Hivi viongozi wetu huwa mnajisikiaje juu wananchi kukosa maji safi na salama tangu Nchi hii ipate uhuru?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,530
3,435
Naandika kwa masikitiko makubwa kwa sababu hali ni mbaya. Wilaya ya Mbogwe ni Wilaya moja wapo katika mkoa wa Geita na ipo karibu na Ziwa Victoria ila haijawahi kugusa maji safi na salama kutoka bombani tangu mwaka 1961 impala leo.
 
Wanajisikia vizuri sana ili next time wakati wa kampeni wawaambie "mkinichagua nitaleta maji ya bomba hadi ndani".

Imagine nchi hii pakiwa hapana tatizo la maji, huduma ya afya, barabara, na ajira.

imagine tutapigwa sound gani?
 
Naishi wilaya hiyo tena kusini,mashariki,kaskazini,magharibi kuna DHAHABU...yaan watanzania sisi bwana maji tunatumia meupe kama yana maziwa...! Alafu sijawah kutana na mwenyeji akisema kuhusu maj..wameridhikaaaa...arghhh
 
Tukutane Mang'ombe ili angalau tujadiliane kidoogo.
 
Wanajisikia vizuri sana ili next time wakati wa kampeni wawaambie "mkinichagua nitaleta maji ya bomba hadi ndani".

Imagine nchi hii pakiwa hapana tatizo la maji, huduma ya afya, barabara, na ajira.

imagine tutapigwa sound gani?
Umesema jambo la msingi sana, hata mimi huwa najiuliza hivi wabunge wazanzibar walioko kwenye bunge la jmt huwa wanawahidi nini wananchi wao.
 
Naandika kwa masikitiko makubwa wanakuwa sababu hali ni mbaya. Wilaya ya Mbogwe ni Wilaya moja wapo katika mkoa wa Geita na ipo karibu na Ziwa Victoria ila haijawahi kugusa maji safi na salama kutoka bombani tangu mwaka 1961 impala leo.
Ishu ya umeme, afya(hospital) na maji kama ningekuwa President ndani ya mwaka mmoja tu ningepunguza au kumaliza kabisa naumia sana watu kukosa huduma muhimu kama maji, umeme na hospital.

Umeme

Sielewi kwa nini umeme umekuwa kama anasa na roho huwa inaniuma nguzo zimepita kando kando na vijiji au miji lakini eti umeme hawajapewa kwa nini, shida nini nyie Viongozi mbona wabinafsi sana?

Maji

Nchi hii imezungukwa na vyanzo vingi sana vya maji kuanzia maziwa, chemchem mpaka mito kwa nini Wananchi wakose maji. Mwaka mzima maji yanatiririka kwenda baharini, maziwani na mabondeni lakin unakuta Wananchi mijini na vijijini hawana maji kwa nini nyinyi Viongozi manakuwa ovyo?

Afya

Hivi hatuwezi kweli kujenga hospital za kanda zikawa kama Muhimbili vifaa na majengo kwani kiasi gani?. Leo mtu wa cancer atoke Kigoma aende Dar ocean road hospital kweli tupo serious? Kwa kweli hapa roho ndio huwa inanichefua kabisa.
Tuweke nguvu ya kusomesha na kujenga hospital zenye viwango vya kimataifa na vifaa vipo tu na bei sio kali lakini Viongozi wapo tu

Binafsi hivyo vitu vitatu ndio vingekuwa vya kwanza kwenye utawala wangu na kwa miaka mitano walai ningemaliza vyote na kwa usahihi kabisa. Viongozi jaribuni kuvaa viatu vya wananchi kabisa.
Shida nini si mkakati tu wa mwaka mmoja matatizo haya yanaisha
Raisi Mama Samia na Makamu Mpango ivi hamuwezi fanya jambo kwa muda wenu kupunguza tatizo la maji, umeme na hospital kubwa kwenye kanda nchini mwetu kweli yani. Mfano nyie Viongozi mkiumwa sehemu ya kwanza kwenda Kenya au South Africa na hii tabia ni ya miaka mingi sana. Kweli tunashindwa kufanya ivi vitu hapa kwetu ?
Sitaki kuamini hili kabisa bora hata tukope hata mipesa kiasi gani lakini hivi vitu vimalizwe.

Ivi mnapogombea uongozi mawazo yenu yanakuwa ni nini juu ya Wananchi ??

Hii miradi ukiweka mkakati 2 trillion umemamliza aidha kwa kukopa au mapato ya ndani
 
Wanajisikia vizuri sana ili next time wakati wa kampeni wawaambie "mkinichagua nitaleta maji ya bomba hadi ndani".

Imagine nchi hii pakiwa hapana tatizo la maji, huduma ya afya, barabara, na ajira.

imagine tutapigwa sound gani?
Umesahau tulipigwa fix kuwa wataleta mvua ya kutengeneza?? Siasa = Uwongo mwingi + Ukweli kiduuchuu.
 
Karibu Lugunga kwenye mitumba ya kutosha ingawa wauzaji inasemekana ni warundi sijui waliingiaje pale kijijini.​
 
Back
Top Bottom