Hivi uzalendo ni kufanya kazi bila malipo? Au uvumilivu usio na kikomo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi uzalendo ni kufanya kazi bila malipo? Au uvumilivu usio na kikomo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Jan 8, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo mara yangu ya kwanza kushangazwa na hii sirikali ya JK wa pili. Hivi kwa nini watu wanakosa utashi wa kufanya mambo kwa akili zao na badala yake wanafanya kazi kwa kutumia akili za watu wengine? Mtu kama JK hivi kweli anafanya adha ambayo watu wanaipata kwa kukosa huduma za madaktari pale muhimbili?

  Au anafanya hivyo kwa sababu hakuna ndugu yake ambaye anatibiwa MNH? Watu wanafanya kazi kwa kujituma kutoa huduma kwa mioyo yao yote halafu hawapati malipo kisha wanaambiwa wawe wazalendo.


  Najiuliza, Uzalendo ni kufanya kazi bila malipo? Au ni kufanya kazi kwa uvumilivu usio na kikomo?
  Kwa nini hili suala la Uzalendo linaelekezwa kwanza kwa wanfayakazi wa sekta za umma, kama madaktari, waalimu, polisi na wengine wengi? Kwa nini viongozi wa kuu wa serikali kama rais, waziri mkuu wake na wabunge siyo wazalendo? Au wao siyo watanzania?

  Au wabunge wakiongozwa na Bi Kiroboto kudai posho za 200000/- ndiyo uzalendo? Mbona sijasikia rais kutaka kupunguza mshahara wake kuonesha uzalendo? Mbona sijasikia mawaziri wakakataa kutumia mashangingi ili kuokoa gharama kubwa za uendeshaji wa magari hayo ili kuelekeza fedha hizo kwenye huduma mbalimbali za jamii, au wao siyo Watz?

  Naamini, kuna siku haya yote yataisha na tutaipata Tanzania yetu iliyopotelea kwa mafisadi wa CCM. Haya yatatokea tu kama wote kwa pamoja tutachukua hatua kwenye sanduku la kura.
   
 2. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hivi nini kinaweza kutuonyesha kuwa JK yeye ni mzalendo???
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kitendo cha wananchi kukaa kimya dhidi ya manyanyaso kwa watumishi wa umma ndio sumu inayoliua taifa taratibu.leo hii walimu au madaktari wanalalamikia maslahi yao ili waweze kuwatumikia wao wapo kimya.ndio maana watumishi wa umma huamua kukaa kimya na kupeleka nguvu zao kwenye ufisadi na rushwa.
   
 4. u

  utantambua JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Uzalendo ni kutohoji haki zako, kukubali kucheleweshewa mshahara na stahili zako na kushangilia ongezeko la posho za wanasiasa.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mim ntaufafanua uzalendo in my head kwa harakat za mkwawa na wazee walopigania uhuru,
  pia ukii0na documentary ya ujenz wa reli ya tazara,utaweza kuelewa uzalendo ni nin?
  It meanz c kwa mujibu wa kauli za wadau wa sasa
   
Loading...