Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Baada ya kuwa mwangaliaji wa muda mrefu kuhusu masuala ya ufisadi, ningependa kusema kuwa hakuna kitu kinachoitwa vita dhidi ya ufisadi.
Haya ni maoni yangu binafsi na sina nia ya kuwakatisha tamaa wapiganaji au kuwafagilia mafisadi. Na maoni yangu yanatokana na ukweli kuwa vita vyovyote ni lazima viwe na viongozi, wapiganaji, mbinu za upiganaji na malengo ya kupigana vita hivyo.
Sasa tukija katika vita vya ufisadi, sioni viongozi wowote ambao wanaweza kuunganisha umma na wapiganaji hili kufikia malengo hayo. Mpaka sasa sijaona kiongozi yoyote anayekubalika.
Kuhusu wapiganaji. Hiki pia ni kikwazo. Wapiganaji wengi wanapigana vita vya mtu mmoja mmoja. Kwa maana kwamba kila mtu yupo tayari kutoa mawazo yake kwa kupitia waandishi wa habari, internet forums, blogs lakini hakuna nguvu ya pamoja. Hivyo muda mwingi unatumika kutoa new big ideas katika vyombo vya kutoa habari.
Mbinu zinazotumika ni zilezile wanazotumia mafisadi. Tena mafisadi wanazitumia kwa ufanisi mkubwa. Kwa mfano propaganda ni mbinu ambazo zinamlenga mlalahoi na sio profesa wa UDSM, au mchangiaji wa JF. Hivyo Makamba anaposema wanaopinga Serikali wanaona wivu kwa kukosa madaraka, anayemlenga ni mlalahoi ambaye siku ya uchaguzi ataipigia kura CCM. Hivyo wapiganaji walipo JF kuuliza elimu ya Makamba kutokana na kile alichosema ni kutojua uwanja wa mapambano huko wapi.
Malengo ya vita dhidi ya ufisadi ni finyu. Na kutokana na ufinyu huo, hata mbinu za kupiga vita vyenyewe zinakuwa na matatizo. Ufisadi unatokana na ukweli kuwa binadamu ni Greedy. Na njia pekee ya kupunguza greed ni kuwa na jumuia au taasisi zilizo transparent, zenye ku-check and balance uongozaji wa jumuia na zenye kufuata sheria.
Wenu
Z10