radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
Kuna jambo ambalo wana ccm wanajifariji na kulifurahia kwamba upinzani hasa chadema na cuf ukipotea basi ndio nafuu ya ccm swali dogo tujiulize toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe wamewahi kusikia wafuasi wa vyama vya upinzani baada ya nccr na cuf kupoteza nguvu na mvuto hivyo vyama vikakosa wafuasi kiasi kwamba wakarudi ccm kwa mapenzi yao?
Huo mpambano ktk chaguzi mbalimbali ambao ccm inaupata hao wapiga kura wanatoka wapi? Hapa lazima akili ya ziada inahitajika kujua kwamba upinzani si vyama vya upinzani bali dhamira iliyopo mioyoni mwa baadhi ya watu ambao hawaridhishwi na ccm hii ina maana hata kama chadema na cuf vitapotea hili kundi litaendelea kuwepo ambalo baadae litakuja kuwa na nguvu za ajabu.
Endapo vyama vya upinzani vikatoweka hili kundi ambalo tayari linachembechembe za kutaka mabadiliko litakwenda wapi? Je mtawalazimisha wawe wanachama wa ccm kinguvu? Hapa mwenyekiti wa ccm,katibu na ndugu polepole wanacheza kamari kitu wanachokizalisha baadae watakilipa kwa gharama yoyote ile.
Kwa sasa hamna kumuunga mkono wamekuja na slogan mpya wanapita bila kupingwa huu ni mchezo wa kitoto sana unaofanywa na watu wenye viwango vya udaktari na uprofesa kwa kushabikia hili jambo.
Nguvu kubwa inatumika kurubuni madiwani na wabunge wahamie chama kikuu kweli wengine wanakubali lakini hata ukiwaangalia kwa muonekano wa taswira zao ni watu waliokosa kujiamini na hawana amani kabisa.
Muda ni hakimu mzuri haki ya mtu haipotei ila hucheleweshwa tu.