka chuo cha madini, UDSM na UDOM. Lakini capital iko wapi na nchi yetu wanasema ni maskini haiwezi anzisha mradi mkubwa na wawekezaji wazawa wanaogopa.
 
Mkuu kuna uzi humu wa mtu aliyebobea katika fani hiyo hebu utafute na uusome kwa kituo.

Dhahabu yote inayochimbwa Buzwagi na Bulyanhulu iko katika mchanga mkuu, hakuna dhahabu inayopatikana ikiwa yenyewe tu kama jiwe. Jiolojia ya ukanda ule haina dhahabu ya namna hiyo.

Mawe yooote yanasagwa kwa vinu vikubwa na kuwa mchanga mdogo kabisa saizi ya vumbi na kisha kuanza kupita katika mitambo inayotenganisha dhahabu inayojiachia kutoka kwenye mchanga kwa njia ya gravity(free gold -isiyoshikamana na madini ya sulfide) kwa sababu ya density yake kubwa na nyingine inayoshindwa kujitoa kwenye sulfide minerals inawekewa kemikali inayoifanya ielee kwenye povu (Flotation process) na kisha kukwangua povu hilo, kulikamua na kukausha na hapo ndipo unapatikana huo mchanga wa dhahabu (Concentrate) ambao pia unakuwa na copper na silver.

Natumaini nimetumia lugha nyepesi ambayo utakuwa umeelewa...
 
Wakala wa madini huchukua sample kabla ya kusafirishwa kwenda nje,na kupima kiwango cha makombo kilichomo,na TRA hulipwa chake kabisaaaa kabla mchanga haujasafirishwa
Ndugu sidhani kama umenielewa yale si "makombo" kama ufikiriavyo
 
Kwenye Sakata la Mchanga wa Dhahabu- Nipo Tayari kunyongwa

Back
Top Bottom