Hivi wasipopata wateja watakufa?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Niko hapa katikati ya jiji hili la Dar, kwenye Hoteli moja iliyobadilishwa jina hivi karibuni.
Niko a wageni wangu, na pembeni wapo kina dada wanaojiuza, maarufu kama makahaba. Wapo ambao wameshapata mawindo yao na wengine bado wapo macho juujuu wakisubiri wateja.
Nimejikuta nikijiwa na swali hili, Hivi, iwapo hawa wanawake wanaojiuza watatembea usiku kucha mitaani na kwenye Mahoteli haya makubwa na wasipate wanaume wa kununua hiyo bidhaa yao itakuwaje?
Mimi naamini haitazidi wiki moja watakuwa wameshatafuta shughuli nyingine ya kufanya. Sasa hapa Kahaba ni nani? Mnunuzi au muuzaji?
 
hiyo ni biashara kubwa sana duniani, na wengi wanoongea hadharani hawapendi ndio wanunuzi wakubwa, hata tuimbe kwa sauti namna gani hiyo itendelea kuweppo tu, bora waanze tu kukatwa kodi
 
@Gaga....... Hujajibu swali langu, Je Kahaba ni nani? Muuzaji au Mnunuzi?
 
hakuna kahaba hapo,hao ni watoa huduma muhimu sana, tena hawatoshelezi na ndo maana bei yao iko juu saaana, maoni yangu naomba tu waongezeke labda bei itashuka, kaka wateja ni wengi sana ndo maana ikifika saa 8 mmoja kesha pitiwa kama na watatu hivi, jana nilienda pale sinza nafikiri kila mtu anapajua, du bei ilikuwa noma sana kwani kupata huduma hadi asubuhi ilikuwa elfu 60,000 leo sijaenda lakini nitaenda kuchek, hata hivyo mambo yao nayakubali sana
 
Si pale africa sana kw pembeni?
 
Kazi ipo. Maana hata kama wanatumia kinga kuna kinga za mdomoni? Au biashara hairuhusu kissing? No wonder maambukizi yanaenda juu badala ya kushuka pamoja na ku invest a lot sijuhi TACAIDS sijuhi nini.

Hata wanaofanya hii biashara nje ya nchi they still feel guilty with what they are doing. Niliangalia documentary moja aljazeera wanahoji wadada wa Nigeria wanaojiuza nadhani Italy wanatia huruma sana.

Wanasema kuna mashangingi yanawaleta Ulaya na kuwalipia nauli then wanaandikishiana mkataba eti walipe up to 60,000 USD. Sasa unakuta hata ukahaba anakuwa anamfanyia alomleta maana mpaka kufikisha hicho kiasi si mchezo.

Wakaulizwa kwa nini msivunje huo mkataba. Wanamwambia mtangazaji "unajua juju wewe?" Tumekula kiapo kupitia juju tukivunja makubaliano basi juju itatuadhibu. Na kingine nasikia hao mashangingi yanayowapeleka ulaya yanatuma wahuni kwenda kufanya fujo nyumbani kwa binti Nigeria kama Binti atajifanya mjanja kuingia mtini.

Kwa kweli nyie wateja ndio wa kulaaniwa. Jueni si wadada wote wanafanya willingly kuna mambo ya human traffikcing.
 
hiyo ni biashara kubwa sana duniani, na wengi wanoongea hadharani hawapendi ndio wanunuzi wakubwa, hata tuimbe kwa sauti namna gani hiyo itendelea kuweppo tu, bora waanze tu kukatwa kodi
Ni biashara iliyokuwepo tangu miaka 2000 iliyopita

Ipigwe kodi tu, lets expand ur tax base!
 
Niko hapa katikati ya jiji hili la Dar, kwenye Hoteli moja iliyobadilishwa jina hivi karibuni.
Niko a wageni wangu, na pembeni wapo kina dada wanaojiuza, maarufu kama makahaba. Wapo ambao wameshapata mawindo yao na wengine bado wapo macho juujuu wakisubiri wateja.
Nimejikuta nikijiwa na swali hili, Hivi, iwapo hawa wanawake wanaojiuza watatembea usiku kucha mitaani na kwenye Mahoteli haya makubwa na wasipate wanaume wa kununua hiyo bidhaa yao itakuwaje?
Mimi naamini haitazidi wiki moja watakuwa wameshatafuta shughuli nyingine ya kufanya. Sasa hapa Kahaba ni nani? Mnunuzi au muuzaji?

Kahaba ni wote wawili Mnunuzi na muuzaji!
Haya ni matokeo ya kuwa na mfumo holela wa maisha kama Taifa lisilo na Maadili yake! Tumebaki kuwa Taifa lililo mfano wa Bendera isiyo na uelekeo mmoja, tumekuwa wa2 wa kuiga na kutenda tu NA SIYO TAIFA LA WA2 WENYE KUONA NA KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA!
 
Hivi nikisema kahaba ni Mwanaume nitakuwa nimekosea?
 
@Gaga....... Hujajibu swali langu, Je Kahaba ni nani? Muuzaji au Mnunuzi?

hapo naamini muuzaji maana ndo anayefanya biashara hiyo ... mnunuzi hawezi kuhukumiwa kwa vile katangaziwa biashara (kahamasishwa)
 
@BPM........Historia inatuonyesha kwamba ukahaba ulianza takriban miaka 2000 iliyopita, na hata katika vitabu vya dini zetu hizi za mapokeo Ukahaba umezungumziwa sana. Historia inaonyesha kwamba mwanamke hakuanza ukahaba, bali alilazimishwa na mfumo dume kuingia kwenye ukahaba........ kivipi..?
Mwanaume kwa kutumia nguvu aliyojipa alimlazimisha mwanamke ajiuze kwa faida yake. Wale wanaume waliokuwa akiwapata Makahaba wakati huo, ni watu ambao walikuwa na nguvu kifedha au kiutawala. na kadri Dunia inavyobadilika kiteknolojia, na ndivyo ukahaba unavyobadilika kutoka hatua moja hadi nyingine kulingana na mahali husika..........
Hivi sasa wanaume na pengine wanawake wameikuza hii biashara kwa kuwahadaa wanawake kutoka nchi masikini au kuwatoa vijijini na kuwasafirisha mbali kwa ajili ya kuwaweka kwenye madanguro kwa ajili ya kuwafanyisha biashara ya kuuza miili yao, wanaonufaika ni wanaume na sio wanawake hao................ Sasa hapa Kahaba ni nani?
 
Hivi nikisema kahaba ni Mwanaume nitakuwa nimekosea?
Mr. It seems ww hujatembea big cities around the Globe au hata internet unaweza search utaona Dar ni mji ambao una malaya wachache sana, nenda Nairobi, Addis Ababa, Morocco, Abuja, Pretoria, Joburg, ulaya usiseme ndio wana licence na wanalipia kodi kuwa malaya, Dar wachache mnooooo, ww mgeni sana nahisi
 
Hujanielewa wewe.......Sikuuliza juu ya statistics..........Nimeuliza kahaba ni nani kati ya muuzaji na mnunuzi, haya ya uwiano kati ya TZ na nchi nyingine ni mada mpya ambayo unatakiwa uianzishie Thread yake....................
Halafu kuhusu mimi kuwa sijatembea around the Globe, kunahusika vipi na swali langu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom