Hivi wale nyumbu na wanyama wanaohama kila mwaka tumewafikiria pia katika mahusiano na Kenya au tunaangalia ng'ombe tu?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Nimetafakari hapa naona tuna kitu tunakijenga sio kizuri hata kidogo.

Yote ni mifugo tofauti ni wanyama pori na wakufugwa.

Kuna kila mwaka wanyama huwa wanahama kila mwaka toka Tanzania kwenda Kenya na kutoka Kenya kuja Tanzania katika kutafuta maji na malisho.

Nauliza hivi hawa wanyama hakuna nchi itakuja wazuia kuhama? Au kuvuruga hii taratibu za kuvuka mpaka na kutafuta marisho?
 
Mkuu haujui sheria za kimatifa za urithi wa dunia(Unesco heritage sites) ?
Haujui nchi za EAC ni wanachama wa WWF?
Sheria hizo zina zinakataza kufanya hicho unacho ogopa wewe.

Nafikiri unajua fika haya mambo lakini unataka kuhusisha siasa tu kila jambo.
 
Nimetafakari hapa naona tuna kitu tunakijenga sio kizuri hata kidigo.

Yote ni mifugo tofauti ni wanyama pori na wakufugwa. Kuna kila mwaka wanyama huwa wanahama kila mwaka toka tanzania kwenda kenya na kutoka kenya kuja tanzania katika kutafuta maji na malisho.

Nauliza hivi hawa wanyama hakuna nchi itakuja wazuia kuhama? Au kuvuruga hii taratibu za kuvuka mpaka na kutafuta marisho?

Wakati fulani miaka ya mwishoni mwa 1970 kama sikosei, uhusiano wa Kenya na Tanzania uliharibika sana na hata kufikia tulifunga mipaka kati ya nchi zetu. Hata tulianza kuwaita wakenya manyang'au nk, ukizingatia kwamba Wakenya walituchezea shere katika kuvunjika kwa East African Community wakati huo.

Sasa Wakenya walifanya kitu moja ya ajabu sana. Baada ya wanyama kuvuka toka Serengeti na kwenda Maasai Mara upande wa Kenya (wanyama wanakaa upande wa Kenya kwa kipindi cha miezi kama mitatu tu kwa mwaka) Wakenya waliamua kujenga uzio (fence) ili wanyama wale wasirudi tena Tanzania.

Sasa wakati wa wanyama kuhama Maasai Mara na kurudi Serengeti ulipofika, walikutana na fence ikiwazuia. Sasa wale wanyama walio mbele wakikabili fence wakaanza kusukumwa na wanyama walio nyuma ambao hawakujua nini kiko mbele. Matokeo yakawa kwamba ile fence ilivunjwa ikaanguka, na wanyama wengi kukwama katika fence na kuanza kukanyagwa na wenzao. Wanyama wengi sana walikufa na ilikuwa picha moja ambayo kwa kweli ilisikitisha sana. Hilo ni jambo ambalo hakuna kiongozi wa Kenya anapendwa kukumbushwa. Idiocy of the highest order.

Sasa Mkuu, hilo lilikuwa somo tosha kwa upande wa Kenya na Tanzania, kwamba hata kama tungekuwa na vita kati ya Kenya na Tanzania, hawa wanyama wasiingizwe katika mambo yetu ya kisiasa.
 
Kuna mbuga za wanyama na hifadhi za Taifa vituo ambavyo ni tofauti na malisho rasmi ya mifugo kama ng'ombe, mbuzi nakadhalika. Nadhani umeelewa ewe mwanzisha mada.
 
Mkuu haujui sheria za kimatifa za urithi wa dunia(Unesco heritage sites) ?
Haujui nchi za EAC ni wanachama wa WWF?
Sheria hizo zina zinakataza kufanya hicho unacho ogopa wewe.

Nafikiri unajua fika haya mambo lakini unataka kuhusisha siasa tu kila jambo.

Sheria hizo unazozitaja hapa zilizuia mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme, mbona serikali yetu imezikiuka na kuamua kulijenga?
 
Kumbuka hapa tunazungumzia mgogoro kati ya nchi na nchi. Na utaratibu wa sheria hauhalalishi kosa moja kuwa sio kosa kwa vile kuna kosa jingine lilifanywa na mlalamikaji sehemu nyingine.

Ukimuuwa mtu aliwahi kujaribu kujiuwa utahukumiwa kwa kuuwa kwa kukusudia kama kawaida.
Namaanisha sisi kukiuka ushauri au mkataba wa UNESCO / WWF kwa kujenga Dam selous hakuhalalishi nchi jirani kuzuia wanyama kuishi ktk mfumo wao wa ikolojia kamili ya asili.
Too wrongs don't make it right.
 
Nimetafakari hapa naona tuna kitu tunakijenga sio kizuri hata kidigo.

Yote ni mifugo tofauti ni wanyama pori na wakufugwa.

Kuna kila mwaka wanyama huwa wanahama kila mwaka toka tanzania kwenda kenya na kutoka kenya kuja tanzania katika kutafuta maji na malisho.

Nauliza hivi hawa wanyama hakuna nchi itakuja wazuia kuhama? Au kuvuruga hii taratibu za kuvuka mpaka na kutafuta marisho?
Hapo sasa .natuko ngwe ya visasi .visasi vimefanya mpaka tumesahau mamilioni ya nyumbu na ngombe elfu 5 walioko malishoni kenya kwa ngombe elfu 1 na mia 300 .hii ngwe Mungu ndio anajua
 
Mkuu haujui sheria za kimatifa za urithi wa dunia(Unesco heritage sites) ?
Haujui nchi za EAC ni wanachama wa WWF?
Sheria hizo zina zinakataza kufanya hicho unacho ogopa wewe.

Nafikiri unajua fika haya mambo lakini unataka kuhusisha siasa tu kila jambo.
Wazungu heritage sawa .Africa heritage kosa au !!??
 
Nimetafakari hapa naona tuna kitu tunakijenga sio kizuri hata kidigo.

Yote ni mifugo tofauti ni wanyama pori na wakufugwa.

Kuna kila mwaka wanyama huwa wanahama kila mwaka toka tanzania kwenda kenya na kutoka kenya kuja tanzania katika kutafuta maji na malisho.

Nauliza hivi hawa wanyama hakuna nchi itakuja wazuia kuhama? Au kuvuruga hii taratibu za kuvuka mpaka na kutafuta marisho?
Haiwezakani ukawazuia labda kwa kujenga ukuta kitu ambacho kitakuwa ni upuuzi,kwani kwa kufanya hivyo upande watakaobakia wote watakufa kwa kukosa malisho..
 
Wakati fulani miaka ya mwishoni mwa 1970 kama sikosei, uhusiano wa Kenya na Tanzania uliharibika sana na hata kufikia tulifunga mipaka kati ya nchi zetu. Hata tulianza kuwaita wakenya manyang'au nk, ukizingatia kwamba Wakenya walituchezea shere katika kuvunjika kwa East African Community wakati huo.

Sasa Wakenya walifanya kitu moja ya ajabu sana. Baada ya wanyama kuvuka toka Serengeti na kwenda Maasai Mara upande wa Kenya (wanyama wanakaa upande wa Kenya kwa kipindi cha miezi kama mitatu tu kwa mwaka) Wakenya waliamua kujenga uzio (fence) ili wanyama wale wasirudi tena Tanzania.

Sasa wakati wa wanyama kuhama Maasai Mara na kurudi Serengeti ulipofika, walikutana na fence ikiwazuia. Sasa wale wanyama walio mbele wakikabili fence wakaanza kusukumwa na wanyama walio nyuma ambao hawakujua nini kiko mbele. Matokeo yakawa kwamba ile fence ilivunjwa ikaanguka, na wanyama wengi kukwama katika fence na kuanza kukanyagwa na wenzao. Wanyama wengi sana walikufa na ilikuwa picha moja ambayo kwa kweli ilisikitisha sana. Hilo ni jambo ambalo hakuna kiongozi wa Kenya anapendwa kukumbushwa. Idiocy of the highest order.

Sasa Mkuu, hilo lilikuwa somo tosha kwa upande wa Kenya na Tanzania, kwamba hata kama tungekuwa na vita kati ya Kenya na Tanzania, hawa wanyama wasiingizwe katika mambo yetu ya kisiasa.
Ulilala ukaota hii ndoto na ukathubutu kuandika hapa.wewe sio mzima aisee .unasema nyumbu walizuiwa wakati ataa tulikuwa tunalishia ngombe kenya !!! .kwa taarifa yako mawasiliano pekee ambayo ayakuathiriwa na kuvunjika jumuia ni huu wa nyumbu na malisho ya ngombe .kama ujui uliza
 
Hapo sasa .natuko ngwe ya visasi .visasi vimefanya mpaka tumesahau mamilioni ya nyumbu na ngombe elfu 5 walioko malishoni kenya kwa ngombe elfu 1 na mia 300 .hii ngwe Mungu ndio anajua

Nyumbu hawawezi kuzuiliwa, tofautisha Ng'ombe ni personal wealth na nyumbu wanasimamiwa na UNESCO na hio ndio utaratibu wao kuwazuia UN wataingilia lazima na kamwe hawatoweza kuzuiliwa na wao wanalijua na sie tunalijua..na nyumbu kwenda Kenya au kurudi TZ hawavunji sheria Bali ng'ombe kuwachungia Kenya au TZ huko ni kuvunja sheria mbona ipo clear
 
Haujui nchi za EAC ni wanachama wa WWF?
Sheria hizo zina zinakataza kufanya hicho unacho ogopa wewe.

Chifu, unafahamu WWF ni NGO tu, right? Na sijawahi kusikia kuna nchi zilizo wanachama wa WWF! Isipokuwa WWF, kama International NGO, ina offices katika nchi mbalimbali. Na WWF haina sheria zozote ambazo nchi inapofanya kazi, zinafungwa na hizo sheria.

Pengine kuna jambo ulitaka kusema, lakini haujaliweka sawa.
 
Nimetafakari hapa naona tuna kitu tunakijenga sio kizuri hata kidigo.

Yote ni mifugo tofauti ni wanyama pori na wakufugwa.

Kuna kila mwaka wanyama huwa wanahama kila mwaka toka tanzania kwenda kenya na kutoka kenya kuja tanzania katika kutafuta maji na malisho.

Nauliza hivi hawa wanyama hakuna nchi itakuja wazuia kuhama? Au kuvuruga hii taratibu za kuvuka mpaka na kutafuta marisho?
Hii ninishu ya nature, haizuiliki! Iko kwenye dna ya hao wanyama kwenda na kurudi.
 
Haiwezakani ukawazuia labda kwa kujenga ukuta kitu ambacho kitakuwa ni upuuzi,kwani kwa kufanya hivyo upande watakaobakia wote watakufa kwa kukosa malisho..
Ndivyo vivyo hivyo ilivyo kwa domestic animals. For generations wamasai wametumia Serengeti-Masai Mara ecosystem kufugia na kuchungia mifugo yao. Kufanya alivyofanya Magufuli ni kuleta athari kubwa kwa wamasai na mifugo yao.

Kama mtu wa kutoka kabila la wafugaji (sukuma), siyo mshabiki sana wa wamasai. Pamoja ya tabia yao ya wizi, vilevile wamekuwa wakipendelewa sana na mashirika ya nje, kwa kuonyesha picha kwamba wanaonewa sana na serikali. Ilhali hata siye wasukuma tumeonewa sana na sera na mipango mibovu ya ufugaji ya serikali.

Lakini katika hili la kuzuia wamasai kutumia Serengeti-Masai Mara ecosystem, nipo pamoja na wamasai.
 
Back
Top Bottom