Hivi wanajeshi wa kike wa JWTZ wana kazi gani?

Salaam wana JF

Muda Fulani hivi kwenye ITV walionesha wanajeshi wa kike wa JWTZ wakiwa Kongo ikasemakana kwamba wameenda kulinda amani.Dada yangu anapenda sana kuwaona wanajeshi hasahasa wa JWTZ nikamwita aje kuwaona akaja mbiombio nikamwambia hawa wameenda kulinda amani kongo. Alinijibu kwa mshangao mkubwa sana akasema wanajeshi wa kike wa JWTZ hawaendagi vitani(ingawa ile haikuwa vita ila mapigano yanahusika).

Hivi ni kweli wanajeshi wa kike hawaendagi vitani na kama ni ndiyo je kazi yao kuu ni nini wakiwa jeshini?

Karibuni mnijuze zaidi

Tangia nimwone Msanii Ommy Dimpoz alivyopewa " drills " za uhakika pande za katikati ya Mwenge na Kawe sina hamu hata ya kuchangia threads za hawa jamaa na sana sana tu niwatakieni kila la kheri nyote mnaochangia.
 
Ukitaka kujua wanajeshi wa kike wana kazi gani..
Pita mitaa ya Lugalo au Kurasini, ukimuona mwanajeshi wa kike msimamishe, muulize hivi kazi zenu ni zipi jeshini..?
Ukiona hiyo itachukua muda, jaribu kumpokonya simu halafu mwambie kama ana mabavu aje kuichukua kwa nguvu..!!
ila hapo hakikisha umetembea na #bima, #kadi ya benki na #kitambulisho halali kuonesha ww ni mtanzania
 
Mmmh kazuri ,dah poda na lipstick jamani uwiii captain wewe utaua jamani,mi nilijua Jeshi hapaki poda.
Anaweza kupaka Mkuu lakini kwa mkao huo akiwa na combat(kwa mjeshi) inatia ukakasi. sidhan kama inaruhusiwa.
 
Mleta mada bwana, yaani umesha ainisha kazi yao kua wanaenda kulinda amani halafu, unakuja kutuuliza tena kazi yao?
 
Kazi zinazofanywa na wanaume pia zinafanywa na hao wa kike huko jeshini.
 
Mkiambiwa mwende hata jeshi la mgambo ili muelewe mambo hamuendi.
Wakati wa sherehe wale marubani wa ndege za kivita wanawake wanaoendesha ndege za vita za JWTZ unafikiri zile ndege ni saluni? Kikiwaka unafikiri huwa wanaenda nazo vitani kusuka nywele?
 
Wengi kutoa huduma kwa askari wale wanaojeruhiwa vitani. Ina maana ni wataalamu manesi au madokta.
 
Katika majeshi mengi wanawake huwa hawapelekwi kwenye mstari wa mapambano ila wanabaki kwenye shughuli mbalimbali za kuisaidia(support) au hata uongozi lakini mstari wa mbele ni askari wa kiume. Kimafunzo wote ni askari timamu.
 
f8ab2f1be9c4b3a90e80e5f8fa4d7bd6.jpg
mcheki mjeda wa nne kutoka kushoto kati ya hao waliosimama, unavyodondosha denda kwa mtoto mrembo
 
Salaam wana JF

Muda Fulani hivi kwenye ITV walionesha wanajeshi wa kike wa JWTZ wakiwa Kongo ikasemakana kwamba wameenda kulinda amani.Dada yangu anapenda sana kuwaona wanajeshi hasahasa wa JWTZ nikamwita aje kuwaona akaja mbiombio nikamwambia hawa wameenda kulinda amani kongo. Alinijibu kwa mshangao mkubwa sana akasema wanajeshi wa kike wa JWTZ hawaendagi vitani(ingawa ile haikuwa vita ila mapigano yanahusika).

Hivi ni kweli wanajeshi wa kike hawaendagi vitani na kama ni ndiyo je kazi yao kuu ni nini wakiwa jeshini?

Karibuni mnijuze zaidi

Wanafanya kazi zote kama wanaume.
 
Wewe unayejadil mambo yajeshi humu naomba uache aisee mana tunawezafika mbali ikawa shida... JWTZ wanaheshimika dunian kwauwezowao mkubwa wakivita so bilashaka majib umepata.. Naomba ukae kimya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom