Intaneti ya Vodacom yakatika nchi nzima - Februari 23, 2020

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,761
5,877
Aisee ,nimeamka asubuhi na mapema kama kawaida yangu nianze shughuli zangu kupitia internet..

Bahati mbaya kwangu na nzuri kwa wapinzani wangu kibiashara, nakuta internet ya vodacom haifanyi kazi.!

Napiga huduma kwa wateja najibiwa 'Kuna tatizo la kimtandao, tafadhari kuwa mvumilivu, mafundi wetu wanashughulikia'...

Nimeamua kutumia Freebasics ya tigo sababu siwezi nunua kifurushi wakati Voda nina bando la mwezi..

Maswali yangu mawili tu kwa hawa wapumbavu,wajinga,wenye roho mbaya VODACOM,.

1. JE WANAJUA HASARA NINAYOPATA KWA HUU UPUUZI WAO (WAPO TAYARI KUFIDIA).???

2. JE WANAMAANISHA TUHAME SABABU HAWANA SHIDA YA MTEJA MMOJA MMOJA KWASABABU WAO WANA WATEJA WENGI.???

UPDATE:

Baada ya takribani saa 8 tangu intaneti ikatike, Vodacom ndio wamewaarifu wateja kuhusu kasoro hiyo

A7E3D85E-AFD5-4A8A-9AA0-568D8DFE34DB.jpeg
 
Wameniudhi sana, mimi bila internet ni sawa niko jela. Imenilazimu kununua kifurushi airtel kasi ya kobe ila bahati mbaya hutokea tu kwenye hii mitandao yetu.

Naamini vodacom watarudi hewani soon.
 
Hawa jamaa wajinga sana,nimetoka kuwapigia mda si mrefu nawahoji naona wanajikanyaga kanyaga tu

Nilijiunga jana jioni na kifurushi chao cha internet cha GB 2/siku 3,leo asubuhi kila nikijaribu internet inagoma

Na nilikua na kazi muhimu sana,nikahisi labda tayari lile jini lao la kula GB limeshafanya yake,sikujali sana nikaamua kujiunga upya tena na kifurushi cha GB 2/ masaa 24

Ajabu sasa kila nikijaribu tena chengaaaa, nikaona huu ufala sasa nikaweka line yangu ya mtandao mwinigine nikafanya yangu nikamaliza

Sasa hivi nimetoka kuwabwatukia na maswali wanaashindwa kunijibu

1. Kama kuna tatizo la kimtandao kwa muda mrefu namna hii,mmeshindwa nini kututumia msg ya kutufahamisha? mbona meseji zenu nyingine sijui songesha,mara jimwage mnazitumaga nyingi tu tena bila kuwaambia?!!

2. Kwa vile mmeshindwa kututumia message kutuambia tatizo mmesababisha baadhi yetu kujiunga na kifurushi kipya tukidhania kuwa kifurushi kilichokuwepo kimeisha...na kwa vile maroboti yenu uwa hayapitishagi hata sekunde moja kusitisha kifurushi mda wake ukiisha, ebu niambieni sasa,mtanilipa vipi mimi niliejiunga na kifurushi cha masaa 24 halafu masaa karibia saba sipati huduma??????!!!!!!!

Je, mtanicompasate muda wangu au inakuaje? huwezi amini customer care kakosa jibu....bogas kabisa hawa jamaa!!!

Na nimepanga mtandao ukirudi tu,walaah lazima wanifidie muda wangu wa kifurushi,sitaki utani kabisaaaaaa!!!

Wizi wa kijinga jinga namna hii nimechokaaaaa!!!
 
Mi wamenipa tangu jana ofa ya 250MB, hadi sasa nafungua holaa. ngoja niendelee kufaudu hiki kifurushi changu cha halotel
 
Mi jana tu nimeunga bando la gb3 leo asubuhi nakuta intanet sina. Nauliza kila mtu nyumbani anasema nae hana. Intanet inaonekana imekata kuanzia saa 6 usiku mpaka muda huu haijarudi. Sijajua watanifidia vipi muda wote huo ambao huduma haipo?
Nimemkumbuka yule jamaa aliekua anawashtaki sijui kaishia wapi?
 
Kinachowapasa kufanya ni kufidia huu muda wanaoukata kwa wale wenye vifurushi vyao, maana vifurushi ni vya masaa, siku, wiki, mwezi. Hivyo unapositisha huduma ni lazima ufidie pesa yake
Na hilo ndo linalopaswa kufanyika mimi nimejiunga 3.5GB za siku tatu tokea jana jioni, hadi Sasa Salio langu linaonyesha nina 2.7GB sijui siku ya leo niliyokosa huduma yao nayo wataihesabu kwa kweli Watanzania hii mitandao inatuibia sana, tumekuwa wanyonge mno hii mitandao inatunyonya na kuiba sana
 
Back
Top Bottom