Hivi wabunge wetu mapungufu haya yamewashinda au hamko serious? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi wabunge wetu mapungufu haya yamewashinda au hamko serious?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jun 29, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,999
  Likes Received: 37,701
  Trophy Points: 280
  Binafsi huwa napata taabu sana kuona hawa wabunge wetu wakiendelea kuvumilia na kuangalia mhimili huu kuendelea kuendeshwa na kanuni hizi za bunge ambazo ni mbovu kabisa na zinahitaji marekebisho makubwa ili kuongeza ufanisi wa bunge.Kibaya zaidi ni namna spika na wasaidizi wake wanavyotumia mapungufu ya kanuni hizi kudidimiza watanzania kwa mfano anapoamua kukataa mwuongoza kuhusu mgomo wa madaktari.Hivi unapokuwa spika wewe ndio unajua kanuni zaidi kuliko wenzako au ni matumizi mabaya ya kiti chako kama spika.Au hawa wanaomba muongozo ama taarifa hawajui kanuni yaani wanakurupuka?Na ukishatoa maauzi hakuna kuhoji maamuzi ya spika kwa wakati huo labda mtu akate rufaa baadae wakati maamuzi umeshayafanya na ambayo tayari yanaweza kuwa na madhara kwa wakati huo.

  Nachokiona ni kuwa spika wa bunge amepewa madaraka makubwa mno kama mtu mmoja kiasi cha kuweza kuzima hata hoja za msingi.Mambo mengi ni ridhaa ya spika(amue anavyoona inafaa).Ukiachia mbali maswla ya muongoza na taarifa hata kamati za bunge inavyosemekana zinapaswa kwanza kuwasilisha taarifa kwa spika nae ndio aamue kama taarifa hiyo iende bungeni kujadiliwa au laa.Kwa maneno mengine anaweza kuruhusu taarifa ya kamati ya bunge iliyotumia kodi za wapiga kura isomwe au isisomwe bungeni!Mfano ni sakata la mh.mmoja alietishia kujiuzulu baada ya taarifa yake kama mwenyekiti wa kamati kutaka kukataliwa na spika kwa mujibu wa gazeti moja ambalo liliwahi kuripoti habari hiyo siku za nyuma.

  Sasa hawa wabunge mbona sijawahi kuwasikia wakilalamika au kudai hizi kanuni za bunge zipitiwe upya!Au nao wanaridhika na mwenendo huu wa uendeshaji bunge?Basi waache kulalama.Mbona mapungufu ya katiba mnayajua vizuri na haya ya bunge lenu hatuwasikii mkiyalalamikia.

  Binafsi huwa naumia sana kuona mambo ya msingi yanazimwa na wabunge kutokuchukua hatua za kudai mabadilko.

  Timizeni wajibu wenu muokoe hawa wananchi wenu ambao nawaona sasa wamebaki kama watoto yatima.
   
Loading...