Hivi wabunge wa CCM hamuoni udharura wa hili jambo?

February 6, 2020
Iringa, Tanzania

Barabara ya mlima Kitonga yageuka mto

VIDEO Hii inakuonyesha hali ilivyo katika Mlima Kitonga uliopo mkoani Iiringa ambapo maji mengi yanayosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini yamevamia mlima huo baada ya kupotea njia...




Source: Global TV online TV

Mafuriko ya ajabu mlima Kitonga mkoani Iringa uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania



Source: mbeyazone online
 
Mlima Kitonga na barabara yake

Kwa wale wasioufahamu Mlima maarufu wa Kitonga ambapo barabara ya TANZAM Tanzania kwenda Zambia na nchi za Kusini mwa Afrika hupita video hii itakupa taswira ikipitiwa au kugeuzwa mto wa mafuriko ya leo February 6, 2020 itawapa changamoto gani watumiaji wa barabara hiyo muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini ikiwemo Lubumbashi Katanga DR Congo



Souce: millard ayo
 
February 6, 2020
Iringa, Tanzania

Barabara Mlima Kitonga yageuka kuwa mto



Source : Jidy TV
 
Mvua kubwa inayonyesha nchini limekuwa ni kama jambo la dhararu kwani mafuriko yanayosababishwa na mvua hiyo yameleta madhara makubwa sana kwa watanzania.

Wabunge wa CCM badala ya kujifanya mna dharura ya kumjadili Zitto ama Lissu, hebu jadilini kwa dharura hili jambo kwani watanzania wengi wameshapoteza maisha na miundombinu ya kutosha imeshaharibiwa kutokana na mvua inayoendelea kunyesha.

Sehemu kubwa ya Tanzania itakuwa na njaa mwakani kwani mazao mengi ya wakulima ama yamesombwa au kufunikwa na maji. Maeneo mengi yanakolimwa mpunga yamefurikishwa.

Mnapojadili vitu visivyo vya dharura kidharura na kuacha kujadili dharura wakati wa dharura ni matumizi mabaya ya wingi wenu bungeni.

Nakumbuka wakati wa MKIRU mliwagomea wapinzani kujadili kilichokuwa kinaendelea kule, na hata sasa mnaona siyo dharura wakati watanzania wenzenu hawana pa kuishi kwa kuwa makazi yao yamebomolewa, hawana chakula kwa kuwa mashamba yao yameharibiwa na chakula kwenye majumba yao kimezolewa na maji.

View attachment 1347613
Barabara ya kwenda Dodoma kutokea Iringa.
Picha kwa hisani ya Mwalimu Expedito Mduda.
Hawawezi kujadili kwani mvua haikuletwa na serikali ya CCM, ila kama kuna misaada tutawapangia utaratibu mzuri wa kutuletea nasi tutapanga utaratibu mzuri wa kuigawa kulingana na mahitaji.
 
Back
Top Bottom