Hivi wanachofanya wabunge wa CHADEMA ni haki kweli!?

"kweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha" waswahil husema hivyo ni mala ngap wabunge wa Ccm wamekuwa wakiropoka au kuzomea wenzao lakin hujalighusia hilo? Mbona umeangalia tu upande mmoja wa shilingi au wanayotenda wabunge wa Ccm ni sahih lakin kwa CDM si sahih?

Ni hayo tu mwisho nakuomba pia zingatia bias inayofanywa na mkalia kiti.
 
heb angalia kidogo mabunge ya nchi zengine, mfano japan. Wapinzani hawana mchezo na haki zao. CDM wanaifundisha magamba somo walilolisahau katika uongozi, challenge. Big up CDM, mkinyimwa haki itafteni kwa nguvu.
Makinda bora aachie hinyo ngazi asije akafa kwa presha.
 
Sawa sikatai spika was wrong na hakutenda haki lkn kwanini wapige kelele makofi wanaongea bila mpangilio wanaharibu utaratibu wa Bunge!

Ndugai ndiye aliyeharibu bunge kwa kuruhusu Lukuvi avunje kanuni. Mahali popote ukiona panaenda ovyo, mara nyingi chanzo ni uongozi mbovu.
 
Gamba likiomba mwongozo wa spika anapewa! Akiomba LEMA GODBLESS anaambiwa hana nidhamu!

Chadema wakigonga meza, eti inakuwa "pasipo 7bu" Magamba yakizomea aaah... "SAFI"!!
Sasa kwa hali hii cjui wewe ungesemaje au ungefanyaje ukiwa kama mbunge wa Upinzani!!

NB. Fuata haki siku zote!
 
Posho bado wanalipwa hawa wabunge wetu?......tunapoteza hela kwa mihuni isiyojali nini mwananchi wa kawaida anahitaji.They all suck!
 
Wabunge wa CDM wa kipindi hiki ni wingi wa Inzi tu, nakumbuka bunge la kipindi cha Dr Slaa, CDM walikuwa na wabunge wachache lakini wenye vision ya hali ya juu!

Hawa wa sasa ni Wahuni hawana nidhamu hata kidogo kama Lema na Lissu ni watu wa violence kila sehemu

Nidhamu ya aina gani kwa hao wahuni mkuu. Tuache ushabiki bila fikra na wananchi tumechoka sasa. Huwezi kuongoza kiujanjajanja na ulategemea watu wasi react.

MODUS OPERANDI ya Bunge letu ni to biased na huenda hata Mungu "HATUELEWI". Too ancient, ukandamizaji, ubabe, ujinga, upumbavu. ahh
 
Kwenye taarifa ya habari leo TBC1-8PM, mwanasheria mkuu wa serikali Werema amenukuliwa akikemea kile alichokiita wabunge kutofuata kanuni za bunge. Hata hivyo jambo kubwa alisema ni kuhusu maandamano. Amesema 'njia sahihi ya kupinga matekeo ya uchaguzi ni kwenda mahakamani'. Pamoja na kusema kuwa maandamo ni haki kisheria lakini kilichonistua ni pale aliposema 'tunaweza' kupitisha sheria itayokataza maandamano maeneo ambayo 'wenyewe' hawataki.

My take
Kimsingi ukitafakari ni kwamba Werema anasema serikali inataka kuweka sheria ya kuzuia maandamo unless kuwe na kibali cha 'wenyewe'. Cha kujiuliza, 'wenyewe' nani? RC?, DC? RPC? Mwenyekiti wa kijiji? nani hasa wanamuandaa ili awe ndio mtoa 'kibali cha maandamano? Na huyo atakayekuwa anatoa kibali atakuwa anawakilisha nani?

Werema kama mwanasheria wa serikali kapata wapi mamlaka ya kuonya wawikilishi wa wananchi bungeni wakati wanatimiza wajibu wao? Ni sawa kwa mwakilishi wa wananchi kupewa vitisho na mwanasheria mkuu? Hii siyo 'State Intimidation? Demakrasia ya aina gani hii?

Kama maandamano ni haki ya kisheria (katiba) kama alivyokiri Werema, yeye na serikali anayoiwakilisha kwa nini wanataka kufuta hii haki kwa wananchi? Watu wanaenda kwenye maandamano kwa hiari yao, sasa yeye Werema kinamkera nini? Kuna mtu amekuja kumuomba amgawie 'posho' ili apate nauli ya kwenda kwenye maandamano?

Ushauri wangu, kama ccm wanataka kuleta Tunisia basi watamke kuwa wanataka kuweka sheria ya kudhibiti maandamano. Itakula kwao!
 
Hivi ni sifa zipi zinamfanya mtu awe mwanasheria mkuu,
mbali ya kuwa mwanasheria?
 
Nasikitishwa sana na tabia wanazoonyesha wabunge wa chadema ya utovu wa nidhamu kuongea wakati spika hajaruhusu, kupiga makofi pasipo sababu, kuongea kwenye mic wakati umekaa. Mmetumwa na wananchi kwenda kuwakilisha majimbo yenu sina tutafuta majina. Watu wazima lakini Ovyoooooooooooooooooooo tena kamaTundu Lisu ndo nothing.
Nadhani bila shaka ni mwanachma mwaminifu wa GAMBA lakini naomba utambue kuwa Wabunge waupinzani wamekuwa wakiongoza kwa kutoa hoja zlizofanyiwa utafiti,lakini hoja hizi zimekuwa hazizingatiwi na wanachama wa GAMBA na hivyo bac kupitisha mambo kishabiki hali yakiwa na na athari kwako na kwangu KAMA HUTAMBUI MCHANGO WA LISSU NI TATIZO LAKO LA KUFIKIRI
 
ni wazi hata kama sheria zinakiukwa twendeni mbele tu tusirudi nyuma. ukiwa vitani kama vile vya Uganda ambavyo hata akina dada walikuwa mstari wa mbele ilikuwa ni moja tu, kata msitu. piga mzinga wala hujui adui wapo wangapi. naibu spika kaza buti. sukuma piga ili tushinde vita sisi wanachi wanyonge , akikikuka sheria sukuma nje, toa huko na akizidi fungia. akina dada na watoto tunaona hali ya amani kutoweka.CHADEMA irudi nyuma
Hali ilivyobungeni kwa sasa ni wazi
HUJUI ULILO ANDIKA HIVYO UNAPASWA KUSAMEHEWA,Hivi akili yako uliipa mda kufikiri wakutosha mpaka ukapata jibu kuwa CHADEMA ni chanzo cha upotevu amani? Na unafikiri amani ya nchi inapatikana kwa kushikilia sheria za kidikteta na za maspika madiktekta katika bunge.
 
mwanasheria mkuu wa serikali bila shaka ni mgonjwa matakumbuka alivyo pinga umuhimu wa katiba mpya sasa anapinga maandamano amesahau kuwa CCM nao wameanza maandamano,
 
Hivi ni sifa zipi zinamfanya mtu awe mwanasheria mkuu,
mbali ya kuwa mwanasheria?
inbidi katika utendaji wako wa kazi uwe mwanachama wa GAMBA wasirisiri mfano CHENGE halafu uwe mropokaji mzuri na unyeweza kuwa kibaraka wa GAMBA mzuri hiyo kaw postion ya bongo
 
Nasikitishwa sana na tabia wanazoonyesha wabunge wa chadema ya utovu wa nidhamu kuongea wakati spika hajaruhusu, kupiga makofi pasipo sababu, kuongea kwenye mic wakati umekaa. Mmetumwa na wananchi kwenda kuwakilisha majimbo yenu sina tutafuta majina. Watu wazima lakini Ovyoooooooooooooooooooo tena kamaTundu Lisu ndo nothing.

Sisi ndo tumewatuma wakafanye wanayoyafanya, sasa kama wewe Mbunge wako ni 'mjumbe ndiyo' usituonee wivu sisi wenye wabunge makini.

Kama sikosei wewe mbunge wako atakua ni Prof Majimarefu kama sii Lukuvi. Uchunguzi unaonyesha CCM wameshinda kwenye majimbo ya watu maskini,watu wasiokua na elimu/wajinga. Unatoka jimbo lipi mkuu?
 
Nasikitishwa sana na tabia wanazoonyesha wabunge wa chadema ya utovu wa nidhamu kuongea wakati spika hajaruhusu, kupiga makofi pasipo sababu, kuongea kwenye mic wakati umekaa. Mmetumwa na wananchi kwenda kuwakilisha majimbo yenu sina tutafuta majina. Watu wazima lakini Ovyoooooooooooooooooooo tena kamaTundu Lisu ndo nothing.

Usijali Chacha wa kwetu, yuko pacha wako humu anaitwa Marwa, duh ! Sina hakika nani kaanzisha huu mpango wa kuyatumia majina ya wana Tarime hasa baada ya Polisi kuwaibia maiti. Kama ni Nyangwine mwambieni kapotea njia lakini hapa watu hawadanganyiki kirahisi hivyo. Kila mtu anajua wapayukaji bungeni ni akina nani ingawaje wao hawachukuliwi hatua yoyote. Ukisikia Chadema wamepaza sauti kuna mawili - ama wanabughudhiwa na mikoromo ya akina Wasira wakichapa usingizi bungeni au wanalalamikia ubumbumbu wa wenyeviti wa vikao kama yule wa Dole.

Tatizo la Watanzania ni kuwa mmezoea vya kunyonga hivyo vya kuchinja vinawatia hofu na wasi wasi. Shuhudieni Raisi Obama wa Marekani avyokoromewa na hakuna anayelalama. Sasa hapa Ndugai kukumbushwa tu wajibu wake anaona Spika kadhalilishwa na kuanza kukurupuka kwa kuwatoa nje Wabunge. Huku mitaani tukilalamika kidogo tu, FFU hao, risasi mabomu ya machozi nje nje - je huyo Makinda angekuwa na maji ya kuwasha, si wabunge wangeloweshwa kinoma. Hilo ndilo taifa la Tanzania lenye amani na utulivu linalojivunia demokrasia ya vyama vingi.
 
Nasikitishwa sana na tabia wanazoonyesha wabunge wa chadema ya utovu wa nidhamu kuongea wakati spika hajaruhusu, kupiga makofi pasipo sababu, kuongea kwenye mic wakati umekaa. Mmetumwa na wananchi kwenda kuwakilisha majimbo yenu sina tutafuta majina. Watu wazima lakini Ovyoooooooooooooooooooo tena kamaTundu Lisu ndo nothing.

Mdai Haki Huonekana Mkorofi kwa wasiopenda haki..... Sikushangai sana Nghagwa Chacha you need to go back to school coz twajua wakulya walivyo na hasira but You Don't need to express it here Madame!
 
Back
Top Bottom