Hivi! waliotoka ni UKAWA? au waliotoka ni CCM?

Kifuna

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
434
225
Pengine tungepata uchambuzi wa neno kutoka " kwa ninavyoona mimi waliotoka ni wajumbe wa bunge la katiba wa CCM ila kwa sababu wana nguvu na ubabe uliokomaa ndio maana wameng'ang'ania mjengoni lakini kimsingi wametoka kabisaa! hawa UKAWA hawajatoka kwa maana wanaitetea Rasimu ya Mzee Warioba. Lakini CCM wana rasimu yao hilo tu linatosha kuwaomba warudi kwenye MADA sio mjengoni! Tafakari hili kama kutoka ni kwenye Mjengo wa Bunge UKAWA wametoka lakini kama kutoka ni kwenye MADA au HOJA iliyoletwa basi CCM wametoka" Bado nauliza ni nani katoka?
 
yegowasu

Senior Member
Jun 29, 2014
141
0
Vema. Chama chetu ndo kimetoka ndani ya bunge kwa kushindwa kujadili rssimu ya serikali 3.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,384
2,000
Tukiiweka hivyo kwa maana ya hoja waliuoyoka ni Wabunge wa Chama Chetu cha Mafisadi.
 
bhiseko

JF-Expert Member
May 9, 2014
387
250
Pengine tungepata uchambuzi wa neno kutoka " kwa ninavyoona mimi waliotoka ni wajumbe wa bunge la katiba wa CCM ila kwa sababu wana nguvu na ubabe uliokomaa ndio maana wameng'ang'ania mjengoni lakini kimsingi wametoka kabisaa! hawa UKAWA hawajatoka kwa maana wanaitetea Rasimu ya Mzee Warioba. Lakini CCM wana rasimu yao hilo tu linatosha kuwaomba warudi kwenye MADA sio mjengoni! Tafakari hili kama kutoka ni kwenye Mjengo wa Bunge UKAWA wametoka lakini kama kutoka ni kwenye MADA au HOJA iliyoletwa basi CCM wametoka" Bado nauliza ni nani katoka?
CCM ndo WALIYOTOKA NJE YA HOJA RASMI. Dhana ya kutoka mjengoni imejikta katika mawazo MFU. Mara nyingi watu wenye mtazamo wa mawazo ya namna hii huwa ni wale wenye sifa ya "NDIYO MZEE". Kwao BAYA huwa ZURI ili mradi tu limesemwa na mkubwa WAO. Na zuru huwa ni BAYA KWAO ili mradi tu mkubwa wao kasema. Viongozi wa namna hii huwa hawasumbui AKILI ZAO kabisa ILI KUCHAKATA HOJA RASMISHWA na badala hubaki wakusubiri mkubwa wao kasema nini ili na wao wapate KUDANDIA KAMA KONDA WA DALADALA anayesubiri gari GARI LIONDOKE ILI ARUKIE PASIPOKUJUA KUWA ANAHATARISHA MAISHA YAKE.
Narudia kukuunga mkono kwamba "CCM NA KUNDI LAO LA WANAOJIITA WENGI WALITOKA NJE YA HOJA ILIYOKUWA MBELE YAO KIMANTIKI NA VIWILI WILI VYAO VIKABAKIA VIKALIA VITU VYA MJENGONI".
Aibu yao ya mwaka 2014 kwa WATANZANIA NA WATANGANYIKA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom