Elections 2010 Hivi wanawake wana haja ya kuipigia kura CCM?

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Ndugu zangu kabla ya kampeni kuanza nilipata bahati ya kutembelea hospital mbalimbali Huku kwetu kanda ya kaskazini. Ukienda utakuta wakina mama wanaosubiri kujifungua wamelala wawili kitanda kimoja yaani mzungu wa nne! Wakirudi majumbani kwao wanaenda na magonjwa mengine kutoka kwa watu walioshare nao vitanda. Nchi baada ya miaka karibia hamsini baada ya uhuru watu wanalala mzungu wa nne hospitali kusubiri kujifungua !

Sio mimi tu baada ya siku chache "chombo cha umma" TBC kilionyesha sehemu kadha wa kadha nchini hali ikiwa hiyo hiyo! nikapata wazo kwamba inawezekana nchi nzima iko hivyo.

Kwa kuwa wakina mama ni wapigaji wazuri wa kura, na kwa kuwa kutoipigia kura CCM watakuwa wameelezea kilio chao, je hawaoni kuwa ni wakati muafaka kuipenalize CCM?

NAOMBA KUWASILISHA.
 
wamuulize huyu mtoto:

Photos_Tanzania.jpg
 
ndugu zangu kabla ya kampeni kuanza nilipata bahati ya kutembelea hospital mbalimbali huku kwetu kanda ya kaskazini. Ukienda utakuta wakina mama wanaosubiri kujifungua wamelala wawili kitanda kimoja yaani mzungu wa nne! Wakirudi majumbani kwao wanaenda na magonjwa mengine kutoka kwa watu walioshare nao vitanda. Nchi baada ya miaka karibia hamsini baada ya uhuru watu wanalala mzungu wa nne hospitali kusubiri kujifungua !

Sio mimi tu baada ya siku chache "chombo cha umma" tbc kilionyesha sehemu kadha wa kadha nchini hali ikiwa hiyo hiyo! Nikapata wazo kwamba inawezekana nchi nzima iko hivyo.

Kwa kuwa wakina mama ni wapigaji wazuri wa kura, na kwa kuwa kutoipigia kura ccm watakuwa wameelezea kilio chao, je hawaoni kuwa ni wakati muafaka kuipenalize ccm?

Naomba kuwasilisha.

swali lako ni la msingi na ni zuri sana, jaribu pia kumuuliza mama yako/shangazi yako/dada yako/bibi yako/nyanya wako/mke wako na ndugu zako wanawake watakujibu kwa ufanisi na kiundani zaidi. Kila la kheri
 
Wakikumbuka wengi wa wanawake pia wanavyopata shida ya kusaka maji na kuni huko vijijini na katika baadhi ya miji! Ukizingatia wanawake wanatarajiwa kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura nguvu yao ni kubwa sana - wanatakiwa kuitumia nguvu hiyo vizuri kupata viongozi watakaowafaa.
 
Kina mama ni watu wavumilivu mno! Siasa za ugandamizaji kama zetu huwa zinaumiza kina mama zaidi, na ukiangalia ndio wanateseka mno tunapokuwa hatuna huduma ya maji(wanatembea umbali mrefu kwenda kuleta maji), tukikosa nguvu(energy- ndio wanakwenda kutafuta kuni mbali mno na kubeba mzigo mizito), tukinywa pombe sana, wao wanachukua jukumu la kulea familia hata kama ni kuchimba mizizi watoto wapate kula, tukichukua nyumba ndogo, hawakimbii watatunza watoto, na hata tukifukuzwa nyumba ndogo tukiwa hoi kabisa watatupokea kama vile hatujakosa na kutuhurumia, hata kule mahospitalini ndio wanalala chini na watoto wetu, wananyanyaswa wakati wa kujifungua nk.....MIDADA HIVI HAMFIKIRI HATA MARA MOJA TAABU ZOTE HIZO - MKATAMANI MABADILIKO? MABADILIKO AMBAYO YANAWEZA YAKALETA MATUMAINI MAPYA!?? AU MMELAANIWA!?

Najitolea kuwajibia maswali haya niliyotoa hapa juu, mnaaminiana mno kati yenu ( hivi nazungumza na wanawake wapi? of course naanza na dada zangu hapa JF). Wachache wenu hunyeshwa divai tamu na kujisahau ( kina Sofia Simba) nao huanza kuwarubuni hata mkasahau uchungu wote. Hebu changamkeni saa ya mabadiliko ni sasa sio kesho, AMKENI KUMEKUCHA!
 
Sielewi kinachowapumbaza watz wakati wa uchaguzi nini. Mtu eti miaka yote anaahidiwa mambo kemkem, kila miaka mitano wanarudia ahadi zilezile bila kutekeleza za kwanza, afu anachaguliwa. Sijui ni ujinga au....
 
Sio wanawake tu, mtu yeyote anayeishangilia CCM sioni kama ana akili timamu.
 
Sio wanawake tu, mtu yeyote anayeishangilia CCM sioni kama ana akili timamu.
Bila shaka wewe unahitaji kumuona daktari wa magonjwa ya akili (Psychiatrist).Kwa anayemfahamu amsaidie huyu jamaa maana muda si mrefu ataanza kuokota matabara majalalani.
 
Sielewi kinachowapumbaza watz wakati wa uchaguzi nini. Mtu eti miaka yote anaahidiwa mambo kemkem, kila miaka mitano wanarudia ahadi zilezile bila kutekeleza za kwanza, afu anachaguliwa. Sijui ni ujinga au....

Kanga na nyimbo za Komba na Kopa
 
Tatizo wanadhani kulala wawili au sometimes chini wanadhani ni haki yao hawajui kuwa ata iyo afya wanaweza ipata bure kwa kuondokana na CCM.
Mtoto anaezaliwa katika mazingira kama hayo what do you expect?

Nashukuru mungu mama yangu nshamwambia khanga,kofia,fulana chukua ila kura ni siri yako ikiwezekana wa upinzani hasa CHADEMA.
Akanijibu itatokea vita nkamwambia nani wa kuleta vita kwani CHADEMA ni jeshi?Akawa mpole.CCM hwa wanawalisha thumu watu kuwa vyama vingi ni vita
 
Sophia simba kawapiga mkwara wale wanawake wote ambao waume zao watakataa kuipigia kura ccm wawanyime unyumba (tendo la ndoa)...........kwa hiyo pamoja na hayo yoote lakini wanahaja ya kuipigia kura ccm kwani sophia simba kawapa ushauri wa maana......maisha mazuri hayataki haraka
 
Bila shaka wewe unahitaji kumuona daktari wa magonjwa ya akili (Psychiatrist).Kwa anayemfahamu amsaidie huyu jamaa maana muda si mrefu ataanza kuokota matabara majalalani.
Bwe he he..

Dalili naiona..
 
Ndugu zangu kabla ya kampeni kuanza nilipata bahati ya kutembelea hospital mbalimbali Huku kwetu kanda ya kaskazini. Ukienda utakuta wakina mama wanaosubiri kujifungua wamelala wawili kitanda kimoja yaani mzungu wa nne! Wakirudi majumbani kwao wanaenda na magonjwa mengine kutoka kwa watu walioshare nao vitanda. Nchi baada ya miaka karibia hamsini baada ya uhuru watu wanalala mzungu wa nne hospitali kusubiri kujifungua !

Sio mimi tu baada ya siku chache "chombo cha umma" TBC kilionyesha sehemu kadha wa kadha nchini hali ikiwa hiyo hiyo! nikapata wazo kwamba inawezekana nchi nzima iko hivyo.

Kwa kuwa wakina mama ni wapigaji wazuri wa kura, na kwa kuwa kutoipigia kura CCM watakuwa wameelezea kilio chao, je hawaoni kuwa ni wakati muafaka kuipenalize CCM?

NAOMBA KUWASILISHA.

Na sisi waume, watoto, wajomba, mababu, makaka...etc etc tuna sababu gani ya kuwapigia kura watu hao........????
 
Hivi wanawake pekee wangeipigia kura ccm ingeshinda kweli?!

Wanaume bebeni majukumu yenu
 
swali lako ni la msingi na ni zuri sana, jaribu pia kumuuliza mama yako/shangazi yako/dada yako/bibi yako/nyanya wako/mke wako na ndugu zako wanawake watakujibu kwa ufanisi na kiundani zaidi. Kila la kheri

Mke wangu kaniambia wanapigia sura nzuri ya Kikwete siyo ccm.
 
Back
Top Bottom