Hivi vita ya kupambana na madawa ya kulevya imeishia wapi?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,815
20,660
Hivi karibuni tulishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akianzisha kwa kasi ya ajabu vita dhidi ya madawa ya kulevya, huku akiapa to leave no stone unturned.Wananchi tulifurahi na tukaamini kwamba sasa tutapata suluhisho la kudumu la tatizo la madawa ya kulevya ambalo limeharibu maisha ya vijana wetu wengi na hata kugharimu maisha yao.Hata hivyo katika hali ya kushangaza na isiyotegemewa,vita dhidi yake ikaanza hata kutoka kwa watu ambao walipaswa kusaidia katika vita hiyo.Naamini kwamba vita dhidi ya Makonda ilianzishwa na wauzaji wa madawa ya kulevya ili kufisha juhudi zake katika vita hiyo. Vita dhidi ya Makonda ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na Makonda alifikwa na adha isiyoweza kutamkika.Hata hivyo ili kuendeleza vita hii, Serikali ilichukua juhudi za makusudu kabisa za kuendeleza juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kumteua Kamishna mpya wa Kuzuia na Kupambana na Madawa Dawa za Kulevya,Kamanda Rogers Sianga.

Katika hali ya kushangaza pamoja na ahadi nyingi za serikali na Kamishna Robert Sianga mwenyewe kwamba adhma ya kupambana na madawa ya kulevya ipo pale pale, siku zinavyo zaidi kwenda inaelekea kwamba kuna jambo haliko sawa katika vita hii na kwa kweli juhudi hizo zimefifia kama ilivyotegemewa.Waliokamatwa kuhusiana na sakata hilo hatuoni wala kusikia chochote dhidi yao. Ndio Shikuba na wenzake wamekamatwa na kupelekwa Marekani,lakini hili lilikuwa ombi la serikali ya Marekani!Je,tuamini kwamba serikali inasita kujikita kikamilifu kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa kuwa serikali itatikisika kama ilivyodaiwa na serikali ya awamu ya nne?

Chonde Chonde viongozi wetu,vijana wetu wanaangamia, kete yetu ya mwisho ni ninyi,tusaidieni katika hili.

.
 
Tukujibu tu hii part ya kimya kimya ila nazani tunaona tunavyozidi kupoteza watu kwa madawa inatisha kwa kweliii
 
Mkuu
Ukitaka kufanya jambo jema sharti na ww uwe msafi. Huwez kutoa pepo wakati unapepo, hiyo haipo.
Hii ilikuwa hiv mwizi wa pikipiki anawakamata wezi wa bajaji. Hapo unafikiri zoez litafanikiwa?
 
Tukujibu tu hii part ya kimya kimya ila nazani tunaona tunavyozidi kupoteza watu kwa madawa inatisha kwa kweliii
Unajua hii vita ni nzuri ya kupambana na madawa ya kulevya ila mtu aliyekuwa anasimamia alikuwa mchafu. Kupitia uchafu wake ndiyo watu wakapata nguvu ya kumdhoofisha. Ni sawa na mtu ametoka kunywa pombe halafu anakemea pepo, utakesha. Hakuna mafanikio.
Mkuu hata km ndiyo ww unatoa hukumu ya kifo kwa wahalifu halafu una makosa ya kubaka lazima ushindwe tu. Ndiyo yaliyomtokea mkuu wenu. Jiwe mmoja tu chali, sasa hiv kawa km priton. Anatumbua mimacho. Juz juzi alikuwa na wanabongo movie wakiandamana.
 
Madaraka ya kulevya chalii daudi Albert bashite ile ilikua vita ya kuchukua mali kwa matajiri kwa kuwasingizia wauza ngada
 
Back
Top Bottom