Hivi wanaopuuzia kuweza kuzungumza lugha ya kiingereza wanakumbuka katuba inasemaje juu ya lugha hiyo!!

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,858
2,348
katiba ya tanzania inatambua lugha mbili, nazo ni kiingereza na kiswahili

kwa wale wote wanaopuuzia kiingereza hebu rudini kwenye katiba mjifunze inasemaje kuhusu kiingereza
vinginevyo tutakuwa vituko,

watu wanatoka huko makwao kuja tanzania wakijua kuwa english is an official language here together with kiswahili,

halafu wanapopiga kambi humu nchini wanaanza kupata tabu na watu ambao kwa uvivu wao wa kujifunza lugha wanaona kiingereza kitiwe kapuni
 
katiba ni msahafu wa taifa wewe hufuatwa kama ulivyo, hubadilishwa kwa taratibu ndefu sana
Katiba hajasema lazima kuongea kiingereza ila imesema ni lugha inayotambulika kutumika kama kiswahili. Tunakoelekea tunataka Kiswahili kitambulike kimataifa ili tuachane na lugha ya kitumwa. Afrika ya Kusini walipambana kwa kila hali baada ya Makaburu kutaka lugha yao ya kikaburu itumike mashuleni ndiyo chimbuko la mauaji Soweto. Tufike sehemu tujitambue kwa kupenda tamaduni zetu na lugha yetu! Tufike sehemu mikataba inayohusu rasilimari zetu inaandika kwa lugha yetu. Angalia magari ya Kijapan wameandika kila kitu kwa lugha yao mbona bado yananunuliwa? Tukiendelea hivi kuabudu lugha zao hata kwenye rasilimari zetu wataendelea kutuibia tu kwa kuwa kwenye mikataba tutashindwa kujenga hoja kwa lugha zao!
 
Hao wanaopambana kiswahili kitumike kuanzia level zote za Elimu unajua watoto wao wanasoma wapi?
 
Back
Top Bottom