Hivi watanzania tunajua kwamba vita dhidi yetu ni kali sana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi watanzania tunajua kwamba vita dhidi yetu ni kali sana?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jul 10, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watanzania na wanadamu kwa ujumla tuko vitani, lakini sidhani kama tuna hata chembe ya ufahamu kwamba tuko vitani.Tumezingirwa kabisa na ushindi wa vita hivi kwa sasa unaonekana ni mfinyu sana.

  Vita hivi vimechukua sura nyingi ,lakini kinacho windwa hasa ni maisha ya yetu.Sisi ndio adui.Vita viko katika maeneo yote yanayohusu maisha yetu.Nani asiyejua hatma ya kuharibika kwa uchumi uwe wa Tanzania au wa dunia.Mwisho wake ni nini, si vifo tuu.Na uharibifu wa afya za watu kupitia kwenye madawa,vyakula visivyo faa na nguo zenye sumu je; vifaa mbali mbali wanavyotumia wanadamu kama simu ambavyo vina madini yenye sumu na ambazo zinatoa mionzi yenye nia ya kuharibu uzazi wa mwanadamu na hatimaye kumfanya awe zezeta!

  Nani hajasikia mpango huu unaokuja wa kunyunyiza dawa majumbani ambao wanadai nia yake ni kutokomeza malaria, kumbe nia yake ni kumtokomeza mwanadamu.Nani asiyejua siri iliyojificha kwenye vyandarua vyenye dawa,water guard,chanjo,dawa za uzazi wa mpango,condom,uharibifu wa mazingira wa makusudi na hatimaye kumuingiza mwanadamu katika matatizo yasiyotamkika ya njaa nakadhalika.Ni mjinga tu atakaye ataamini kwamba upungufu wa mvua,matufani ya kutisha n.k. sehemu sehemu duniani ni bahati mbaya!Tanzania iko katika njaa ya kutisha na watu kila mahali wako kwenye mashaka makubwa.

  Magonjwa ya kutengenezwa kama HIV AIDS,Ebola, Swineflu n.k., kuna mjinga kweli asiyejua siri yake?Tangu lini ugonjwa kama Swineflu ukaua watu si zaidi ya 200 ukaitwa janga la dunia,huu si uchuro tu.Eti mwanafunzi katoka Uingereza kaja Tanzania kauleta.Hivi Heathrow Airport hakuna wataalam wa afya mpaka mwanafunzi huyo apite uwanjani humo bila kutambulika kwamba ana Swineflu.Jamani Uingereza, I don't believe it.Hivi sisi tunafavywa mbumbumbu sana eti.Nina hakika mambo haya yamepangwa.Imepangwa ili ionekane kwamba sasa ugonjwa umesambaa dunia nzima. Hawa watu wa WHO nao vipi, mpaka watamke kwamba Swineflu haudhibitiki tena?Kwani ilikuwaje wakadhibiti Polio na hata Smallpox wakati ule, na leo washindwe Mafua ya Nguruwe?Jamani hivi si vituko tu.Ninachojua ni kwamba haya ni matisho tu,to scare us to death,jambo ambalo nia yake ni kutudhibiti kisaikolojia.Ni vita kwa kutumia hofu.Hili ni tatizo la kupanga!In other words it's a hoax.

  Na huu uharibifu wa maadili yetu ambao umetuingiza katika matatizo makubwa ya kijamii nao vipi.Nani hajasikia ubakaji, watu wanavyo tembeza ngono bila hata aibu,watoto wasivyosikia wazazi wao,kina dada kutembea nusu uchi, madawa ya kulevya,mauaji ya albino,ushirikina,ujambazi n.k..Nani asiyejua huku kupenda pesa kuliko pindukia ambako kumetuletea ufisadi ambao sasa umechukua sura mbaya zaidi ya kutojali hata maisha ya watu.Wote tumeshuhudia matukio ya kutisha sana kule North Mara.Wananchi wanakufa kama panzi kwa kunywa maji yenye sumu kali za Sodium Cyanide na Mercury kutoka mgodini,huku serikali ikisema kwamba haina ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo,wakati independent organizations zimeshathibitisha hivyo.Vita ni kali sana.Hivi serikali inataka tuamini kwamba Mkemia Mkuu ndiye wa kuaminika.Nani anayayeweza kujichunguza mwenyewe kama sio uzandiki tu.

  Yapo matukio mengi mengine duniani ambayo mtu mwenye akili timamu ukiyachunguza ataona wazi kabisa kwamba yametengenezwa,sio ya bahati mbaya. Matukio kama ajali za ndege zinazotishia maisha ya watu sasa hivi,uvamizi wa meli kule kwenye Horn of Africa,vita vya Somalia na sehemu zingine duniani yamepangwa.Na nia yake ni kuweza kudhibiti watu kwa kutumia hofu. Television ndicho chombo kinachotumiwa sana kusambaza hofu hii kwa wanadamu,this is the last front.

  Kwa kumalizia nasema hiviii, vita dhidi yetu ni kali mno, na kama hatukuzinduka watatumaliza.We are already dying in terms of thousands kupitia kwenye mikakati yao mbali mbali michafu,dawa feki na za uzazi wa mpango,njaa,AIDS n.k.. Mungu atusaidie sana.
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Yeah, aliens hao. Mimi nilikutana nao jana usiku walishuka na UFO lao. Tuliongea kwa muda mrefu sana wakanieleza mambo mengi sana tu. Kitu cha ajabu walipoondoka sikukumbuka hata kitu kimoja tulichoongea!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Excuse me Dingi... what exactly is your point here?
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  soma Post mama yote uielewe kwanza. Jibu lipo hapo
   
Loading...