Hivi WAHESHIMIWA ni akina nani, ni WANANCHI au ni VIONGOZI wanaotumwa na wananchi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi WAHESHIMIWA ni akina nani, ni WANANCHI au ni VIONGOZI wanaotumwa na wananchi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 29, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,
  Rafiki yangu mmoja amenipigia simu na kunieleza jambo moja lililonisukuma kuandika thread hii. Anasema juzi aliwasiliana na diwani mmoja kwa tiketi ya cdm ili ampatie kero za mtaani kwake ili amsaidie. Wakati wanaongea, alizuiliwa na diwani asitumie neno 'mheshimiwa' anapomtaja. Pamoja na zuio hilo, rafiki yangu alikuwa anajisahau mara kwa mara na kurudia neno 'mheshimiwa'. Kila wakati diwani alikuwa akimkumbusha asitumie hilo neno.

  Jamaa alipomuuliza kwa nini nafanya hivyo, diwani alimweleza kuwa sisi wananchi ndiyo tunaowachagua wao na kuwatuma watuongoze na siyo kinyume chake. Katika kujenga hoja yake, diwani wa cdm alimuuliza yule rafiki yangu kwamba anayetuma na anayetumwa ni nani anastahili kuitwa mheshimiwa? Jamaa yangu alimjibu 'anayetuma'. Diwani 'akasema basi wewe ndiye mheshimiwa , siyo mimi'. Diwani aliendelea kumuuliza tena 'hapa tilipo ni nani anamtuma mwenzie kwenda kufuatilia ahadi ya serikali katika kutatua kero za mtaani kwake? Jamaa yangu yangu alimjibu 'ni mimi'. Diwani akahitimisha kwamba tangu Hayati Mwl. Nyerere ang'atuke madarakani viongozi wa ccm wamewapoka wananchi madaraka na kujitwika. Badala ya wananchi ambao katiba imewapa cheo kikubwa kwamba ndiyo chanzo cha madaraka, kuheshimiwa na kunyenyekewa, wanadhauriwa na kutukanwa kama mbwa.

  Diwani alihitimisha kwa kusema kuwa cdm ikiingia madarakani na kuunda serikali itarejesha haraka sana madaraka na heshima waliyopokwa wananchi. Neno 'mheshimiwa' litafutiliwa mbali na kuzikwa milele.

  Wazee mnaionaje injili hiyo??
   
Loading...