Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 25,903
- 67,887
Habari za wikiendi wakuu, bila kupoteza wakati niende moja kwa moja kwa linalonitatiza. Kama mnavyojua kuwa kukosea ni sehemu ya maisha na mda mwingine ni njia moja wapo ya kujifunza(sihalalishi kukosea kuwa ni sahihi). Baada ya kutambua kosa ni kuomba samahani na hapa kuna kusamehewa/kutokusamehewa.
Inakera sana mtu anakuambia amekusamehe lakini anavyoenenda ni tofauti kabisa na msamaha wake. Ni furaha kusameheka lakini inahuzunisha zaidi msamaha unakuwa nusu nusu.
Hivi unasamehe lakini husahau( sio lazima kusahau na sion ubaya kwenye hili). Kusahau imekua ngumu kuna haja gani ya kumkumbushia kila mara kuhusu lile ulilolisamehe? Mkipishana kidogo wimbo ni ule ule kwa lile ulilowahi kukosea na ni miaka imepita. Hii tabia inanikera sana wakuu .
Binafsi nikishasamehe sina muda wa kukumbuka na kumuhubiria mtu alichowahi kunikosea na sio busara kufanya hivyo. Hii tabia nimeiona kwa Ke watatu niliowahi kuwa nao.
Sasa dada zangu wazuri kabisa huwa mnasamehe kweli baada ya mda gani? Au ndio huwa hakuna msamaha?
Na hapa kama nimekosea mnisamehe na kazi iendelee.