Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Wakati wa utawala wake wa awamu ya 4 Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete aliamua kuunda Tume ya kuratibu maoni ya wananchi ili Taifa lipate Katiba mpya.
Wakati anakabidhi majukumu hayo ya kuratibu maoni ya wananchi, Jakaya Kikwete alisema kuwa Katiba ya nchi yetu imepitwa na wakati kwa hiyo ilikuwa haikidhi mahitaji ya wakati huu, kwa kuwa ni Katiba ambayo tumeitumia kwa zaidi ya miaka 50 tokea tupate Uhuru, ingawa imekuwa ikiwekewa viraka mara kwa mara.
Kwa hiyo Rais mstaafu, Jakaya Kikwete alitamka wakati huo kuwa angetamani nchi yetu ipate Katiba mpya ambayo itatuvusha kwa miaka mingine 50 ijayo.
Tume ya Warioba ikakamilisha kazi yake ya kukusanya maoni ya wananchi kwa ufanisi mkubwa na ikakabidhi Rasimu hiyo ya Katiba kwa Rais huyo mstaafu Jakaya Kikwete.
Baada ya hapo likaundwa Bunge la Katiba ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kutoka CCM na likawa na wajumbe wachache kutoka vyama vya upinzani.
Kwenye Bunge hilo la Katiba ndipo kulipotokea "sekeseke" kubwa baada ya wajumbe hao kutoka CCM kuamua "kunyofoa" vipengele vingi vyenye maslahi mapana kwa Taifa na badala yake wakareplace na vipengele ambavyo vilikuwa vimeandaliwa pale mtaa wa Lumumba chini ya uandishi wa mwanasheria wao nguli Andrew Chenge, kwa maslahi ya chama chao cha CCM!
Kutokana na hali hiyo wajumbe wa Bunge hilo kutoka vyama vya upinzani wakaamua kususia Bunge hilo kwa kutoka kwenye Bunge hilo na kuwaachia wanaccm watupu ambao walipitisha Katiba yao pendekezwa ya CCM.
Na hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa kuundwa kwa Umoja wa vyama vya siasa vya UKAWA.
Hata hivyo hadi leo hii hiyo Katiba pendekezwa haijaweza kupigiwa kura ya maoni na wananchi kama takwa la kisheria linavyohitaji.
Kwa maana hiyo hadi hivi sasa nchi yetu haijaweza kuwa na Katiba mpya kama yalivyokuwa matarajio ya wananchi wengi kutokana na wabunge wa Bunge la Katiba wa kutoka CCM kuweka maslahi yao binafsi na ya chama chao na hivyo kukataa vipengele muhimu vilivyokuwa kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba ambavyo vilitokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa nchi nzima na Tume ya Warioba.
Kitu kingine ambacho kinatia uchungu zaidi ni kuwa mchakato mzima wa kutafuta Katiba mpya uligharimu pesa za walipa kodi kiasi cha shilingi zaidi ya bilioni 300 ambapo hatimaye Katiba hiyo ya Warioba ilitupwa kwenye "dustbin" na wabunge wa Bunge la Katiba kutoka CCM na Katiba yao waliyoipendekeza hadi hivi sasa nayo imebuma!
Tujaribu pia kuimagine hivi hizo pesa zipatazo shilingi bilioni 300 ambazo zimepotea bure kutokana na kuwa hadi hivi sasa hatijapata Katiba mpya........
Hivi pesa hizo kama zisingepotea kwenye matumizi hayo "mabovu" ya kuratibu maoni ya wananchi ambayo wanaccm waliyaona "rubbish" hivi pesa hizo zingeweza kufanya mambo mangapi muhimu kwa maslahi mapana kwa Taifa letu badala yake?
Sasa swali kubwa tunalowauliza wana CCM wanajisikiaje hivi sasa baada ya kuweka maslahi yao binafsi na ya chama chao mbele na kutojali maslahi mapana ya Taifa na hivyo kusababisha Taifa limekwama kupata Katiba mpya?