mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Nimeamini CCM ni ile ile.Nilitegemea Askari wa Miamvuli wa Rais wetu Mh.Magufuli ungekuwa Na sura , zenye nguvu, mawazo mapya hazina kashfa zozote ili waendane Na kasi yake.Lakini imekuwa kinyume Na matarajio ya watanzania.Tunashuhudia waliokuwa viongozi ambao wapiga kura walituthibitishia kuwa hawana uwezo Na kutowachagua Leo ndio Mawaziri, mabalozi Na wakuu wa mikoa.Kuna kundi jingine la watu ambao wameitumikia serikali Na kufika ukomo Kwa kustaafu Kwa maana ya kupumzika Na kupisha wenye umri mdogo lakini Leo ndio wanateuliwa kushika nyadhifa mpya.Tunamwomba Mh.Rais atufikirie Na sisi vijana kama tuna sifa Na CV .anazozihitaji atuteue Na hao waliomaliza muda wao wa Utumishi wabaki washauri kwani busara zao zinahitajika tena katika maeneo yao.