Hivi wanaofananishwa na Nyerere wanamuenzi kivitendo?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854



Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu hasa viongozi kufananishwa na Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere. Kila nikijaribu kufuatailia hotuba mbalimbali za wakati wa uhai wake naona utofauti mkubwa sana kati ya hao wanaofananishwa naye kiutendaji waziwazi. Mathalani suala la kulinda na kuheshimu katiba ya nchi ambalo alikuwa akilipigia kelele kila aliposimama.

Leo tunaambiwa hakuna siasa mpaka 2020 kinyume kabisa na matakwa ya sheria na katiba, tunapandikiziwa ubaguzi wa kimaeneo na uadui usio na sababu yani ukiwa mbunge wa jimbo A basi marufuku kwenda kwa jirani yako hata kuomba ushauri tu achilia mbali kuhemea.

Leo ukisema chochote unapotezwa au kuitwa msaliti, utaambiwa huna uzalendo na maneno mengine mabaya kisa tu umesema ambacho wakubwa hawapendi kusikia.

Nauliza sasa je wanaowafananisha hawa na baba wa taifa wanatumia vigezo vipi?
 
Back
Top Bottom