Hivi waliotumwa kumuua Lissu waliaminishwa wakaamini tatizo la Tanzania ni Lissu?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Najiuliza Ni doctrine gani waliyokuwa nayo wale waliokwenda kumfyatulia risasi Lissu. Najiuliza walidhani Lissu ndo tatizo la Tanzania ? Walidhani ugumu wao wa maisha unaletwa na Lissu? Waliaminishwa Nini Hadi wakaamua kuvaa nafsi ya mauaji?

Lakini najiuliza waliowatuma waliaminishwa na Nini kwamba anayewatuma yupo sahihi? Unapomtuma mtu kwenda kuua kiumbe kisicho na hasira unalipwa Nini au pumzi unayovuta inabadilika?

Leo Tundu yule yule waliotaka kumuua ndiyo anayewatetea Watanzania kuliko waliowatuma. Naamini hata kwa Mbowe wapo watu nchi imewashinda wanataka Askari waamini tatizo ni Mbowe. Unakabidhiwa rasilimali zote usimamie unajikita kupambana na wananchi, polisi jitafakarini mjiulize tatizo ni hao mnaowakamata Hadi nyumba za ibqda?

Lisu awafundishe mnaotumwa kujiuliza endapo mnachotumwa kina tija? Unakwenda kuua ukidhani utapata cheo kesho wanakufukuza Kama mbwa. Tendeni haki achaneni na wanasiasa wenye uchu wa kumwaga damu, siku za wamwaga damu si nyingi jitafakarini
 
Yule wa muhimbili aliepigwa ganzi ya jino akavimba ubongo umemsahau? Na je nyauli......NGO ambae ndio Master mind hujamsikia kapata ajali miguu kwanyuu
huyo wa muhimbili hebu ongeza malelezo.Nyaul....NGO nilisikia amepata ajali bagamoyo kavunjika miguu..hivi yupo hai?
 
Lissu si tatizo la taifa bali lake mwenyewe.Hata hivyo, kutoa uhai wa mtu si jambo jema na ujinga na ushamba pia.
 
huyo wa muhimbili hebu ongeza malelezo.Nyaul....NGO nilisikia amepata ajali bagamoyo kavunjika miguu..hivi yupo hai?
Nyau mhitimu wa Musoma Alliance 1983 HGL then akajoin NASACO TANGA, 1987 akachukua maamuzi magumu na kujiunga na idara.
Muda Sasa sijamsikia.
 
..halafu walioshiriki unyama ule baadhi wamekufa na Lissu bado anadunda.

..sasa jiulize waliobaki wakienda kuwazika washirika wa jaribio lile wanajisikiaje?
Hivi wakioshangilia kifo cha Magu waliamini tatizo ni Magu?

Alafu cha ajabu baada ya kifo cha Magu wamepata kibano kikali zaidi ya kile
 
Hivi wakioshangilia kifo cha Magu waliamini tatizo ni Magu?

Alafu cha ajabu baada ya kifo cha Magu wamepata kibano kikali zaidi ya kile

..huenda waliamini Magu ndiye mastermind.

..Na furaha yao huenda iko palepale kwasababu wanaamini aliyetuma walenga shabaha ni Magu.
 
Back
Top Bottom