Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Nahisi nipo nje ya mada kidogo lakini sometimes wanawake tunajichanganya

Tunataka haki sawa kwa wote wakati huo huo tuna ile kauli mbiu yetu eti wanawake tukiwezeshwa tunaweza...SMH!😔😔

Kwanini tuhitaji kuwezeshwa wakati tuko na mikono na miguu miwili mixer ubongo kama wanaume
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.

Mara nyingi mambo ya mitandaoni yanakuwa tofauti na maisha halisi
 
Mimi siyo mjuzi ila ninaeleza kile ninacho elewa mimi.

Tunapoongelea usawa tunamaanisha tuondoe ule mnaouita mfumo dume kwamba binadamu wote ni sawa kitu ambacho si kweli. Mnaouita mfumo dume ni ule unaom favor mwanaume zaidi katika nafasi mbalimbali. Lakini kiukweli huo usawa mnaoulilia hauwezi kuja kutokea kwa sababu hata mkipewa nafasi bado hamtaweza kufanya vitu ambavyo mwanaume anafanya.

Mwanaume kaumbiwa roho ya ukakamavu, uvumilivu, na kujitoa muhanga katika hatari wakati huo mwanamke ana hali ya unyonge, kulia lia kila kitu na mwepesi kukata tamaa. Sasa mtu kama huyu anataka usawa na mwanaume.

Usawa tunaoulalamikia sisi ni ule wa kuingilia mipaka yetu achana hiyo uliyoongelea hapo.
 
Back
Top Bottom