Hivi wanawake huwa mnasamehe kweli baada ya muda gani?

Kusamehe ni process mkuu,lakini inahitaji maamuzi binafsi kutoka ndani kwa kuwa inahusisha hisia.
Ni rahisi kusamehe au kutokusamehe kama aliyetendewa anaamini aina ya kosa lina uzito gani kwake.
Viwango vya kushikilia na kutokuachilia kwa muda gani watu wote wanatofautiana sio wanaume wala wanawake.Kwa upande wa dini issue ya kusamehe ni very sensitive.Kwa mfano kwenye Biblia inataja usamehe kabla ya jua kuzama(tafsiri rahisi ndani ya masaa kumi na mbili).
Kwanini?Kuna faida kubwa za kusamehe kwa muda mfupi kuliko kutokusamehe na kuachilia kwa muda mfupi,zipo sababu za kiroho,kiafya,kisaikolojia na kimahusiano pia.
 
Labda utuambie ni kosa gani..kuna makosa msamaha hautoki kirahisi

Hakuna kosa ambalo halisameheki ndio maana unaloshindwa kulisamehe wewe kuna mwingine anaweza kusamehe. Hapa ieleweke kusamehe sio ishu ya lazima inategemea na mtu japo ni muhimu kusamehe(ndio maana wengine wanaamua kuondoka jumla kwa kushindwa kusamehe au wanasamehe lakini kuendelea haiwezekani kutokana na kuwa hawezi kusahau na kukuamini tena). Umeshindwa kusamehe basi kaa nalo kimya moyoni kama unangoja muda ufike ulipize ngoja kimya kimya sio uniaminishe kuwa umenisamehe.
 
Kusamehe ni process mkuu,lakini inahitaji maamuzi binafsi kutoka ndani kwa kuwa inahusisha hisia.
Ni rahisi kusamehe au kutokusamehe kama aliyetendewa anaamini aina ya kosa lina uzito gani kwake.
Viwango vya kushikilia na kutokuachilia kwa muda gani watu wote wanatofautiana sio wanaume wala wanawake.Kwa upande wa dini issue ya kusamehe ni very sensitive.Kwa mfano kwenye Biblia inataja usamehe kabla ya jua kuzama(tafsiri rahisi ndani ya masaa kumi na mbili).
Kwanini?Kuna faida kubwa za kusamehe kwa muda mfupi kuliko kutokusamehe na kuachilia kwa muda mfupi,zipo sababu za kiroho,kiafya,kisaikolojia na kimahusiano pia.

Vizuri mkuu nimekuelewa sana hapo kwenye kisaikolojia na kiroho nnahusika pia imenitokea mara kadhaa. Mimi nikiwa sijasamehe huwa sina amani kabisa yani usiku silali kwa raha ni mfululizo wa ndoto mbaya mpaka ntakaposamehe, kwa hiyo kwa afya ya roho yangu kutoa msamaha n kitu muhimu sana.
Hii nilijifunza kipindi fulani nilikosewa sana na mtu na nikawa mwenye hasira kweli kweli ikawa shida sana kwangu hadi kutafuta msaada. Nilimtafuta ndugu yangu mmoja nikamueleza hali nnayopitia(sikumgusia hata kuhusu kukosewa kwangu). Nakumbuka aliniambia kama kuna mtu kakukosea msamehe hali itakuwa shwari. Baada ya mda nilifanya hivyo na nikawa healed na kuanzia hapo msamaha nnauthamini mno.
 
Mimi bwana nikitamka kwa mdomo wangu dhahiri nakuwa nimesamehe kweli na muda wa kuanza kukukumbushia sina na siwezi kufanya hivyo hata kama tukapishana tena na tena,.ila ukiniomba msamaha nikakuambia subiri kwanza au nipe muda basi nakuwa kwenye tafakuri hasa,.kwahiyo naweza kusamehe na kuachilia siku hiyo hiyo au baada ya muda fulani inategemea na moyo umelipokeaje jambo hilo..
Huwa sielewi neno nipe muda, maana it's like unasema ngoja nishibe ndo nkusamehe.

Mwambie mtu fresh lakin sitak mazoea
Mie nawazaga kumsamehe mtu inaclick kwanza kwenye logic zake then ndo maneno na vitendo..
 
Mimi nilikuaga na demu wangu mmoja kumbe ilikua kila kosa nalofanya yeye ana kidaftari anaandika! Siku ya siku yamemfika hapa nikashangaa mtu katoa daftari anaanza kunisomea makosa yangu yote, siku, tarehe na muda! Aisee japo tulikua tumegombana lakini nilishindwa kujizuia nikajikuta nimeangusha bonge la kicheko mpaka yeye mwenyewe akajishtukia ikabidi twende kitandani tukasameheane tu..
Atakuwa wa kishua ndo mambo yao hayo...
Kama si wa kishua kachukua tabia za telemundo
 
Nachoshindwa kuelewa ni hapo tu, unafanya jambo kubwa unamuumiza mtu sana kihisia, unavunjavunja moyo wake vipande vidogo vidogo, unamsaliti mtu aliyekuamini with all her life, kisha mnataka eti, akilala akiamka kila kitu kiwe tu sawa as if jambo ulilofanya ni dogo mno..! that's next to Never,

Kusamehe siyo jambo rahisi kama unavyofikiri, unatamani kuachilia lakini unajikuta ule uchungu na maumivu viko tu pale, vinaku haunt, kila ukifikiri unashindwa kuamini hivi ni huyu kweli kanitenda haya..??

Enwei, wataalamu wanasema sometimes it takes mpaka 2 years kusamehe kabisa na kuachilia kwa makosa makubwa kama usaliti,

Endelea kubadili mwenendo wako kuonesha kuwa umebadilika kabisa, show her you're not the very same person, atasamehe ila itachukua muda, unapaswa kuvumilia, na huwa hatufanyi makusudi wala, ni unajikuta tu maumivu yanakukereketa moyoni hasa..!!
Mimi makosa makubwa sisamehi kila mtu achukue time yake
 
Hakuna kosa ambalo halisameheki ndio maana unaloshindwa kulisamehe wewe kuna mwingine anaweza kusamehe. Hapa ieleweke kusamehe sio ishu ya lazima inategemea na mtu japo ni muhimu kusamehe(ndio maana wengine wanaamua kuondoka jumla kwa kushindwa kusamehe au wanasamehe lakini kuendelea haiwezekani kutokana na kuwa hawezi kusahau na kukuamini tena). Umeshindwa kusamehe basi kaa nalo kimya moyoni kama unangoja muda ufike ulipize ngoja kimya kimya sio uniaminishe kuwa umenisamehe.
Tukubaliane yapo makosa hayasameheki kwa wengine na kwa wengine yanasameheka usiseme tu hakuna lisilosameheka boss.
 
Habari za wikiendi wakuu, bila kupoteza wakati niende moja kwa moja kwa linalonitatiza. Kama mnavyojua kuwa kukosea ni sehemu ya maisha na mda mwingine ni njia moja wapo ya kujifunza(sihalalishi kukosea kuwa ni sahihi). Baada ya kutambua kosa ni kuomba samahani na hapa kuna kusamehewa/kutokusamehewa.

Inakera sana mtu anakuambia amekusamehe lakini anavyoenenda ni tofauti kabisa na msamaha wake. Ni furaha kusameheka lakini inahuzunisha zaidi msamaha unakuwa nusu nusu.

Hivi unasamehe lakini husahau( sio lazima kusahau na sion ubaya kwenye hili). Kusahau imekua ngumu kuna haja gani ya kumkumbushia kila mara kuhusu lile ulilolisamehe? Mkipishana kidogo wimbo ni ule ule kwa lile ulilowahi kukosea na ni miaka imepita. Hii tabia inanikera sana wakuu .

Binafsi nikishasamehe sina muda wa kukumbuka na kumuhubiria mtu alichowahi kunikosea na sio busara kufanya hivyo. Hii tabia nimeiona kwa Ke watatu niliowahi kuwa nao.

Sasa dada zangu wazuri kabisa huwa mnasamehe kweli baada ya mda gani? Au ndio huwa hakuna msamaha?

Na hapa kama nimekosea mnisamehe na kazi iendelee.

Wanacchana wa dizaini iyo wanakera mno mkuu. Utatamani uachanenae kwa vi2ko anavyokufanyia japo alishasamehe msamaha wa kinafiki.
 
Back
Top Bottom