Hivi watambua kuwa kuthubutu kutakutoa hapo ulipo

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,242
2,000
Natumai mko fiti wanajf wote,
Awali ya yote nawatakia sikukuu njema ya
XMASS na mwaka Mpya mwema. Ila nina jambo nataka kuwashirikisha kipindi hicho cha mwisho wa mwaka huu 2012 Si kila mtu anaweza kuvuka katika yale aliyoyatarajia tokea January mpaka December hii wala si wote walioweza kuvuka ng'ambo ya mto mwingine, kuna wengine waliishia njiani na kuona dhoruba kali ya mawimbi ya maji yakikwamisha yale waliojiwekea, walidhani kuwa ipo siku wangeweza kutatua hayo yaliyowakumba lakini mwishoe walioambulia patupu, habari hii ni kwa wale wote waliopigana na maisha na hawakutegemea kuona mlango wa kutokea katika shida, matatizo, barries, ama jambo lolote walilopanga mwaka huu. Ningependa kuwashauri na kuwatia moyo kuwa wasikate tamaa na kuona kuwa hatawerza tena lipo tumaini la kuvuka ng'ambo ya mto na kutoka hapo walipo, kitu ambacho ningeweza kuwakumbusha ni kuondoa dhana ya kushindwa kuthubutu kufanya kile ulichojiwekea mwaka huu au ile hali ya woga ya kutokuthubutu kutekeleza. Ukiondoa dhana hiyo potofu basi utaweza kutokea katika mlango wa pili wa mstakabali wa maisha yako nawe UTASHINDA vikwazo vilivyoko kwako. Napenda kuwatamkia baraka na amafanikio kwa wale walioona kuwa mwaka huu wameshindwa wajue kuna kuvuka kwa mwaka mwingine wa 2013 pale UTAKAPOTAMBUA NA KUTHUBUTU KUFANYA AU KUTENDA LILE ULILOLIPANGA ANZA SASA KUPANGA MATARAJIO YAKO BADO UJACHELEWA. UKITHUBUTU TU UTASHINDA KWA MWAKA MIWNGINE WA 2013. NAWATAKIA KHERI NA MAFANIKIO NA BARAKA MWAKA 2013.

N.B:
KAMA NILIPOST AU NILIANDIKA JAMBO / KITU KIKAKUUMIZA NA KUKUKWAZA MWANAJF RAFIKI YANGU WA MOYO NISAMEHE NA TUANZE UPYA UKURASA MWINGINE WA URAFIKI nawapenda
NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2013
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom