Hivi waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania wanalipwa vizuri kweli? Tusilete lawama bure tu!

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,489
188,636
Habari wanamichezo na wapenda soka wote ndani na nje ya Tanzania.

Haya mambo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara katika misimu yote ya ligi kuu ya Tanzania kwa sasa 'NBC Premier League' kuhusu lawama kwa Kunguru wetu hawa wa mpira. (Referees)

Tutafute hoja za msingi na mambo yanayoleta yote hayo yote ni kweli hawa Waamuzi wanalipwa vizuri kulingana na kazi yao viwanjani au ni siasa za mpira hadi kwenye malipo.

Naamini hawa watu (Kunguru) ni watu wenye weledi kuhusu kazi hiyo si wapuliza kipenga na watu wa mchongo.

Swali langu kwa wanamichezo na TFF hivi hawa Kunguru wanalipwa vizuri?

Nimetumia neno "Kunguru" maana ndio neno tuliotumia kwa kipindi kirefu sana kipindi cha nyuma, I mean no offense.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Uwenda awalipwi vizuri,lakini pia kuna swala la kiufundi kwa marefa je'wanazingatia sheria zote na kanuni wanapokua uwanjani.

Angalia madhaifu makubwa ya marefa wetu,penati inapigwa akiwa anaruhusu wachezaji zaidi wa wanne wakiwa ndani ya box la 18 mechi ya Namungo na Utopwinyo.

Mechi ya jana Simba na Geita kabla refa kufanya maamuzi angalau angeuliza wasaidizi wake wa pembeni angetenda haki.
 
Najua Kuna wataalam na watu wa jikon hapa ,tunataka kujua refa analipwa Bei gani per game ,ili tuone uwiano wa haya yanayoendelea ,isiwe ikawa Wana njaa Sasa watawezaje kukataa bahasha yenye 500k Kama wanalipwa kiduchu?

Tafadhari jaman tupen Bei elekez per game kwa marefa Hawa wa Bongo land
 
Ile mechi kocha tayari alikuwa ameshapaniki ndio maana ht hakuona hayo makosa ya wachezaji kuingia ndani ya box ht kabla penalty haijapigwa
 
Kama malipo ni haba basi hata weledi wa mtu kwenye kazi husika utashuka kwa kasi.
 
Najua Kuna wataalam na watu wa jikon hapa ,tunataka kujua refa analipwa Bei gani per game ,ili tuone uwiano wa haya yanayoendelea ,isiwe ikawa Wana njaa Sasa watawezaje kukataa bahasha yenye 500k Kama wanalipwa kiduchu?

Tafadhari jaman tupen Bei elekez per game kwa marefa Hawa wa Bongo land
Hii imekaa vyema sana tukijua hata mshahara inaweza kutoa picha halisi ya nini kipo nyuma ya pazia.
 
Ile mechi kocha tayari alikuwa ameshapaniki ndio maana ht hakuona hayo makosa ya wachezaji kuingia ndani ya box ht kabla penalty haijapigwa
Hiyo pia inaonyesha udhaifu mkubwa maana uwezi kukosea kama muamuzi wa mchezo na uendelee panic hiyo itaongeza makosa na si kusahihisha makosa.
 
Back
Top Bottom