Chakaza unaamini kwa dhati kwamba lowasa ni mtu sahihi wa kusimamia mabadiliko unayoyahitaji tangu hiyo 1997 ulipojiunga na chadema?!Mkuu uko sahihi, nimejiunga JF 2007 nikiwa ndani ya Chadema kwa miaka 10, yaani nilijiunga nayo 1997. Ups and downs za Chadema kama taasisi nazielewa na kuzikubali. Lakini pia CCM naifahamu vizuri kwani nimekuwa mtumishi Wa umma kwa miaka mingi kabla sijaachana na utumishi huo.
Naifahamu ccm ya Nyerere hadi hii ya Magu tena pengine kuliko hata hao walio ndani yake na kwa vyeo vya juu. CCM kila Siku iendayo mbele inakuwa nafuu Jana kuliko Leo.
Sasa kwa vile sitegemei kula Yangu na familia katika siasa kwa nini nijikombe Kule ambako "nafuu Jana kuliko Leo?"
Hakika kwa hawa vijana wasio jua, ni kwamba ccm ya sasa ni mbovu kabisa kuliko wakati mwingine wowote. Kama unaona wakina Kitila, Masha nk wanaenda huko na wanataka kujua ukweli kwa nini wanaenda kwa mbwembwe wawaite pembeni na kuwashikisha misahafu waape na kusema kweli. Watajibu "MASLAHI TUU"
Naamini Mungu atanijalia niishi mpaka nione ccm ikiondolewa na wale wanaotenda mambo mabaya kama yale ya Lissu, Saanane, Mawazo nk wakionyeshwa hadharani na kupata haki yao. Pia watu wote wakifaidi Neema ya nchi yao.
Siku hiyo yaja na haiko mbali