negotiator nodegi
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 403
- 127
Ni ushamba!! tu kwenda mbele, kwanza kama rais tunaamini yuko well informed kuliko mtu yeyote hapa nchini kwa resources alizonazo haiingii akilini rais kutojua changamoto walizonazo watanzania mpaka akutane na makundi mbalimbali..ni ushamba tu aisee!Rais Magufuli must stop goofing around - atumie vizuri muda wake kufanya kazi, not to waste the time of busy people...Mara nyingi nimekuwa nikikaa kumsikiliza tangu anapoanza kuhutubia hadi anapomaliza I am sorry kusema sikumbuki kama kuna wakati wowote amewahi kuniongezea maarifa mapya - anazungumza vitu obvious, bare facts na anakwepa pressing issues...
Hii mikutano yake na makundi mbalimbali haina tija yoyote....hivi honestly anahitaji kukutana na mtu yeyote kuelewa kuwa nchi ina matatizo lukuki? Doesn't he read? Kama hasomi hata kusikia hasikii? Au anawaita tu kutafuta some sympathy kwa makosa lukuki ya miaka mitatu ya uongozi wake ambayo sasa anaona ni vigumu kuyasahihisha?
Kama alikwishaandikiwa nyaraka RASMI za Kiuaskofu na hakuelewa issues zilizokuwa raised badala yake akaishia kutishia kufuta makanisa na kuwanyang'anya Maaskofu hati zao za kusafiria na kuhoji uraia wao, anahitaji vikao vingine na hawa viongozi asikie nini kipya? Anataka kusikia wanavomsifia UONGO?
Kama ameshaandikiwa na EU na US na wadau wengine na bado hajajua issues ambazo ziko raised anahitaji kukutana na makundi mengine ili asikie nini?
Kama mtu keshakutana na wafanyabiashara katika mabaraza yao na bado haelewi kuwa nchi inakabiliwa na matatizo lukuki katika uongozi wake na hoja zao hajazifanyia kazi anahitaji vikao vingine ili ajue nini?
Kama mtu ameshakutana na wasanii na bado haelewi kero zinazoikabili nchi anataka asikie kitu gani zaidi?
Ma-DC na ma-RC wake ni kero kubwa na wamejenga chuki kubwa kwenye jamii na ameelezwa countless times hasikii wala haelewi, anahitaji vikao hivi kila siku on live TV ili asikie kitu gani kipya?
Three years mtu bado haelewi matatizo ya nchi, like seriously?
Sent using Jamii Forums mobile app