Hivi wale wahariri waliokutana na Al Adawi walikuwa wametekwa kwa mtutu?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Wajameni, mimi nashangaa jinsi hawa wahariri wa magazeti yetu jinsi walivyonyoroshwa na huyu mwekezaji (aka Ali Hadaiwi), nijuavyo mimi waandishi wa habari ni watundu sana na huweza kumpiga picha mtu bila hata yeye kujua kuwa kapigwa picha au karekodiwa. Sasa kinacho nishangaza mimi ni jinsi hawa wahariri walivyotii amri ya kutompiga picha au kurekodi sauti ya huyu mwekezeji, je walikuwa chini ya ulinzi wa mtutu wa bunduki?

Au ni unyenyekevu na usikivu tu wa Watanzania??
 
Kwa kweli kabisa walizidiwa kwa hoja. Kwani team aliyokuja nayo ambao ndio wasaidizi wake walikuwa mahiri na waliobobea sana kiasi hata wahariri wetu walishindwa hata kujitetea.
 
picha yake we inakusaidia nini?alichokisema kinatosha,ukimuona inabadili ukweli wa mambo?:decision:
 
picha yake we inakusaidia nini?alichokisema kinatosha,ukimuona inabadili ukweli wa mambo?:decision:

Picha yake na sauti yake vingesaidia kupata ukweli kuwa aliyekuwa anaongea ni Al Adawi na halikuwa gugu maji kama ambavyo watu wanadai, ingesaidia pia kumsuta iwapo atakuja kukataa baadaye kuwa hakuwa kuongea nao. Ikumbukwe alishawahi kuikana Dowans alipoongea na KHLN (mwanakijiji) na kumekuwepo na mikanganyiko mingi kuwahusu wamiliki halali wa kampuni hii tata
 
picha yake we inakusaidia nini?alichokisema kinatosha,ukimuona inabadili ukweli wa mambo?:decision:

Nilifikiri ni mimi tu nimewaza hivi kumbe wengi, hona sasa mdada Dyslexia unavyoaibika, kwani uko gazeti gani vile?? uandihsi wa habari ni kila kitu, kama sivyo tusiwe na TV, camera n.k! hata wewe toa picha yako ya uongo kwenye avatar yako! huna hoja dada!
 
had the same thought kama walikuwa chini ya ulinzi na kamera zao ziliwekewa UVC ili zisifanye kazi
 
Wajameni, mimi nashangaa jinsi hawa wahariri wa magazeti yetu jinsi walivyonyoroshwa na huyu mwekezaji (aka Ali Hadaiwi), nijuavyo mimi waandishi wa habari ni watundu sana na huweza kumpiga picha mtu bila hata yeye kujua kuwa kapigwa picha au karekodiwa. Sasa kinacho nishangaza mimi ni jinsi hawa wahariri walivyotii amri ya kutompiga picha au kurekodi sauti ya huyu mwekezeji, je walikuwa chini ya ulinzi wa mtutu wa bunduki?

Au ni unyenyekevu na usikivu tu wa Watanzania??
183692_1727629282539_1592647395_1637518_5276786_n.jpg

walikuwa hivyo.....
 
Nchi imavamiwa na mamuluki kwa angalia wahariri walioshirikishwa ni kutoka baadhi ya vyombo vya habari hapo hapo wakapewa masharti ya kibabe ambayo waliyaridhia bila kuhoji Najiuliza hivi wahariri waliambiwa kabla kuwa kamera na vinasa sauti vilikuwa haviruhusiwi au walifika na vitendeakazi vyao wakalazimishwa kuviacha nje ya ukumbi wa mikutano Bila kufanya ajizi wahariri wanaojali utu wao wangeonyesha jeuri yao kwa kusitisha mahojiano na tapeli Al Adawi kama ishara dharau iliyonyeshwa na mwaarabu huyo
 
Waambieni wawagawie kidogo walichopewa, njaa zitawaua ""wahariri-waandishi uchwara""
 
Lakini kwa uopande mwingine, maadili ya uandishi yanataka mwandishi kuheshimu matakwa ya mtu (kama hataki kupigwa picha, kutajwa jina lake kama chanzo cha habari n.k). Lakini kwa kujali kazi yao, baadhi ya magazeti yalifanya kila juhudi na kuipata picha ya bwana huyo katika mazingira mengine.
Kumbuka kuwa mwarabu huyu alitembelea ofisini kwa makamu wa rais ambako nako alitoa sharti la kutopigwa picha na waliheshimu hilo. Au na mofisini kwa makamu wa rais nako walichukua kitu kidogo?
 
Wajameni, mimi nashangaa jinsi hawa wahariri wa magazeti yetu jinsi walivyonyoroshwa na huyu mwekezaji (aka Ali Hadaiwi), nijuavyo mimi waandishi wa habari ni watundu sana na huweza kumpiga picha mtu bila hata yeye kujua kuwa kapigwa picha au karekodiwa. Sasa kinacho nishangaza mimi ni jinsi hawa wahariri walivyotii amri ya kutompiga picha au kurekodi sauti ya huyu mwekezeji, je walikuwa chini ya ulinzi wa mtutu wa bunduki?

Au ni unyenyekevu na usikivu tu wa Watanzania??

Na hapo walikua kwenye ardhi yao, wanapewa amri haramu wanatii.
Wangekua kwenye ardhi ya huyo "mwekezaji" ingekuwaje?
 
Na hapo walikua kwenye ardhi yao, wanapewa amri haramu wanatii.
Wangekua kwenye ardhi ya huyo "mwekezaji" ingekuwaje?

Unajua "usikivu" na "unyenyekevu" wetu utatumaliza. Ni nchi gani nyingine ambayo mambo yanaweza kutokea {mfano milipuko ya Mbagala, Gongo la Mboto, Dowans, Umeme, etc} na watu wala hawaoni kuna haja ya kuwawajibisha viongozi?? Kama jeshini hawajiuzuru basi wanasiasa wawajibike kwa kujiuzuru na wakishindwa tuwashinikize, lakini kwa kuwa sisi ni wasikivu na wanyenyekevu tutatii na kutekeleza
 
Aiseee tuna waandishi na wahariri uchwara wenye njaa sijapata kuona waandishi na wahariri wa ajabu kama wa Tanzania si ajabu angewaambia hata wavue nguo wangevua kama inavyoonekana kwenye katuni ya nathan wamedhalilisha taaluma yao:A S 112::A S 112::A S 112:
 
Nasikia walipewa sh. 300,000/- kila mwandishi aliyehudhuria. Haya ni maneno ya mitaani nilikosikia. Sina uhakika nayo. Lakini lisemwalo lipo.
 
Back
Top Bottom