Hivi watanzania hatufahamu helicopter?

General mex

Senior Member
May 1, 2011
158
185
Mimi binafsi nimeshindwa kuelewa ina maana ni ushamba wetu au ni kukosa habari! Kwani vyombo vya habari sasa badala ya kueleza sera na hoja zinazotolewa na wagombea huko Igunga, imebakia kuelezea kwamba vyama vimeanza kutumia helicopter kwenye kampeni! Mimi binafsi sijaona kama hii ni habari ya kupewa kipaombele kama inavyoripotiwa na vyombo vya habari. Wana jf mtizamo wenu uko vipi? Nawasilisha.
 
Cha kushangaza ni nini? kwani hujui kuwa Tanzania ilikuwa kwenye kifungo cha mawasiliano kwa muda wote Nyerere aliokuwa madarakani?

Ametujaza ushamba na ujinga hata helikopta ni vitu vya ajabu. Sishangai kuwa helikopta ni vitu vya ajabu, kandambili tu zilikuwa ni vitu vya ajabu nchi nzima mpaka Nyerere alipoondoka.
 
Hujatoa scientific analysis. Issue sio Nyerere na yaliyopita kwani ni muda mrefu sana tangu nyerere aondoke. Hali inapahswa kuwa imebadirika. Watanzania vijijini wamo gizani ndio maana watu wanapata Kanga , kofia , vitenge etc wanamchagua mtu na si kwa sera au uwezo wake katika kuwatumikia. Hii inakuonyesha shallow thinking ya watanzania, wanahabari. Using helicopter should not be news at all. Wanahabari badirika
 
Sidhani kama ni ajabu, watu wamezoea kuiona katika picha sasa suala la kuiona "live" ndio yanawavuta watu wengi.
Kuna sehemu gari tu kuiona ni ajabu, sembuse helkopta??
 
Cha kushangaza ni nini? kwani hujui kuwa Tanzania ilikuwa kwenye kifungo cha mawasiliano kwa muda wote Nyerere aliokuwa madarakani?

Ametujaza ushamba na ujinga hata helikopta ni vitu vya ajabu. Sishangai kuwa helikopta ni vitu vya ajabu, kandambili tu zilikuwa ni vitu vya ajabu nchi nzima mpaka Nyerere alipoondoka.

Nyerere ametawala jumla ya miaka 25 umesema ametuweka kifungo cha mawasiliano,Mwinyi,Mkapa na Kikwete wametawala jumla ya zaidi ya miaka 25 bado tuko kwenye kifungo cha mawasiliano mpaka leo,hivyo basi kwa kutumia hiyo hoja yako inamaana serikali yote ya CCM imechangia kifungo hicho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom