Hivi viongozi wa chadema wanataka kutuaminisha msaada wa nje ni bora kuliko wa ndani katika kupigania haki zao.

Na haka katabia kakupiga watu risasi na kukamata wapinzani nako ndio solution ya ( )
Kwani watu katika taifa hili wamepigwa risasi katika awamu hii tu. Ama nyie mnabagua watu; walipigwa risasi wakiwemo polisi mnaona sio watu. Baada muungane nguvu moja kupigana na hawa waharifu wanaopiga watu mnaleta porojo za kipuuzi. Ama nyie ndio mnatuma hao wanaopiga risasi
 
Ni sawasawa na na kesi ya mwizi umpelekee jambazi,, unataka washitaki ndani alafu polisi wakwambie Amri kutoka juu imesema msubiri
 
Wengi wanaotetea mfumo huu wa utawala wanafaidika nao...

Wengi wasiofadika nao wakilalamika wanaonekana si wazalendo.

Bunge halitimizi wajibu wake wa kusimamia Serikali ( wabunge wa upinzani wanapeleka hoja binafsi zinakataliwa)

Mahakama hazipo huru kihivyo kwa kuwa tumeona mhimili wa utendaji ukisigina Katiba lakini mihimili wa Haki unaona haya kuhukumu vinginevyo.

Njia zote za kujaribu kupata haki zimebinywa ukiwamo uhuru wa kupata na kutoa Habari.

Vyama vya upinzani marufuku kufanya siasa za wazi.

Hivi Nyie mnataka watu wafanye nini? Mnataka waitishe maandamano risasi za moto zirindime?
Kiongozi mbona kuna mashauri mengi serikali inashindwa katika mahakama za Tanzania. Ana wepesi kusahau mashauri mnayoshinda mnashangilia. Au hamlioni. Hoja za upinzani zipi zilizotupwa na Bunge. Be specific tuzijue. Pia je hoja hizo zimekataluwa na wananchi.
 
Kuna katabia kanaonekana kutaka kuota mizizi kwa viongozi wa chadema kutumia vyombo vya nje kuichongea serikali na taifa la Tanzania kwa mambo wanayoyaona hayaendi sawa. Je hiyo nguvu inayotumika kuchongea serikali nje inatarajiwa kuleta neema kwa watanzania ama manufaa gani kwa watanzania. Tumeona juhudi za viongozi wakitaifa wa chadema akiwemo Mbowe; Lisu na baadhi ya wabunge wakitumia nguvu nyingi kama kuishtaki serikali ya tanzania kwa vitu wanavyoona haviendi sawa badala ya kutumia watu wenye maamuzi ya mwisho kwa taifa hili. Kuna mitazamo tofauti inayoendelea ikiwemo kuiona chadema kukosa muelekeo na kujikita na juhudi za kutaka kuvuruga tanzania; na wengine wakiona chadema wako sahihi ili mashirika ya nje yaingilie kati. Je kwa mikakti ya kutumia vyombo vya nje chadema itatoboa kweli?
Naomba kuwasilisha. Tutambue Tanzania ndio taifa pekee tulilopewa na Mungu.
Watawala kandamizi hupunguzwa nguvu zao kwa kukatiwa mahusiano na nchi nyingine...Kukosa ushirikiano na mataifa mengine "kunaziba pumzi" ya serikali dhalimu
 
Mataifa ya nje yaliwasaidia wapinzani kuwaondoa viongozi kama Muammar Gaddafi, Hosni Mubarak na Saddam Hussein.
Kaangalie kinachotokea katika mataifa hayo utajua hizo haki unazozitaka kama wanazipata. Hukuona clip ya watu wakifanywa watumwa katika moja ya hayo mataifa.
 
Kuna katabia kanaonekana kutaka kuota mizizi kwa viongozi wa chadema kutumia vyombo vya nje kuichongea serikali na taifa la Tanzania kwa mambo wanayoyaona hayaendi sawa. Je hiyo nguvu inayotumika kuchongea serikali nje inatarajiwa kuleta neema kwa watanzania ama manufaa gani kwa watanzania. Tumeona juhudi za viongozi wakitaifa wa chadema akiwemo Mbowe; Lisu na baadhi ya wabunge wakitumia nguvu nyingi kama kuishtaki serikali ya tanzania kwa vitu wanavyoona haviendi sawa badala ya kutumia watu wenye maamuzi ya mwisho kwa taifa hili. Kuna mitazamo tofauti inayoendelea ikiwemo kuiona chadema kukosa muelekeo na kujikita na juhudi za kutaka kuvuruga tanzania; na wengine wakiona chadema wako sahihi ili mashirika ya nje yaingilie kati. Je kwa mikakti ya kutumia vyombo vya nje chadema itatoboa kweli?
Naomba kuwasilisha. Tutambue Tanzania ndio taifa pekee tulilopewa na Mungu.
Kwani hujui kuna vitu jamii ya kimataifa lazima iingilie kati?hasa haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza?
 
Kiongozi mi sijawahi kuona kiongozi yeyote wa Uingereza; Russia; Kenya wakitumia vyombo vya nje ya taifa lao kusema vibaya taifa lao.
Unaweza ukawa sahihi, lkn pia jiulize wapinzani wa nchi hizo wanafanyiwa kama wa kwetu?
Mm binafsi issue ya Lissu kama binadamu inauma sana.
 
Ilishasemwa "ishu sio ubora" bali usalama, unahudumiwa na anayetaka ufe, what do you expect?
 
Unaweza ukawa sahihi, lkn pia jiulize wapinzani wa nchi hizo wanafanyiwa kama wa kwetu?
Mm binafsi issue ya Lissu kama binadamu inauma sana.
Ishu ya Lisu ni jinai jamani muelewe. Tatizo mmeingiza siasa katika lile tukio. Watu ambao wangewezesha kutoa preliminary ingormation hasa mtu kama dereva wanamficha hivi inatia akilini kweli. Tunataka uchunguzi ufanikiwe taarifa za mashahidi namba moja ni muhimu mno kuliko siasa tulizoingiza
 
Uwezo wako wa kufikiri mdogo sana. Walipata msaada wa kuondoa utawala WA kikoloni si utawala wa taifa huru.
Unajua maana ya uhuru wewe? Nchi huru inaongozwa kidikteta na watu kupotea na kupigwa risasi kwa sababu tu ya kutoa maoni yao ambayo ni haki yao kikatiba? No wonder umeitwa punguani na wengi humu
Watawala kandamizi hupunguzwa nguvu zao kwa kukatiwa mahusiano na nchi nyingine...Kukosa ushirikiano na mataifa mengine "kunaziba pumzi" ya serikali dhalimu
 
Kaiuulize familia yako na sio watanzania wapenda haki na wanaoheshimu katiba.
 
Kuna katabia kanaonekana kutaka kuota mizizi kwa viongozi wa chadema kutumia vyombo vya nje kuichongea serikali na taifa la Tanzania kwa mambo wanayoyaona hayaendi sawa. Je hiyo nguvu inayotumika kuchongea serikali nje inatarajiwa kuleta neema kwa watanzania ama manufaa gani kwa watanzania. Tumeona juhudi za viongozi wakitaifa wa chadema akiwemo Mbowe; Lisu na baadhi ya wabunge wakitumia nguvu nyingi kama kuishtaki serikali ya tanzania kwa vitu wanavyoona haviendi sawa badala ya kutumia watu wenye maamuzi ya mwisho kwa taifa hili. Kuna mitazamo tofauti inayoendelea ikiwemo kuiona chadema kukosa muelekeo na kujikita na juhudi za kutaka kuvuruga tanzania; na wengine wakiona chadema wako sahihi ili mashirika ya nje yaingilie kati. Je kwa mikakti ya kutumia vyombo vya nje chadema itatoboa kweli?
Naomba kuwasilisha. Tutambue Tanzania ndio taifa pekee tulilopewa na Mungu.
Angalia ITIKADI ya CDM katika Katiba yao (2006) Sura ya 3.B.

Ukiisoma utaona lengo lao ni kuiuza hii nchi kwa mataajiri wa nje. Hata ardhi itataifishwa. Hii ni hatari kwa nchi yetu zaidi ya ufisadi, rushwa, watumishi hewa, ukwepaji kodi kwa pamoja.

Lengo la CDM ni kuikabidhi nchi kwa mabepari (wengi wa nje) waiendeshe.

Itikadi yao inajulikana kama NEOLIBERALISM. Itikadi hii ni hatari sana na ndio inayoiingizia Marekani umasikini kwa kasi kubwa sana. Unaweza kuisoma hii itikadi hapa chini.

Neoliberalism - Wikipedia

Ndio maana kila mara unawaona CDM wanakimbilia nje kuomba msaada wa kuiangusha serikali ya Magufuli.

Hawa watu ni hatari sana.

Unafikiri UFISADI ni mbaya, subiri mpaka CDM washike dola. Watanzania masikini watageuka kuwa watumwa nchini mwao.
 
Unajua maana ya uhuru wewe? Nchi huru inaongozwa kidikteta na watu kupotea na kupigwa risasi kwa sababu tu ya kutoa maoni yao ambayo ni haki yao kikatiba? No wonder umeitwa punguani na wengi humu
Ukikua utaelewa. Naona hujielewi. Hujajibu hats hoja. Rudia kusoma ujibu swali
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom