Hivi wananchi wa majimbo ya waheshimiwa Mwigulu, Rage, Nchimbi na Aeshi Wanajisikiaje?

MWananyati

Senior Member
Feb 3, 2011
160
52
Jamani wanajamvi nimefikiri nikaona ni bora tubarizi hapa juu ya matendo yanayoendelea ya waheshimiwa wa chama tawala.

Suala la nidhamu katika CCM inajulikana wazi kuwa halipo kwa sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni kushindwa kufanya maamuzi magumu ya kuokoa chama kutoka katika mikono ya 'wafadhili' (tunawaita mafisadi). Lakini ikumbukwe kuwa kuna kigogo mmoja alisema kuwa ndani ya CCM hakuna aliye msafi (wa tabia/mwenendo)

Hebu tuangalie hapa:
  1. UZINZI - Kutembea na mke wa mtu (Kuzini/kufanya uasherati) (Mwigulu Nchemba)
  2. KUVAMIA - Ujambazi (Aeshi & Bulaya)
  3. KUFYATUA RISASI - Ujambazi (Aeshi)
  4. KUTISHIA WATU MAISHA (kwa kutembea na silaha nje nje (Rage)
  5. KUIBA SANDUKU LA KURA - Uchakachuaji (Nchimbi)
  6. UONGO - Danganya wananchi (Aeshi na bulaya)
Binafsi nathibitisha kuwa CCM kimebaki kuwa chama cha waovu ambao wako radhi kufanya chochote ili kufanikisha malengo ya kuendelea kutawala, liwe jambo BAYA au HATARISHI kwa maisha yetu sie wananchi ambao tumewacagua kwa kura zet wanachi.


Uchokozi wanaofanya ni pamoja na KUTEMBEA NA WAKE ZETU. Huu ni udhalilishaji na namna gani ambao serikali ya cvhama tawala inatufanyia sie wananchi? kwa vile hizi ni TABIA NZURI KWAO, hawaoni umuhimu wowote wa kuchukua hatua kwa mtu kutembea na wake zetu. IGUNGA JAMANI, Mbona mwastahili pole?? TUMWAMINI NANI?
IGUNGA TOENI ADHABU STAHIKI KWA CCM. WAMEWADHALILISHA VYA KUTOSHA-WANAMUME KWA WANAWAKE


MATUMIZI ya silaha za moto yametawala sana kwa viongozi wa serikali hii. Ukiacha AEshi, hebu angalia Ditopile, Rage (bahati bulaya hakuamua kutoa yakwake). Hizi silaha ni kwa ajili ya kuua WANYAMA GANI WA MJINI IGUNGA? Makosa tuliyofanya 2010 tusiyarudie wana IGUNGA, WATATUMALIZA WAKIINGIA MADARAKANI. Aliyetkiwa kusimamia sheria anaamua yeye mwenyewe aichukue mkononi. kutoa roho kwao ni kitu kidogo (Angalia Andrew Chenge, Ditopile)


UCHAKACHUZI wa KURA na KULEWA MADARAKA. Watu hawa zaidi ya kutumia silaha za moto, lakini pia wapo tayari kupora demokrasia na haki ya msingi ya kila raia.Hii inatuonesha kuwa
  1. mpaka sasa wapo madarakani kwa hila za wizi wa haki za wananchi
  2. wataendelea KUIBA MALI ZA UMMA hadi WATAPOTOKA MADARAKANI
Sisi wananchi hatutakubali kuibiwa rasilimali zetu na majambazi wachache wa CCM. Tutazilinda kwa namna yoyote ile ili zinufaishe kizazi kijacho SI FAMILIA ZA VIGOGO WA CCM TU. Wana IGUNGA, mkeshe mkilina KURA ZENU kwa ajili ya kupambana na wezi wa mali za watoto wetu

UONGO NA KURUBUNI WANANCHI. Hili tumeliona tangu uchaguzi mkuu, AHADI HEWA ZISIZOTEKELEZEKA kwa namna yoyote ili wapate madaraka. Bulaya na Aeshi, wanadanganya wanachi waziwazi na CCM imekaa kimya ikionesha kukubaliana na VITENDO VYA UVAMIZI WA KUTUMIA SILAHA NA SUALA LA KUSEMA UONGO KWA JAMII. Inamaanisha kuwa huu ulikua ni mpango wao ili kuhujumu UKOMBOZI WA WANA-IGUNGA NA WATANZANIA KWA UJUMLA.
Haiwezekani mkawa kila siku mnatudanganya afu tukae kimya ilhali maisha yenu na yetu ni tofauti sana.


OMBI KWA WANA IGUNGA:

1. TUNATAKA UKOMBOZI WA TAIFA LETU TOKA KWA WAZINZI, WEZI NA WAFANYABIASHARA WALIOSHIRIKI KATIKA KUUZA MALI NA KUDHALILISHA UTU WETU. CHAGUENI CHADEMA kwa sababu mpaka sasa CUF ni sehemu ya CCM walioasi
2. kataeni dhulma kwa kuiadhibu ccm na wafanyakampeni wake. WAZOMEENI kwa kuwa ni wabadhirifu na wezi wa mali zetu. CHAGUENI UKOMBOZI CHADEMA


OMBI KWA WANANCHI WA MAJIMBO YA WAHESHIMIWA NCHIMBI, AESHI, MWIGULU, RAGE

1. Kuweni makini sana na hawa jamaa kwa sababu UHAI WENU kwao HAUNA MAANA zaidi ya UROHO WA MADARAKA
2. wAaambieni WAONDOKE, WAWAACHIE MAJIMBO YENU ILI MUPATE UKOMBOZI MANAKE MNATAWALIWA NA MAGAIDI NA MAFIA
3. AKINA BABA MUWE MAKINI NA WAKE ZENU KUSHIRIKI SIASA KWA MAANA TUMEONESHWA NINI KINAENDELEA NA HUWA KINAFANYIKA KATIKA VIKAO VYAO VYA NEC NA VINGINEVYO HUKO DODOMA. Hebu wewe baba fikiria, mkeo, umemtolea mahari, unamthamini, LEO HII ANAENDA KUCHAKACHULIWA KWA JINA LA CHAMA, INAINGIA AKILINI?

HAMIENI CHADEMA, SAA YA UKOMBOZI NI SASA!!!!


PEOPLES POWER!!
NGUVU YA UMMA NI CHANZO CHA MABADILIKO, UNGA MKONO CHADEMA TUKOMBOE NCHI YETU!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom