Hivi vitu wanavyovalishwa Watoto Wachanga wa Kiafrika mikononi, viunoni na miguuni mbona navitafuta kwa wa Kizungu sivioni?

Kama hujawahi kupata tatizo ambalo hata vipimo vya kidayansi havitoi majibu ndo utadharau mila.remember mila zipo bfor science
Nikuulize swali Kwa nini unaenda hosp ikiwa Mila zilikuwapo kabla ya science, wewe Neno science kwako linamaanisha nini? Hata Mila ni sayansi pia. Kuna mila gani ktk kumchora Mtoto na wanja Kwa lengo la kumkinga na kama ni Mila mbona unasahau kuwa wanja umetoka kiwandani? Cheza na akili yako mwenyewe, hakuna kitu chochote kuvalisha Mtoto mahirizi kiuononi, mikononi alafu akigua tunakuta tena hosp ili Hali anakinga, achana na hizo habari mlishe Mtoto chakula Bora, maji salama, mahali salama pa kulala, akiugua haraka mpeleke hosp that is it. Hiyo ndo hirizi tosha.
 
Kuna Mama Mmoja nilimkuta Kamvalisha Mwanae na nilipojaribu Kumuelimisha kwa Kumuambia kuwa huo ni 'Upuuzi' na kutaka Kumvua alinitishia kuwa nikithubutu tu nakuwa Chura Maji muda huo huo nikasalimu Amri.

Nashukuru Mungu sikuvalishwa kabisa.
Vile naviitaga ving'amuzi haha haaaa
 
Ni kweli sisi tuko gizani hatuna elimu ndo maana hatuna akili.mfano mtu mnene kafariki ghafla kijijini kumbe alikuwa na pressure ila kijiji kizima wataamini kalogwa na huku hawajampima chochote

Akili na Elimu ni vitu viwili tofauti kabisa.

Kuna kipimo cha kutambua aliyerogwa?
 
Back
Top Bottom