Hivi watanzania mna nini lakini ? Haya hawa wengine "questra holdings"

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
820
1,335
Haki mmelogwa..juzi nlizungumzia QNET haya nasikia kuna hawa wengine soma vile wanajitambulisha

Questra Holdings ni kampuni ya Uwekezaji.
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2009 ikijulikana kama SFG Group.
Mwaka 2013 ilibadilisha jina na kuitwa Questra Holdings.
Kampuni imesajiliwa Virgin Island - Great Britain
Makao Makuu ya Kampuni yapo Murcia, Spain.
Kampuni ina ofisi pia Moscow, Hong Kong, na ofisi nyingine imefunguliwa Madrid. Kuna mpango wa kufungua ofisi nyingi kote duniani mwaka 2017.
Questra ina manager 25 pamoja na wafanyakazi 158 katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya (EU).
Questra ina bima (Insurance fund) yenye thamani zaidi ya Euro 53 milioni.

Kampuni hii ina matawi mawili:-
1. Altantic Global Asset Management (AGAM) ambayo inahusika na uwekezaji.

2. Questra World ambayo inahusika na shughuli za utangazaji wa fursa za uwekezaji.

SHUGHULI ZA QUESTRA
1. Asset Management
2. Trust Management (kama UTT)
3. Project Management
4. Stocks
5. Kusaidia kampuni mpya kufanya IPO. Ilishazisaidia Facebook, Alibaba, na Tesla kufanya IPO.
6. Financial Instruments (Debentures)
7. Forex - Biashara ya Fedha
8. Wananunua Makampuni potential yanayo filisika, inayarekebisha na kuyauza kwa faida.

Pia inafanya kazi kwa karibu sana na Bloomberg ambao wanafanya Financial Data Analysis ulimwenguni

VIWANGO VYA VIFURUSHI VYA UWEKEZAJI - AGAM :-
1. White Tsh 234,000
Faida kwa
week. : 10,400
mwezi: 41,600

2. Yellow Tsh 702,000
Faida kwa
week : 31,850
mwezi: 127,400

3. Green Tsh 2,106,000
Faida kwa
week : 104,650
mwezi: 418,600

4. Blue Tsh 6,318,000
Faida kwa
week : 341,250
mwezi: 1,365,000

5. Red Tsh 18,954,000
Faida kwa
week : 1,066,000
mwezi: 4,264,000

6. Black Tsh 56,862,000
Faida kwa
week : 3,695,900
mwezi: 14,783,600

7. Indigo Tsh170,586,000
Faida kwa
week : 11,457,550
mwezi: 45,830,200

Package zingine nikama ifuatavyo:

8. VIP Tsh 260,000,000

9. VIP Gold Tsh 650,000,000

10. VIP Platinum Tsh1,300,000,000

Pesa utakazowekeza zitakwenda kufanya biashara kwenye maeneo mbalimbali yaliyotajwa hapo juu. Mfano rahisi mimi na wewe tusingeweza kuisaidia Facebook kufanya IPO, lakini kwa mtaji wako wa Tsh 2,106,000/= unaweza kushiriki kwenye biashara kubwa kama hizi duniani na ukalipwa faida kila wiki, kila mwezi.

UPEKEE WA QUESTRA

1. Fedha utakayowekeza utarudishiwa baada ya mkataba kuisha ikiwa utapenda kuichukua. Au unaweza kuiwekeza tena
2. Kampuni inafanya KYC - Know Your Customer kama tunavyofanya wakati wa kufungua account bank. Yaani kujaza taarifa zako na anwani yako ya ukweli ya makazi.

3. Ukishafanya KYC ukipenda kuletewa mkataba wako utaletewa.

4. Kampuni inakupa Bima ya fedha ulizowekeza ili kukuonyesha kwamba hutapoteza fedha zako hata kama kampuni itashindwa kufanya Biashara.

5.Hakuna makato ya mwezi wala makato ya kutransfer hela kwenda kwa mwenzio.


Hizo sifa sijaziona kwenye makampuni mengi ya uwekezaji niliyowahi kufanya nayo kazi na mengine mengi ninayoyafahamu. Hii ni kubwa kuliko.

Kama unaweka pesa bank ambako riba ni kidogo sana, kwa nini usiweke pesa zako sehemu ambayo faida ni kubwa marudufu !!
 
Thanks mkuu,..umeielezea vizur
Naomba ungeelezea na jinsi yakuisoma nakuiptia vzr kwa vtabu labda
Lets run it,
 
Yani midume na mafouz unampa midume mengine hela zako kizembe.

Bora kuning'niza mapoumbou (kutofanya kazi) tu
 
Vijana tumekuwa wavivu wa kufikili sana eti unatoa 234000 afu faida yako kwa wiki ni 10400 ebu tuweni unafikilia basi coz kwa Uo mtaji kwa wiki unaweza kuzalisha pesa zaidi ya iyo elfu kumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom