Uchaguzi 2020 Hivi Vyama vya Upinzani Tanzania viko serious na kuongoza Serikali?

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
424
725
Wasalaam wanaJF,

Kwa bahati nzuri nimefanikiwa kufuatilia mchakato wa kutafuta wagombea/wawakilishi wa nafasi mbalimbali kwenye vyama mbalimbali kwaajili ya kupeperusha bendera za vyama vyao kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2020.

Kiukweli na uwazi ni dhahiri kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejitanabaisha na kujipamba sawia katika wagombea wake kuanzia ngazi za udiwani kwani katika vitu vyote walivyofanya kwenye mchakato huu kumewajengea jina watu wanaoenda kuwa wagombea wao na katika duru za siasa umaarufu ni mtaji mkubwa kwenye kutengeneza wapiga kura kitu ambacho vyama vya upinzani Tanzania havijatilia mkazo katika hili.

Kitu cha pili ni mpango mkakati, Vyama vya upinzani Kwa mfano Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) nguvu kubwa wamewekeza kwa wagombea wa nafasi za uraisi! Sasa najiuliza mgombea wa CHADEMA akishinda nafasi hii ya uraisi ataongoza Serikali ya namna gani? Je, atadumu kwenye kiti ya uraisi hata kwa mwaka mmoja?

Kwanini vyama vya upinzani haviwekezi nguvu kwenye kutafuta wabunge na madiwani ili kupata wawakilishi wengi kwenye mabaraza na Bunge? Leo hii asilimia kubwa ya wabunge wa upinzani ni matokeo ya M4C na movements mbalimbali Kwanini wametelekeza mkakati huu. Hivi wakiamua kusimamisha wagombea 200 wa uhakika na kuachana na Urais walau kwa kipindi kimoja na kulishika Bunge kisawasawa hawaoni watajenga zaidi nafasi yao?

Uhitaji kutumia nguvu kubwa kuona kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huu ujao na si kwasababu za kufichika hapana bali CCM wamejiandaa vizuri kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vingine vya siasa.

Naomba kuwasilisha
 
Cesar Saint,

Ngoja waje wahusika utapata majibu yanao kutoshelesha, ila kwa haraka haraka wewe inaonekana ni mgeni hapa Tanzani, vinginevyo wewe utakuwa new recruit toka Lumumba ndio uko mafunzoni, maana wale wakongwe wa Lumumba post zao kidogo wameziboresha, jitahidi nawe utafika kiwango chao.
 
Mkuu huu ni ukweli McHugu lazma tujiweke dhabit kwa Yale tuyatendayo kiukweli hata jambo la kuchelewa msibani limenifanya nione wazi kabisa kuwa viongozi wa cdm hawako pancho kabisaaa SASA tutaongozwa na serikali ambayo haiwezi hata kwenda nana muda
 
Kojoa kalale yani usiku wa manane unaamka kuandika huu ushuzi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Uhitaji kutumia nguvu kubwa kuona kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huu ujao na si kwasababu za kufichika hapana bali CCM wamejiandaa vizuri kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vingine vya siasa.

Naomba kuwasilisha
Mkuu Cesar Saint, kwanza asante kwa bandiko hili very objective, naunga mkono hoja, pili kuna maukweli mengine ni maukweli yenyewe halisi ya kinachokwenda kutokea uchaguzi huu wa 2020, kwenye issue ya urais, ulichosema ni ukweli kabisa, lakini kwa vile humu kuna watu wanaishi ndotoni na kufanya utopian politics, wakiota ndoto za mchana kweupe, wao watakupinga na wata kubeza.

Bandiko lako hili limejibu baadhi ya maswali ambayo mimi niliyauliza ile 2015
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

P
 
Na maccm yanaamini hivyo hivyo na kuwaona Chadema ni wahuni, lakini uhuni wao wa kugombea hadi wanawake hadharani kwa kumsingizia anatembea na wake za watu hawauoni.

Hata Edward Twinning, Governor wa mwisho wa Uingereza kabla ya Uhuru hakuamini kama TANU ingeweza kuongoza nchi.
 
Sky circumstance za TANU ,CCP,ANC na vyama vingi vya kiukombozi au mageuzi Afrika vilikuwa katika mazingira tofauti na zaidi viliwekeza katika strategy za muda mrefu hasa kwa kufahamu nafasi finyu waliokuwanayo na rasilimali walizokuwa nazo kisha juu ya wote walikuwa na mtaji wa watu.

Leo hii watu wanaondoka vyama vya upinzani kama njugu huwezi kuita wote wasaliti ijapokuwa ni kweli yawezekana wakawepo lakini chama ili kiendelee kinahitaji kuwa na uwezo wa kufunda watu,kukuza watu na kutunza watu wake .Na ndio maana umeona hata CCM walipopata mkwaruzano hapa kati asilimia kubwa ya wale watu wamebakizwa kwenye chama Hebu fikiria nguvu ya upinzani kama wangempata mzee Makamba,Mzee Kinana,Nape,January na wengineo?
Au fikiria kama CDM ingekuwa na wakina Slaa,Zito,Dr Kitila na is wengineo.

Vyama vya upinzani Tanzania vinakosa mipango ya muda mrefu na huu ndio ukweli!
 
Na maccm yanaamini hivyo hivyo na kuwaona Chadema ni wahuni, lakini uhuni wao wa kugombea hadi wanawake hadharani kwa kumsingizia anatembea na wake za watu hawauoni.

Kiuhalisia kama vyama vya upinzani vingekuwa na mipango ya muda mrefu na endelevu pengine vingeweza hata kupata Serikali ya mseto! Maana kama CCM ni dhaifu na bado inawazidi kujipanga kiuchaguzi vyama hivi kama taasisi na dhahili vinapungua mahali.
 
Kama vyama vya upinzani ni DHAIFU inakuwaje uchaguzi HURU na wa HAKI utakaosimamiwa na Tume Huru UNAOGOPWA? Maccm yametufikisha hadi uchumi wa kati kwa nini baada ya “mafanikio” hayo makubwa wahofie uchaguzi utakaokuwa halali!? 😳

Sky circumstance za TANU ,CCP,ANC na vyama vingi vya kiukombozi au mageuzi Afrika vilikuwa katika mazingira tofauti na zaidi viliwekeza katika strategy za muda mrefu hasa kwa kufahamu nafasi finyu waliokuwanayo na rasilimali walizokuwa nazo kisha juu ya wote walikuwa na mtaji wa watu.

Leo hii watu wanaondoka vyama vya upinzani kama njugu huwezi kuita wote wasaliti ijapokuwa ni kweli yawezekana wakawepo lakini chama ili kiendelee kinahitaji kuwa na uwezo wa kufunda watu,kukuza watu na kutunza watu wake .Na ndio maana umeona hata CCM walipopata mkwaruzano hapa kati asilimia kubwa ya wale watu wamebakizwa kwenye chama Hebu fikiria nguvu ya upinzani kama wangempata mzee Makamba,Mzee Kinana,Nape,January na wengineo?
Au fikiria kama CDM ingekuwa na wakina Slaa,Zito,Dr Kitila na is wengineo.

Vyama vya upinzani Tanzania vinakosa mipango ya muda mrefu na huu ndio ukweli!
 
Sky circumstance za TANU ,CCP,ANC na vyama vingi vya kiukombozi au mageuzi Afrika vilikuwa katika mazingira tofauti na zaidi viliwekeza katika strategy za muda mrefu hasa kwa kufahamu nafasi finyu waliokuwanayo na rasilimali walizokuwa nazo kisha juu ya wote walikuwa na mtaji wa watu.

Leo hii watu wanaondoka vyama vya upinzani kama njugu huwezi kuita wote wasaliti ijapokuwa ni kweli yawezekana wakawepo lakini chama ili kiendelee kinahitaji kuwa na uwezo wa kufunda watu,kukuza watu na kutunza watu wake .Na ndio maana umeona hata CCM walipopata mkwaruzano hapa kati asilimia kubwa ya wale watu wamebakizwa kwenye chama Hebu fikiria nguvu ya upinzani kama wangempata mzee Makamba,Mzee Kinana,Nape,January na wengineo?
Au fikiria kama CDM ingekuwa na wakina Slaa,Zito,Dr Kitila na is wengineo.

Vyama vya upinzani Tanzania vinakosa mipango ya muda mrefu na huu ndio ukweli!
1. Kwanini serikali ya CCM haitoi nafasi sawa kwa vyama vya upinzani katika ulingo wa siasa?

2. Ni viongozi wangapi waliotoka Chadema na wamefanya kazi nzuri katika serikali ya CCM. Mfano Dr Slaa, Juliana Shona, Mwampamba (aliharibu tu kumpenda mke wa mkubwa😂)

3. Nguvu watuya Chadema umeiona mwenyewe uwanja I J3,na pale wengi waliogopa kufika kwa vitisho vya polisi.
 
PUMBA TUPU!

Mkuu Cesar Saint, kwanza asante kwa bandiko hili very objective, naunga mkono hoja, pili kuna maukweli mengine ni maukweli yenyewe halisi ya kinachokwenda kutokea uchaguzi huu wa 2020, kwenye issue ya urais, ulichosema ni ukweli kabisa, lakini kwa vile humu kuna watu wanaishi ndotoni na kufanya utopian politics, wakiota ndoto za mchana kweupe, wao watakupinga na wata kubeza.

Bandiko lako hili limejibu baadhi ya maswali ambayo mimi niliyauliza ile 2015
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

P
 
Kama vyama vya upinzani ni DHAIFU inakuwaje uchaguzi HURU na wa HAKI utakaosimamiwa na Tume Huru UNAOGOPWA? Maccm yametufikisha hadi uchumi wa kati kwa nini baada ya “mafanikio” hayo makubwa wahofie uchaguzi utakaokuwa halali!?

Sidhani kama vya upinzani ni dhaifu ila nachofikiri ni kuwa havifanyi majukumu yake vizuri na zaidi havina mipango ya muda mrefu.

Kuna msemo wa kiingereza unasema “Respect is not given nor granted rather than Earned “

Vyama vya upinzani vinafanya nini kupata uchaguzi huru na haki ,Vinafanya nini kuchangiza mabadiliko ya katiba? Vyama vya upinzani vinafanya nini kujiandaa na uchaguzi?
 
Mkuu Cesar Saint, kwanza asante kwa bandiko hili very objective, naunga mkono hoja, pili kuna maukweli mengine ni maukweli yenyewe halisi ya kinachokwenda kutokea uchaguzi huu wa 2020, kwenye issue ya urais, ulichosema ni ukweli kabisa, lakini kwa vile humu kuna watu wanaishi ndotoni na kufanya utopian politics, wakiota ndoto za mchana kweupe, wao watakupinga na wata kubeza.

Bandiko lako hili limejibu baadhi ya maswali ambayo mimi niliyauliza ile 2015
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

P
Msifikirie TL hajui hili, la hasha analijua ila nia yake ni kuja hapa, afanyiwe mizengwe (ambapo ujio wake umebugi) ili afanyiwe mizengwe na baadaye arudi akachume mihela ya wazungu wasioitakia mema Tanzania. Kiuhalisia huwezi kumuondoa rais aliye madarakani kwa mtindo huu wa tarumbeta. Rais aliye madarakani anaondolewa kwa yeye kujisahau na kudhani kila kitu kipo sawa.

Chama serious kwa wakati huu kingejikita kutafuta wabunge ili 2025 kichukue nchi. Wahenga walisema kwenye miti hapana wajenzi, mchakato wa ubunge wa CCM mwaka huu umetengeneza Makundi ambayo hayajapata kutokea kiasi kama CDM ingalikuwa imejipanga ingechukua majimbo mengi kiulaini kama Halima mdee anavyochukuaga Kawe . Ila wao wanahangaika na kusukuma mwamba ambao hausukumiki.
 
Mkuu Cesar Saint, kwanza asante kwa bandiko hili very objective, naunga mkono hoja, pili kuna maukweli mengine ni maukweli yenyewe halisi ya kinachokwenda kutokea uchaguzi huu wa 2020, kwenye issue ya urais, ulichosema ni ukweli kabisa, lakini kwa vile humu kuna watu wanaishi ndotoni na kufanya utopian politics, wakiota ndoto za mchana kweupe, wao watakupinga na wata kubeza.

Bandiko lako hili limejibu baadhi ya maswali ambayo mimi niliyauliza ile 2015
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

P
No wonder wajumbe walikutendea haki kule kwenye kura za maoni.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom