Hivi wanaosema Kiswahili kitumike kufundishia kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu wanafikiria sawasawa kweli?

Sella turcica

Senior Member
Oct 13, 2020
104
193
Kwanza kabisa nikiri kuwa sikifahamu kiswahili pamoja na kuzaliwa Tanzania na kusoma hadi chuo kikuu. Ukitaka kujipima kama unakijua kiswahili au la basi set simu yako iwe kwa kiswahili kisha utapata majibu.

Kiswahili ni lugha ambayo inatuunganisha watanzania, hilo ni jambo jema kabisa, japo kuna watanzania baadhi hawajui kabisa kiswahili.

Mtanzania wa kawaida hawezi kuzungumza kiswahili pasi na kuchanganya na kingereza. Na hii ni katika mazungumzo ya vijiweni tu.

Sasa mtu unaposema eti kiswahili kitumike kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu nabaki kushangaa.

Yani mtu asome sheria kwa kiswahili!
Madaktari wasome pathology, pharmacology na surgery kwa kiswahili!

Kwenye research utakuta studies nyingi zimefanyika Ulaya, hapa Tanzania ni chache sana.

Sasa utafanya vipi literature review ilhali publications tunazotegemea ziko kwa kingereza?

Kwakweli hawa watu wanaopush hii agenda naona hawako serious kabisa.

Ningewaelewa kama wangesema kingereza kitumike kufundishia kuanzia elimu ya msingi hadi chuo, kiswahili kibaki kuwa somo. Nawasilisha.
 
wanakichaa

IMG-20220326-WA0009.jpg
 
Tafuteni vya Kwenu kwanza. Tatizo waafrika wengi Akili ndio zimeharibika siyo Lugha . Mmeshaharibiwa Akili mpaka mnaona Lugha Yenu et haifai

We unadhani masomo hayo Yote walioyaandika ni Wanaojua Kiingereza Tu. Hujui hata Vitabu vingine vimetafsiriwa
 
Kwa sisi bado sana, inahitaji nguvu kubwa sana kuwezesha hilo.

Anaesema hivyo hajafikiria mara mbili.
 
Back
Top Bottom