Hivi wanaoshinikiza migomo duniani kwanini hawakai mstari wa mbele kwenye tukio?

neym8990a

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
244
196
Nimekaa chini nikatafakari, mara nyingi tumekuwa tukiona watu wakishinikiza wengine wafanye migomo. Utakuta kuna baadhi ya watu pengine hata viongozi wanaongelea migomo na kuwalisha watu sumu lakini hata mara moja hawa watu waga hawaonekani eneo la tukio, kwanini?

Kwanini umtamgulize mtoto wa mwingine akaumie kwa ajili ya kitu ambacho kitamnufaisha mwingine?

Ila yote tisa kumi ni zile mbwembwe za jana mitandaoni sikutegemea leo ingekuwa kimya..lol
 
Jiulize kwa nini George Bush na Tonny Blair hawakuwa msitari wa mbele kwenye vita vya Iraq, na kwa nini Nyerere hakuwa msitari wa mbele vita ya Uganda, ukipata jibu utajua kwa nini organizers wa maandamano hawakai msitari wa mbele.
 
ndio maana nimeona niulize waziwazi hapa
 
Mimi nilikuwa muongoza migomo shuleni, yaani kuwa mbele unatanguliza wafuasi tu.
 
Ndio maana kwa nchi kama bongo ambako binaadamu wameanza kushtuka ni vigumu sana kupata wafuasi wa mgomo.
 
Back
Top Bottom