Hivi viongozi wa vyuo vya Elimu hawalioni hili kama tatizo.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Hivi karibuni wizara ya elimu ilitangaza tarehe 30 Aug 2017 kuwa siku ya mwisho ya wanaoomba kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kujisajili.

Wakati huo huo ka
una wanafunzi wa diploma wanaotegemea kufanya mitihani ya marudio (supplementary) kuanzia katikati ya mwezi Septemba 2017 na kuendelea na wakati huo huo wanatakiwa kujisajili kwa kozi za digrii vyuo vikuu. Hivi kwa utaratibu huu viongozi wa vyuo na wizara hawalioni hili kama ni tatizo linaloweza kuwapigisha maktaimu ya mwaka mzima wanafunzi hao bila sababu.

Kwani haiwezekani kupanga utaratibu ambao utawawezesha wanafunzi kufanya sup na kukawa na muda wa wao kujiunga na vyuo ndani ya muda maalum bila kuahirisha kujisajili vyuoni mwaka mzima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom