Hivi wakina dada mnavyoitwa mademu, mnakubaliana na hili jina?

DSpecial

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
480
158
Sikuzote kumuita msichana Demu huwa siwezi, na hili neno kulitamka kwenye kinywa changu ni zito sana kwakweli. Na kwa nilivyokuwa nikidhani hapo awali nilikuwa najua kama kunmuita msichana demu ni kama kumdhalilisha flani hivi. Ila naona linatumika sana kwakweli, lakini sijui kwa nini hili neno kwangu mimi linakuwa ni zito kulitumia. Sasa wadau na hasa kina dada wa humu JF naomba mnieleweshe vizuri kama hili neno mnakubaliana nalo kuitwa hivyo au huwa hampendi mnapoitwa mademu?
 
Mbona umeliandika?

Maana ya Dame na asili yake ni nini kwanza?

Halafu nitafutie na unielezee kirefu cha DBE
 
Definition of dame: lady - mistress - madam - gentlewoman

mbona wenyewe wako comfy nalo tu mkuu... kama wa kwako hapendi kuitwa hivyo uchune tu...
 
Subiri kongosho aje, mi ngoja ni bane pembeni hapa
 
Sikuzote kumuita msichana Demu huwa siwezi, na hili neno kulitamka kwenye kinywa changu ni zito sana kwakweli. Na kwa nilivyokuwa nikidhani hapo awali nilikuwa najua kama kunmuita msichana demu ni kama kumdhalilisha flani hivi. Ila naona linatumika sana kwakweli, lakini sijui kwa nini hili neno kwangu mimi linakuwa ni zito kulitumia. Sasa wadau na hasa kina dada wa humu JF naomba mnieleweshe vizuri kama hili neno mnakubaliana nalo kuitwa hivyo au huwa hampendi mnapoitwa mademu?

Unashauri waitwe vipi ili nawe uungane nasi?
 
Na maana ya kiswahili? I mean waswahili tunavyosema demu tunamaanisha nini?
Kaunga...Hili neno si la kiswahili. Ni neno ambalo limeanza kutumika dhidi ya akina dada miaka michache iliyopita sidhani kama imefika hata miaka 20 tangu lianze kutumika nchini. Ni neno ambalo asili yake ni Uingereza.
 
BAK si tumelikopa na kulipa maana yetu? Na limeonekana ni tatizo, ndio maana nataka kuelewa ili niseme kwamba it is okay kwa mimi kuitwa Demu au siyo!

Nakubali ni neno la kiingereza na maana zake kwa huko si mbaya hadi watu walichukie!
 
Last edited by a moderator:
BAK si tumelikopa na kulipa maana yetu? Na limeonekana ni tatizo, ndio maana nataka kuelewa ili niseme kwamba it is okay kwa mimi kuitwa Demu au siyo!

Nakubali ni neno la kiingereza na maana zake kwa huko si mbaya hadi watu walichukie!

@kaunga katika baadhi ya marafiki zangu niliowahi kuwasikia wakilitumia neno hilo dhidi ya maGF wao sikuona kama walilitumia kuonyesha ubaya wowote dhidi ya hao marafiki zao wa kike. "Angalia sentensi kama hizi, "Demu wako alikupigia simu ameacha ujumbe ukirudi umpigie." "Jana nilikuwa na demu wangu kwenye harusi ya mjomba wake." hivyo kama unavyoona halina maana mbaya lakini sijui labda siku hizi limebadilishwa maana na hivyo kuwa na negative connotation
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom