Hivi wabunge walipitishaje budget isiyokuwa na nyongeza ya mishahara?

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
671
1,427
Kuna taarifa za uhakika kuwa nyongeza za mishahara ya watumishi wa umma kwa mwaka 2016/2017 hazikufanyika coz hazikukuwepo kwenye budget ikiwa na maelekezo toka kwa Mkulu, wabunge walipitishaje bila kujua au kuhoji,ile 15% ya loan board nayo ilipitishwa na binge letu bila kuhoji kuwa kuna watumishi wana madeni kwenye taaasisi mbalimbali hivyo kuongeza makato bila nyongeza yoyote ni hatariii,kiukweli Nina dauti na umakini na weledi wa Bunge letu tukufu.
FB_IMG_1490896357684.jpg
FB_IMG_1490896357684.jpg
 
Kuna wengine wakati wa majadiliano waliziba midomo na karatasi wakatoka nje na wengine waliobaki ndani walijibu ndio bila hata kusoma kilichoandikwa...kiufupi bunge lilivurugwa wakati wa kupitisha bajeti, kama wabunge wangeweka uchama pembeni na kusimamia ukweli na maslahi ya waliowachagua huenda haya yasingetokea:rolleyes:
 
Wabunge wengi bungeni wanaangalia maslahi ya vyama vyao kwanza!
 
Tangu lini bunge letu likafanya hivyo?
Hapa wa kulaumiwa ni wale walioitikia nndiyo, maana hao unaosema waliziba midomo hata kama wangekuwemo "hapana zao" zisingesikika mbele ya "ndiyo" za wapenda serikali. Kifupi kwa kuwa bajeti ilikuwa imewasilishwa na serikali ya chama chao, hata kama ingekuwa mbaya kiasi gani wangeipitisha tu, isipokuwa tu kama ingekuwa inaonekana kuwa mbaya KWAO
 
Kwanini upindishe ukweli!? Wabunge wa MACCM waligawana milioni 10 kama rushwa ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini.
Wabunge wa Chadema lipi walilofanya la kulinda maslahi yao badala ya yale ya Watanzania!?

Wabunge wengi bungeni wanaangalia maslahi ya vyama vyao kwanza!
 
Nahis tuwe wavumilivu wakuu..mwezi wa nne mambo yatakua mazuri tu. Maana uhakiki unaisha kesho kabisa. So wote ambao wanastahili kupanda madaraja na waliopanda mwaka jana wakasitishiwa..mshahara wa mwez april mambo yatakua safi.
 
Kwanini upindishe ukweli!? Wabunge wa MACCM waligawana milioni 10 kama rushwa ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini.
Wabunge wa Chadema lipi walilofanya la kulinda maslahi yao badala ya yale ya Watanzania!?

Ha!ha!ha! Mkuu najua unajua kulingana na ninavyokufahamu...

Hata katiba ya Chadema inawataka wabunge kulinda na kukitetea chama kwanza kabla ya mengine...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hilo ni muhimu kwa chama chochote kile. Narudia swali langu Wabunge wa Chadema wamefanya lipi Bungeni au hata nje ya Bunge la kuweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Watanzania ukilinganisha na rushwa ya milioni 10 waliyopokea Wabunge wa MACCM!?

Ha!ha!ha! Mkuu najua unajua kulingana na ninavyokufahamu...

Hata katiba ya Chadema inawataka wabunge kulinda na kukitetea chama kwanza kabla ya mengine...
 
Hizi taarifa zako km ni zitakua za kweli basi swali hili ungewauliza wabunge na si kumzushia Mkuu vitu vya uongo uongo.Unao ushahidi kua Mkuu alitoa hayo maelekezo au unajisemea tu?Mda si mrefu yatakupata ya kukupata manake Sasa umezidi..
 
Hapa swali la msingi ni hili, kwani wabunge kwenda bungeni ni kwenda kutetea maslahi ya chama au ya wananchi? Ninavyojua mimi sisi tulio wapigia kura ndiyo tumewaajiri na siyo chama. Ila kinacho nipa afadhali ni wabunge wa upinzani ambao wanajitahidi sana kulinda maslahi ya nchi. Tatizo kubwa ni moja, wako wachache cha kusikitisha walio wengi ndiyo kero mpaka unaweza kujiuliza hivi kweli ni watanzania wenzetu au wanakuwa wametumwa makusudi kupotosha hali halisi inavyotakiwa kuwa.
Kwa style ya bunge letu ilivyo ni bora tuongeze wigo kwa kuruhusu mgombea binafsi.
 
Back
Top Bottom