Hivi Vyama vya Wafanyakazi pamoja na kuchukua michango kila mwezi vinakosa hata tovuti

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
15,161
20,087
Niende kwenye mada kuna kijana kaniomba nimuelekeze wapi zilipo ofisi ya chama cha wafanyakazi kutokana na yeye kuwa na mgogoro na mwajili wake yaani TUCTA.

Kwa kuwa ni mfanyakazi kwenye huduma za mahotel nilimweleza TUCTA ni muunganiko wa vyama vya wafanyakazi toka sekta tofauti ila yeye anatakiwa akaonane na CHODAWU ambayo inahusika na sekta yake.

Akaniomba nimsaidie wpi zilipo ofisi za CHODAWU ili aende kuziona, nikaingia google ili nitafute hizi ofisi kwa kujua umuhimu wa hicho chama nilitegemea taarifa zake nitazikuta lakini cha ajabu hakuna taarifa yoyote niliyokuta inayoweza kusaidia wapi ofisi ilipo au hata tovuti yao hii ilinishangaza kwanini chama kama hicho hakioni umuhimu wa kuwa na tovuti kipindi hiki cha digital au michango ya wanachama wao wanaifanyia nini zaidi ya kulipana posho
 
Aisee,

Yaani katika nchi ambayo vyama vya wafanyakazi tumeviona vya kawaida kabisa na pengine havina umuhimu ni Tanzania. Ni aibu sana kwa trade union kukosa hata tovuti. Lakini pia tuna kazi ya kufanya kama taifa, wananchi na hata wafanyakazi kuhakikisha vyama hivi vinakuwa imara na sio tu kuwakamua wafanyakazi michango bila kuonesha output yoyote kwa taifa.

Nikizitafakari portfolio za vyama kama TUGHE, TALGWU, CWT na wengineo ninasikitika sana kuona ukubwa wa portfolio iliyo nazo hauendani kabisa na sauti zao mbele ya jamii
 
Kitengo cha it cha ndani bado kiko nyuma sana aidha taasisi husika ndo ziko nyuma au laa mana taarifa nyingi za taasisi mbali mbali huwezi kuzikuta kwenye mtandao
 
Ni mambo ya ajabu tunaitwa mashikolo mageni Wananzengo huku...mfano CWT wanayo ila haifanyi kazi.
 
Back
Top Bottom