mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Habari wana Jf
Kwanza naomba niweke nukuu kwa magufuli aliyosema jana;
"Kodi zikiwa chache na viwango vikiwa vidogo biashara inastawi, kinyume chake biashara hudumaa, hii ndio sababu tumeanza kuchukua hatua za kupunguza viwango na utitiri wa kodi" magufuli
Niseme tu kuwa mambo haya ya kodi yamesemwa tangu mwaka 2016.
Siku zote, tulipokuwa tunasema watendaji wanaomzunguka Magufuli hawamwambii ukweli wa hali halisi ya mambo, makada wa CCM na raia wa ambao wapo huu Jf walikuwa wanatushambulia na kutuita wapinzani wa maendeleo na vibaraka wa mabeberu. Tuliitwa “wa ufipa” hata kama si wanachama wa vyama!
Ukiwa na fikra chanya na uwezo wa kutoa changamoto unaonekana mpinzani,Walisema wafanyabiashara wanaolalamika sasa hivi hali mbaya waliambiwa walizoea ufisadi kipindi cha kikwete.
Wakati Biashara zinafungwa mawaziri walikuwa wanasema kuwa wanaofunga ni wapiga dili. Jana nimeshangaa kuona eti Rais anashangaa kwanini Biashara zinafungwa. Eti na maagizo yanatoka kuwa TRA isifunge Biashara za Watu sababu za Kodi. Biashara zaidi ya 2000 zimeshafungwa!
Kwa moyo wa dhati kabisa napenda kuwapongeza wakosoaji wote na muendelee na kasi ya ukosoaji. Hili la kuyumba kwa sekta binafsi na mazingira magumu ya biashara mmelisema pamoja na kejeli kwa wale wasiopendezeshwa na ukosoaji wenu.
Kauli mbiu: UKOSOAJI NDIO SILAHA YA MAENDELEO.
mr mkiki.