Hivi vocha ya simu hubadirishwa vipi na kuwa thamani ya pesa!?

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Ndiyo hivyo tena mwenzenu nipo hapa nakwangua vocha ya Halotel lakini ghafla najiuliza ni kwa namna vocha ya karatasi ya elfu kumi inabadirishwa vipi na kuwa na thamani ya pesa!?

Wajuzi nijuzeni.
 
Ndiyo hivyo tena mwenzenu nipo hapa nakwangua vocha ya Halotel lakini ghafla najiuliza ni kwa namna vocha ya karatasi ya elfu kumi inabadirishwa vipi na kuwa na thamani ya pesa!?

Wajuzi nijuzeni.
Kabla sijakujibu ngoja nione kiwango cha ufahamu wako. Unapoenda sokoni kununua nanasi la shs 2000... umewahi kujiuliza nanasi hilo limebadilishwa vipi na kuwa thamani ya pesa?
 
Kabla sijakujibu ngoja nione kiwango cha ufahamu wako. Unapoenda sokoni kununua nanasi la shs 2000... umewahi kujiuliza nanasi hilo limebadilishwa vipi na kuwa thamani ya pesa?
Aspirin umezalisha swali fanani kama hilo swala langu.Ingependeza utoe jawabu kwa yote.
 
Kwanza hili si jukwaa la uzi wako. Ungepeleka kule biashara na uchumi.

Pili vocha ni malipo ya huduma unayoiomba. Maongezi au mbs. Kitendo cha kununua tu tayari imeshabadilika kuwa thamani ya pesa. Ulitakiwa kuuliza ni mtiririko gani/upi unafanyika/kupitia katika uuzaji wa vocha.
 
Tusipende saana kubeza maswali ya watu ila tushauri tu kuiweka kwenye jukwaa husika, swali alilouliza lina maana kabisa lakin inabidi aelezwe ki standard two aelewe msimpe maelezo ya vyuo hahaha
 
kabisa au angeuliza mtiririko upi unafanya vocha kutumika kulingana na thamani ya hela uliyonunulia?

Pili ni swali lake zuri linaibua maswali mengine,
kwanini Vodacom au Airtel wasijiwekee mtaji mkubwa kupitia airtel money AU mpesa maana wana uwezo wa kuongeza float kwenye laini zao , na kwanini wasifanye hivyo wakajiweka matrilion wakaenda ku draw , au kuna anaye monitor hizo floats ? mambo haya angeyauliza yangemsaidia ,
 
Hyo vocha ni sawa umenunua huduma kama huduma nyingne mkuu sema hyo unakua ni self service hakuna haja ya kujiulza sijui inabadrishwa vipi kuwa pesa.
 
Hili swali ni la msingi sana, na wenye uwezo wa kulifanyia kazi ni mitandao ya simu...

Kuna siku nilitaka kununua muda wa maongezi wa elfu tano bahati mbaya nikaandika elfu hamsini.

Shida ilikuwa jinsi ya kurudisha hiyo elfu arobaini na tano kwenye Mpesa...ilishindikana ..

Hata matumizi yake sikuelewa imetumikaje hadi kuisha.
 
Vocha ni huduma inayoweza kutolewa kwa kusajili number. Huduma yoyote inayoweza kupatikana kwa njia ya kusajili na kutambua number kwenye karatasi huitwa vocha. Ndio maana hata kwenye pembejeo kuna vocha.
 
Kwa upande wa mitandao ya simu, vocha huandaliwa kwa kusajili number na kuipa thamani. Thamani ya vocha ni mlinganyo wa muda au kwa kimombo tuseme "It is a function of time) huku coefficients zikiwa ni eneo ulipo au alipo mteja wako na aina ya mtandao unaoupigia.
 
Vocha ni kama kuponi unalipia kupata huduma fulani kwenye mtandao ukinunua vocha ya buku mbili umelipia huduma ya buku 2 kama ni daki sms au bundle kwa kifupi vocha ji bidhaaa kama bidhaa nyingine ila hii ni kwa kukupa huduma.service.
 
Tusipende saana kubeza maswali ya watu ila tushauri tu kuiweka kwenye jukwaa husika, swali alilouliza lina maana kabisa lakin inabidi aelezwe ki standard two aelewe msimpe maelezo ya vyuo hahaha
Heri wapatanishi maana.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom